Ni muda muafaka sasa kwa Tume ya Ushindani Tanzania FCC kulimulika swala la uwekezaji wa Mo Dewji Simba

Mkumbushe jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikiongozwa na Ali Hassan Mwinyi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiongozwa na marehemu Idrisa Abdul Wakili miaka Ile ya mwishoni mwa 80s zilivyoingilia katika hukumu ya Mahakama ya kulipigia mnada Jengo la klabu ya Yanga kutokana na madeni sugu.
 
Hekaya za abunuasi na stori za ESOPO ZINAENDELEA
 
Hajui lolote huyo, anabwatabwata tu, ulishasikia tena hilo deni?
 












Simba SC ni moja kati ya timu nne kongwe kabisa hapa nchini ikianzishwa mwaka 1936 jijini Dar es salaam. Zingine ni vinara Yanga SC 1935, African Sports 1936 na Coastal Union 1938.

Simba imepitia majina mengi toka kuanzishwa kwake mpaka sasa. Ilipoanzishwa mwaka 1936 iliitwa Queens jina lilidumu mpaka mwaka 1948 walipofanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza na wakati huo mkoa wa Pwani ulianzisha ligi maalumu iliyokuwa ikijiendesha kwa misingi bora ya kisasa.

Wakati huu ndio Simba ilianza kupata ufadhili unaoeleweka mfano jezi nzuri za kisasa na viatu wakati wenzao wakiwa bado wakilisakata kabumbu peku peku .

Simba walibadilishwa jina na kuitwa Eagles baada ya kuonekana jina la Queens linawaletea kebehi kwa watani wao wa jadi Yanga SC ambao kabla ya mwaka 1930 walijulikana ‘ New Young ‘.

Jina la Eagles yaani tai kwa lugha ya kiswahili halikudumu sana. Lilikaa kwa muda mchache sana na kubadilishwa kuwa Sunderland.

Hili ndio jina ambalo wengi wanalifahamu sana . Ni jina ambalo wekundu hawa wa msimbazi wana kumbukumbu nalo kubwa na ndefu kidogo.

Baada ya nchi kupata Uhuru mwaka 1961 na miaka minne baadae kuanzishwa ligi daraja la kwanza yenye sura ya kitaifa yaani ligi iliyoshirikisha timu zote za bara na visiwani, Sunderland ndio ilikuwa timu ya kwanza kubeba kombe la ligi hiyo mwaka 1965 na kulitetea tena kombe hilo mwaka 1966.

Hivyo katika historia Simba SC wakitumia jina la Sunderland waliweza kunyakua ubingwa wa ligi daraja la kwanza mara mbili kabla ya jina hilo kufa mwaka 1971 baada ya raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Karume kuwashauri kubadili jina kwa sababu ya maudhui yake kikoloni na ndipo jina la Simba SC lilipozaliwa.
 
Sasa kosa liko wapi Mo kumuweka babra kisimamia maslahi yake pale simba? Nyie wapiga zumari tushawazoea mikelele yenu wakati hamna hata mia mfukoni
 
SAWA ILA HAWATAKUELEWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…