Ni muda muafaka sasa TRA mtoke hadharani mtuambie hayo mabango yenye picha ya Rais nchi nzima nani anayalipia na yanaingiza kiasi gani

Mkuu ni muhimu ufafanuzi upatatikane, maana kweli kuna mkanganyiko hapa!!!
 
yaani mabilioni ya ruzuku inayopokea CCM yanakaa tu kwenye akaunti za chama right? ndivyo unavyoelewa πŸ’

lakini pia,
wizara na taasisi mbalimbali za kisekta, zinawajibika kuujulisha umma kazi na miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Rais, comrade Dr Samia Suluhu Hassan tayari ameshaifanya kwa umma wa makundi mbalimbali popote nchini..

Mabango unayoyaona ni sehemu ya kuujulisha umma wa waTanzania na kuweka wazi namna ambavyo, ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi 2020-2025 inatekelezwa kwa waTanzania.

kumbuka ilani ni mkataba wa kazi kati ya wananchi na chama husika, ili itakapoundwa serikali itumike kama formula ya kazi katika kuwatumikia wananchi.....

so,
mabango unayoyaona kote nchini yanaweza kugharamikiwa na chama Tawala, wizara, taasisi au mamlaka yoyote ile ya serikali ambayo inawajibika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM πŸ’
 
Hayo mabango yananichekeshaga 🀣🀣🀣🀣
Wananchi mmegoma kuelewa, sasa mnalazimishwa.
 
Huyo huyo kwenye picha ndio Top wa TRA.

Tule chuma hicho Mwaisaa..
 
πŸ†—
 
Upon nje ya mada, tunajua mabango yote yameidhinishwa, tunataka kujua nani anayalipia hayo mabango?
Na kuna umuhimu gani wa serikali kusambaza mabango ya raisi nchi nzima utazani ni chama kinapiga kampeni??
 
Mkiwa mnaambiwa msikilize bajeti mnakaa vijiweni kuongelea Mo na GSM ndiyo madhara yake haya. Simba na Yanga zinapoteza sana watu mpaka akili inahamia miguuni. Toka lini ukasikia mabango ya kisiasa yanalipishwa kodi? Iwe Chamadema,CUf sijui ni CCM ,ACT hakuna bango lao hata moja litalipishwa kodi sababu sheria inasema mabango ya biashara nenda kajifunze siyo kuja leta taarifa za uongo. Pili hao unaowaita tra hata tafuta mwanasheria atakuambia hawakusanyi kodi za mabango kasome tena uje na lalamiko lako lisilo na kichwa kama wewe mwenye kichwa maji. hata kuingia tovuti ya tra umeshindwa na kusoma. Nimechukua dakika kumi tu nimesoma na kuona kodi zipi wanakusanya za mabango hawakusanyi katafute data uje tena au njoo inbox nikusomeshe bwege wewe. hapa chuki yako ni kwa raisi au tra? maana mara tra mara picha ya raisi huyo ni raisi utake usitake mpe heshima na nafasi yake kasuku wewe.
 
Wewe umechukua dakika kumi kusoma kama tra wanalipisha mabango, Mimi Nina mabango ninayolipia tra na mengine nilishindwa nikayatoa, tra ndo wanakadiria na kukusanya Kodi ya mabango
 
Wewe umechukua dakika kumi kusoma kama tra wanalipisha mabango, Mimi Nina mabango ninayolipia tra na mengine nilishindwa nikayatoa, tra ndo wanakadiria na kukusanya Kodi ya mabango
Tatizo mgumu kuelewa mabango yako ni ya biashara na tra hawalipushi hii ni tozo zipo halmashauri mabango ya kisiada hayatozwi kodi sababu hayaingizi mapato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…