Ni muda sasa wa kubadilisha jina la timu ya Taifa na kuipa nembo

Ni muda sasa wa kubadilisha jina la timu ya Taifa na kuipa nembo

Unaweza kutufokea, kutugombeza, kututukana, kutudharilisha na kutubeza hapa kila siku, kila saa, kila dakika.

Ila mwisho wa siku kuna kitu kimoja tu kitabaki kuwa kweli.

Kitu hicho ni hiki;
JINA HALISAIDII CHOCHOTE.

Unataka kutuambia timu ya taifa ya wanawake inafanya vizuri kwa sababu inaitwa TWIGA Stars ?

Ile ya vijana inafanya vizuri kwa sababu inaitwa SERENGETI Boys ?

Na ile nyingine ya Tanzania bara inafanya vizuri kwa sababu inaitwa KILIMANJARO Heroes ?

Au unataka tubadili jina kwa sababu za kihistoria na "kutangaza utalii", na sio kwa sababu za kimpira ?

Tunaweza kuiita vyovyote vile, ila mwisho wa siku JINA HALISAIDII.

Tuiite Rufiji, Malagarasi, Makinikia, Mwalimu Nyerere, Mkwawa, Kinjekitile, Pweza, Nyumbu, Makaa ya mawe, Tamisemi, Oldonyo Lengai Uzalendo, Kisiwa cha amani, n.k bado jina halitasaidia chochote.

Timu ikiwa na uwezo itafanya vizuri tu hata kama jina lake ni ZUBEDA, UYOGA au NANJILINJI.
Umemjibu vizuri sana huyu Mataga,anafikili hata yeye alubadili jina lake akajiita Azam ndiyo atapata mafanikio
 
Timu yetu ya Tanzania ambayo inajumuisha Bara na Visiwani.... Feitoto inapitia kipindi kigumu sana. Ukiangalia karibu nchi nyingi za Afrika timu zao zina majina ya tofauti.

Mfano Rwanda ama Msumbiji kuna Amavubi na Mamba.

Sisi huku ni Taifa Stars... hakuna hata nembo inayowakilisha nchi yetu. Nigeria wanajiita Tai na wanaye hasa Tai.

Ni muda sasa wa kuachana na jina la Taifa Stars na kutafuta jina jipya huenda kutakuwa na mafanikio.
Tuiite The Girrafes!
 
Kwa namna inavyocheza tufute neno STARS kwenye jina la hii timu yetu ya taifa. Labda huko mbele ikija kuwa sawa na ya kisasa ndipo turejeshe hicho kipande kwenye hilo jina. Haiwezekani mtu kama Kibu Denis, Mzamiru,Kennedy Juma nao waitwe Stars!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa namna inavyocheza tufute neno STARS kwenye jina la hii timu yetu ya taifa. Labda huko mbele ikija kuwa sawa na ya kisasa ndipo turejeshe hicho kipande kwenye hilo jina. Haiwezekani mtu kama Kibu Denis, Mzamiru,Kennedy Juma nao waitwe Stars!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kibu kakosea nini? Mzamiru leo ni mkoja wa wachezaji waliocheza vizuri... kenedy kakosea wapi??
Tatizo lako nimeliona!!
 
Nimeshapendekeza hapo juu...
MBWA MWITU wa serengeti... THE WILD DOGS od Serengeti...
Wana sifa gani hao viumbe?
Kwa namna inavyocheza tufute neno STARS kwenye jina la hii timu yetu ya taifa. Labda huko mbele ikija kuwa sawa na ya kisasa ndipo turejeshe hicho kipande kwenye hilo jina. Haiwezekani mtu kama Kibu Denis, Mzamiru,Kennedy Juma nao waitwe Stars!

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuendekeza Usimba na Uyanga kwenye timu ya taifa.
 
Jina halileti matokeo kijana....Germany nikname yao ni nini au Brazil?
Jengeni misingi imara ya kuzalisha vijana tokea chini huko kwenye grassroot...pelekeni vijana wengi nje wakawe hazina ya baadae,hizi timu kubwa Africa karibu kila mwaka wanazalisha vipaji vipya kupitia diaspora...kupitia uraia pacha,Nchi yenu haitaki hivyo wewe unataka timu ibadilishwe jina.
Nchi zote zina nickname hadi hizo za ulaya, na America.

-Brazil wanaitwa Selecao
-Ujerumani wanaitwa Die Manschaft
-Uingereza Three lions etc

Taifa stars ni jina zuri ila Team za Vijana zina majina yenye identity zaidi kama Serengeti Boys, ama Nyengine kama wadada Twiga stars na timu ya Bara kilimanjaro stars.

Usifikirie jina kama kiwango, jina ni identity na pia ni opportunity kuitangaza Nchi, hasa kwa kitu ambacho ni unique kwa nchi husika. Imagine unafuzu mataifa Africa ama Kombe la dunia na Timu inaitwa Kilimanjaro stars, unafikiri watu watakuwa na Doubt tena Mlima kilimanjaro upo Tanzania ama kenya?

Nchi nyingi za Kiafrica wanatangaza vitu unique vya kwao, Egpty na Farao, Angola na swala wao, Nigeria na Tai, Morocco na simba, Senegal na simba pia etc.
 
huwa naona ni ujinga ati timu ya Taifa inaitwa Taifa stars, jina ambalo halitangazi chochote nchini zaidi ya kiswahili, wakati tuna vitu vingi kweli ivya kuvitangaza. angalia wenzetu wa cameroon walivyoipa jina la kutangaza vivutio vya utalii, na nchi zingine zenye akiliw amefanya hivyo. hili jina libadilishwe haraka, pengine ndo maana tunafungwa (kidding)
 
Back
Top Bottom