Ni muda sasa wa kubadilisha jina la timu ya Taifa na kuipa nembo

Umemjibu vizuri sana huyu Mataga,anafikili hata yeye alubadili jina lake akajiita Azam ndiyo atapata mafanikio
 
Tuiite The Girrafes!
 
Kwa namna inavyocheza tufute neno STARS kwenye jina la hii timu yetu ya taifa. Labda huko mbele ikija kuwa sawa na ya kisasa ndipo turejeshe hicho kipande kwenye hilo jina. Haiwezekani mtu kama Kibu Denis, Mzamiru,Kennedy Juma nao waitwe Stars!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibu kakosea nini? Mzamiru leo ni mkoja wa wachezaji waliocheza vizuri... kenedy kakosea wapi??
Tatizo lako nimeliona!!
 
Nimeshapendekeza hapo juu...
MBWA MWITU wa serengeti... THE WILD DOGS od Serengeti...
Wana sifa gani hao viumbe?
Acha kuendekeza Usimba na Uyanga kwenye timu ya taifa.
 
Nchi zote zina nickname hadi hizo za ulaya, na America.

-Brazil wanaitwa Selecao
-Ujerumani wanaitwa Die Manschaft
-Uingereza Three lions etc

Taifa stars ni jina zuri ila Team za Vijana zina majina yenye identity zaidi kama Serengeti Boys, ama Nyengine kama wadada Twiga stars na timu ya Bara kilimanjaro stars.

Usifikirie jina kama kiwango, jina ni identity na pia ni opportunity kuitangaza Nchi, hasa kwa kitu ambacho ni unique kwa nchi husika. Imagine unafuzu mataifa Africa ama Kombe la dunia na Timu inaitwa Kilimanjaro stars, unafikiri watu watakuwa na Doubt tena Mlima kilimanjaro upo Tanzania ama kenya?

Nchi nyingi za Kiafrica wanatangaza vitu unique vya kwao, Egpty na Farao, Angola na swala wao, Nigeria na Tai, Morocco na simba, Senegal na simba pia etc.
 
huwa naona ni ujinga ati timu ya Taifa inaitwa Taifa stars, jina ambalo halitangazi chochote nchini zaidi ya kiswahili, wakati tuna vitu vingi kweli ivya kuvitangaza. angalia wenzetu wa cameroon walivyoipa jina la kutangaza vivutio vya utalii, na nchi zingine zenye akiliw amefanya hivyo. hili jina libadilishwe haraka, pengine ndo maana tunafungwa (kidding)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…