De Opera
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 780
- 1,664
By De Opera ,
Ni takribani miaka minne, tumeona klabu ya soka ya Simba ikifanya vizuri mashindano ya kimataifa kiasi cha kwamba hadi imesababisha uwepo wa vilabu vinne kushiriki mashindano ya CAF yaani Klabu bingwa barani afrika na Kombe la shirikisho barani Afrika ambapo timu mbili zilishiriki/zimeshiriki kombe la shirikisho na timu mbili kushiriki ligi ya mabingwa.
Tumeshuhudia kiwango cha Simba kinachoishi leo si kile kiwango cha Simba ambacho naweza nikasema kilikuwa ni cha gharama ya kawaida tofauti na sasa ambapo timu inawachezaji wa bei ghali wakati matokeo yakipatikana si ya kuridhisha ama hayaridhishi kabisa.
Simba imekuwa ikisuasua kitendo ambacho kimefanya wapoteze michezo miwili kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika kwenye kundi 'C'.
Sasa tunaona mwenendo ulivo na kuna matumaini madogo sana Simba kuweza kusonga hatua ya robo fainali msimu huu, kwani wanahitaji ushindi wa mechi tatu huku waendelee kumuombea Horoya apate matokeo mabaya katika mechi zake. Ni ngumu kwa aina ya kikosi na mfumo unaotumika kwa sasa.
Sisemi kwamba Simba ndio haiwezi kabisa, la hasha! ni jinsi tu ambavyo naona aina ya wachezaji na mfumo unaotumika simba.
Sasa, kutokana na mwenendo huu kama Simba wasipobadilika naweza kusema msimu huu kwenye CAF ni kwakheri, labda Simba ichukuwe ubingwa wa NBC, kombe shirikisho la Azam, ama Yanga wafanye vizuri zaidi kama tunavyoona sasa Yanga inakikosi kizuri inao uwezo huo. Hii itamfanya Simba ajihakikishie kushiriki klabu bingwa msimu ujao ambapo kule kuna nafasi ukishindwa raundi ya pili basi utaenda kupambania nafasi ya kombe la shirikisho, tofauti na kuanza na kombe la shirikisho ambapo ukifungwa mechi hata raundi ya pili, ni nyumbani kumenoga.
So, bila kuweka jicho la husuda, Simba imekuwa ikiibeba Yanga kimataifa nikimaanisha Ligi ya mabingwa na sasa ni zamu ya Yanga kuibeba Simba kimataifa.