Ni muhimu kujua historia ya unayetaka kuanza naye mahusiano

Ni muhimu kujua historia ya unayetaka kuanza naye mahusiano

Dr Restart

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
4,949
Reaction score
24,046
Wasalaam wapendwa wa MMU.

Kumezuka na msemo maarufu wa vijana haswa wa kike 'unataka kuwajua maEX wangu, unataka kuwanunulia gari?'

Huu msemo una nia ya kupotosha. Zaidi, kuwatia watu katika mahusiano yatakayoandamwa na changamoto nyingi. Nakusihi, ni vema kujua historia ya mahusiano ya mpenzi wako (uliye na nia naye) kabla ya kuamua kujiingiza mazima.

Sababu zifuatazo hapa chini zinadhihirisha umathubuti wa ushauri wangu:

a) Itakusaidia kuepukana na magonjwa.
Lazima ufahamu mtu huyo aliachana na mpenzi wake wa zamani kwa sababu zipi. Watu wengine huachana kwa sababu za kiafya. Mwenzake kaukwaa, akaamua kumkimbilia. Hii itakusaidia katika kuchukua tahadhari zote muhimu kuhakikisha kama yeye pia hajaambukizwa.

b) Wengine wameachana, lakini bado mmoja ana kisasi na mwenzake.
Kuachana kwingi ni kwa shari. Mahusiano mengi huvunjika kwa malumbano. Ni wachache wanaoachana kwa amani. Sasa, itokeapo kuna mtu anapanga kisasi kwa mwenzake, hali hiyo itakuathiri nawe moja kwa moja.

c) Sababu za kitabia zisizovumilika.
Kuna wengine huachana kwa sababu ya kushindwana kitabia. Mwenzi mmoja alikuwa mlevi, malaya, mshirikina au tabia yeyote isiyopendeza. Hii itakusaidia nawe kuona kama utaweza kuendana naye kabla ya kuamua kuwa serious na mhusika.

d) Changamoto za kutoweza kupata mtoto ama uwezo wa kuzalisha.
Mahusiano mengine huvunjika kwa sababu mmoja wao ameshindwa kufanikisha upatikanaji wa mtoto. Naam, kuna wengine mtoto si kipaumbele. Lakini, wengine ni muhimu sana kuwa na mtoto.
Hivyo, ukijua wameachana kwa sababu hizo, utajipima kuona kama je, utaweza kuvumilia katika hali ya namna hiyo? Kama ndiyo, go ahead. Kama siyo, usijiingize kwenye hayo mahusiano.

e) Wengine bado wapo kwenye mahusiano. Mtu ni mke wa mtu, lakini anaamua kukuficha ili afanikishe azma yake. Utakuja kufanyiwa kitu mbaya wakati hukukusidia. Wapo wengi wameumia kwa sababu hawakujua hapo kabla.

Zipo sababu nyingi za kwa nini ni muhimu kufahamu historia ya mahusiano ya unayetaka kujiingiza kwenye mahusiano naye.

Kama ambavyo ni vema kufanya research kabla ya kuamua kujiingiza katika biashara fulani, ndivyo hivyo katika mahusiano.

Hii ni ile uwe na mahusiano imara na thabiti. Japo haitazuia changamoto, lakini angalau utajiweka katika nafasi ya unafuu wa kuzitatua.

Fanya uchunguzi Mkuu.
 
Mimi aliniuliza gf wangu mpya wakati huo nikamuuliza unataka kujua kuhusu ex wangu yupi?. Akaniuliza kwani una maX wangapi nikajibu zaidi ya 30, alitoa macho akasema hataki mwanaume malaya. Sasa history ya ex zangu unazitakia nini wakati?, nishapanda daladala,mwendokasi,bajaji,bodaboda wewe ki Vits nataka kukumiliki unaleta shobo.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Wasalaam wapendwa wa MMU.

Kumezuka na msemo maarufu wa vijana haswa wa kike 'unataka kuwajua maEX wangu, unataka kuwanunulia gari?'
Mke wangu alilelewa na single mother, na babake alikuwa kama anamkataa kimtindo. nimemuolea kwa mamake wakati huyo babake amekufa. tofauti na nilivyotarajia, aliishi akiamini ni muhimu sana kuishi na baba, na hilo analidhihirisha kwa watoto wetu, anaheshimu mume kuliko hata ndugu zake na ninajua anaogopa watoto wasijelelewa bila baba wakapitia aliyopitia (ni mwoga kuachana), na ninajua tutaishi miaka mingi sana Mungu attupatia pamoja hatufi leo wala kesho kwa Jina la Yesu ili tufurahie ndoa yetu hii tamu.

Hata tukigombana namna gani, ikija suala la positions za mume na mke, yupo very strict anachukua position ya mke kama mke na anakuachia nafasi ya mume kama mume. Asante Yesu.
 
mke wangu alilelewa na single mother, na babake alikuwa kama anamkataa kimtindo. nimemuolea kwa mamake wakati huyo babake amekufa. tofauti na nilivyotarajia, aliishi akiamini ni muhimu sana kuishi na baba, na hilo analidhihirisha kwa watoto wetu, anaheshimu mume kuliko hata ndugu zake na ninajua anaogopa watoto wasijelelewa bila baba wakapitia aliyopitia (ni mwoga kuachana), na ninajua tutaishi miaka mingi sana Mungu attupatia pamoja hatufi leo wala kesho kwa Jina la Yesu ili tufurahie ndoa yetu hii tamu.

hata tukigombana namna gani, ikija suala la positions za mume na mke, yupo very strict anachukua position ya mke kama mke na anakuachia nafasi ya mume kama mume. Asante Yesu.
Nichukue nafasi hii kukupongeza. Kuna jamaa mmoja shabiki wa majogoo wa London akisoma hapa atakasirika sana, yeye nia yake aone waliooa wote wanalialia
 
Usichunguze historia ya ma-ex tu kama una Malengo nae go deep chunguza had na familia yake, malezi yake, ukoo wake pia.
Hii itakusaidia siku moja
 
Mke wangu alilelewa na single mother, na babake alikuwa kama anamkataa kimtindo. nimemuolea kwa mamake wakati huyo babake amekufa. tofauti na nilivyotarajia, aliishi akiamini ni muhimu sana kuishi na baba, na hilo analidhihirisha kwa watoto wetu, anaheshimu mume kuliko hata ndugu zake na ninajua anaogopa watoto wasijelelewa bila baba wakapitia aliyopitia (ni mwoga kuachana), na ninajua tutaishi miaka mingi sana Mungu attupatia pamoja hatufi leo wala kesho kwa Jina la Yesu ili tufurahie ndoa yetu hii tamu.

Hata tukigombana namna gani, ikija suala la positions za mume na mke, yupo very strict anachukua position ya mke kama mke na anakuachia nafasi ya mume kama mume. Asante Yesu.
Wewe ni miongoni mwa wachache walio-bahatika.
 
Back
Top Bottom