Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Imeshakuwa ni jambo la kawaida watu waliovaa kiraia na gari la kiraia kuondoka na mtu kisha baadae mnaambiwa alikuwa polisi. Wengine wanapotea kauli inatoka waliomkamata hawakuwa polisi. Huu mkanganyiko ni kwa kuwa mara nyingine inakuwa shida kutofautisha watu hawa, na itakuwa matokeo ndio yanaamua nani ni nani?
Suala la ukamataji kwa nguvu pia linaleta maswali kama kweli mtuhumiwa wa chochote alikataa amri au la. Kama hakukataa amri kwa nini asikamatwe kwa muongozo badala ya kutumia nguvu hali inayozua sintofahamu hasa muda huu.
Ili polisi wabakishe imani yao kwa raia, utaratibu wa ukamataji watuhumiwa ufanyike kwa utaratibu na ikitokea watu waliovaa kiraia wanakamata watu, raia wajulishwe kabisa kuwa hao ni wahuni.
Ni muhimu polisi kubaki na image yake nzuri ya heshima.