SoC02 Ni muhimu sana kupenda(like), kutoa maoni(comment), kufuata(follow/subscribe) na kusambaza(share) chapisho linalokugusa kwenye mitandao ya kijamii

SoC02 Ni muhimu sana kupenda(like), kutoa maoni(comment), kufuata(follow/subscribe) na kusambaza(share) chapisho linalokugusa kwenye mitandao ya kijamii

Stories of Change - 2022 Competition

Des Noel

Member
Joined
Aug 8, 2022
Posts
5
Reaction score
12
Afya ya akili na mitandao ya kijamii haiwezi kutengenishwa kwa karne ya 21, na ni jambo muhimu ambalo linapaswa kupewa uzito unaostahiki na watu na wataalamu wa afya ya akili.

Katika nchi zilizoendelea inaonesha vijana wengi wanaathitrika sana na idadi ya watu wanaowafuatilia katika mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii huwapa presha kubwa sana vijana na inaonekana kama inanakisi kukubalika kwao miongoni mwa vijana wenzao na hili pia lipo kwenye jamii yetu yetu ya Tanzania.

Ni ukweli kuwa watu wenye kupandisha vitu visivyokuwa na maadili katika jamii yetu wanapata ufuasi mkubwa sana kuliko wale wanaopandisha mambo ya msingi katika jamii.

Binadamu ni kiumbe cha kijamii huwezi kusema hato athrika na mazingira yake.

Binadamu ni kiumbe anaependa sifa na kutiwa moyo ili aendelee kufanya mambo mazuri kwa wale wanaompa pongezi.

Tunapaswa kupenda, kuwafuata na kusambaza machapisho yenye maana kwenye mitandao ya kijamii na hii ni tendo la kuiokoa taifa letu .

Tunalalamika chapisho za maana hazipati uhusuisho wa kutosha ila lakini ni sisi pia tunayapita haya machapisho kama hatujayaona.

tunawapa nguvu wale wanaochapisha machapisho yanayosaidia jamii wakiona michango mizuri na anapata ufuasi na kufuatiliwa na watu.

Hatakaa kuona kuwa nguvu zake, muda wake anaetumia ili awaletee jambo jema katika jamii linathaminiwa na wahusika.

Kila unayeona anafanya jambo jema katika mitandao ya jamii.
Umfuate
Utoe mchango wako,
Usambaze kwa watu wengine,
Na vile vile tunapaswa tusiwafuate na kutoa mchango kwa wale wanaosambaza vitu vinavyoharibu jamii yetu.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom