funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Kamwe haiwezekani tuishi au kufanya mambo yetu kienyeji au kama wanyama wa porini.
Kama tuliamua kufuata taratibu nzuri za kimagharibi tuzifuate kikamilifu na zile mbaya tuziache kikamilifu.
Zipo stand au bus stations nyingi zimejengwa nchini na zinaendelea kujengwa kwa kasi zikiwa na lengo la kuimarisha staha ya usafiri nchini lakini hazitumiki kisa maslahi ya watu wachache pengine wenye fedha au wanaonufaika wao pekee badala ya umma.
Ni vyema kila mamlaka ya Serikali kuamka na kusimamia sheria,kanuni na taratibu.
Hatuwezi kuwa na standi kila mahala au soko kila kona ...huu ni uhuni.Japo tunaweza kuwa na mipango miji yenye kuanisha mpangilio wa kila huduma .
Sipuuzi malalamiko ya mtu anayeishi kigamboni kuitafuta stand Magaufuli mbezi japo siwezi kuamini kama mbadala wake ni kuegesha basi kila alipo tajiri wa mabasi.
Yapo maeneo yanaweza kuboreshwa kwa haraka na kuhakikisha kuwa huduma ya usafiri wa aina zote unawafikia wasafiri.
Mfano :ilipokuwepo stand ya kisutu tunaweza kuwa na SUBWAY inayokuja kutokea Magufuli Terminal.
Vivyo hivyo kutokea mbagala n.k
hii ndio itakuwa suluhisho la baadhi ya visababu vya kutaka kuzuia mabadiliko.
MAGUFULI TERMINAL IHESHIMIWE ILINDWE ITUNZWE ,IENDELEZWE ,IBORESHWE ITANGAZWE NA HATIMAYE IWE NI EAST,SUOTH AND CENTRAL BUS TERMINAL HUB.
Wafanyabiashara wote wa mabasi walete ushauri mezani wa kuboresha na kuneemeka kupitia MAGUFULI TERMINAL na sio Kuihujumu
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!