Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,053
- 2,207
Kufuatia sintofahamu iliyotokea huko UK ambapo Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonekana kwenye basi lililoandaliwa kuingiza viongozi wa mataifa mbalimbali kwenye eneo la kuaga mwili wa malikia Elizabeth Il.
Inawezekana tukapiga kelele sana ingawa tukashindwa kuwa na sababu thabiti za kwa nini Rais wetu asipande basi?
Binafsi ninapenda kufuatilia protokali za namna viongozi wetu wanapokelewa huko ughaibuni na kulinganisha na sisi tunavyowapokea na kuwatreate viongozi au hata watu maarufu wao.
Hakuna shaka kuwa bado kuna ombwe na utofauti mkubwa.
Nitatoa mfano wa hili kwa kuangazia na kukumbushia tukio la takribani mwezi mmoja uliopita.
Katika mashindano ya michezo ya jumuiya ya madola nilisikitishwa kuona balozi wetu nchini UK akiwa katikati ya msongamano wa wananchi wa kawaida pale aliposhihudia wanariadha watanzania wakituwakilisha vyema katika mashindano hayo.
Balozi Migiro alikuwa amebanwa sana, hakuwa jukwaa kuu kama nilivyotaraji na ilionekana waandaaji hawakuwa na protokali ya kumualika au kuheshimu uwepo wake kwenye michezo hiyo adhimu, iliniudhi.
kwa Tanzania balozi wa uingereza akiwa kwenye shughuli ya namna hiyo ni lazima tumgempa heshima stahiki pamoja na ulinzi wa kipekee.
Inawezekana haya yanatokea pengine kwa kuwa hatuna miongozo rasmi ya namna msafara wa Rais wetu tunataka iwe popote pale anapoenda na isipokuwa hivyo basi sheria kanuni na taratibu zinakuwa zimekiukwa.
Hivyo ni muhimu sasa kwa guru's wote wa diplomasia na protokali kuja na maboresho muhimu na ya kisheria(legal binding) yanayohusu misafara, haiba na nembo mbalimbali za utawala.
Aidha hata picha rasmi zinazotolewa lazima zizingatie sheria yaani tutunge sheria rasmi ya privacy ya Rais na viongozi wetu wakuu.atakayerusha picha yoyote ya Rais iwe popote pale lazima awe na kibali maalumu.
Ni hayo tu.