Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kuna mlolongo wa matukio yanayotokea nchini hivi sasa, yanayonifanya niweze kutabiri yatakayotokea nchini baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini kwetu mwishoni mwa mwaka huu
Tulimsikia wenyewe Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Magufuli akitamka hadharani bila kificho chochote kuwa kura za maoni za vikao vya CCM vya majimbo mwaka huu si lolote wala chochote mwaka huu, kwani mwenye uwezo wa kuamua ni nani atakuwa mgombea wa ubunge mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, atakuwa yeye mwenyewe Mwenyekiti wa CCM Taifa!
Akaendelea kusisitiza kuwa yeye mwenyewe anaweza kumpitisha yule mgombea aliyekuwa wa kumi, katika mchakato wa kura za maoni majimboni kwenu, akiwaacha wale wote walioongoza kwa maana ya wa kwanza hadi wa tisa.na wala hatalazimika kutoa sababu zozote!
Hivi ndivyo ilivyo CCM ya Magufuli, katika kipindi hiki, ambapo yeye hazingatii tena Katiba ya Chama chake inasema nini, bali matakwa yake binafsi, ndiyo yanayozingatiwa
Tumeshuhudia Rais Magufuli akifanya uteuzi mpya wa zaidi ya watumishi 33, katika maandalizi ya uchaguzi mkuu mwishoni mwaka huu, wakiwemo watu "wake" wa karibu wakuu wa mikoa ya Dar na Manyara, Paul Makonda na Alexander Mnyeti "akiwapumzisha" akiwaandaa kuwa waheshimiwa wabunge, baadaye mwaka huu!
Hao ni miongoni ya wale ambao piga ua ni lazima atawateua yeye kuwa wagombea ubunge, kwenye majimbo yao, bila kujali matokeo ya kura za maoni za majimbo husika!
Vile vile jambo lingine litakaloleta chuki kubwa na mtifuano ndani ya CCM, ni kwa wale wanachama wapya wa "kuja" kupewa kipaumbele katika nafasi za kugombea, wakati wale wanachama "asilia" wakiendelea kusugua benchi
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi CCM itaendelea kubaki moja baada ya uchaguzi mwishoni wa mwaka huu, licha ya Mwenyekiti kuwa tayari na watu wake katika nafasi za ubunge kwenye majimbo hayo?
Nimekuwa nikijiuliza pia, ni kwanini Mwenyekiti atumie nguvu kubwa kutaka kuwasimika ubunge wa majimbo, wakati yeye anayo nafasi ya Kikatiba ya kuteua wabunge wake yeye mwenyewe, wasiozidi kumi?
Hivi hii hali haitaleta chuki kubwa miongoni ya wagombea wa CCM, watakaokuwa wamekatwa majina yao, licha ya kuwa wameongoza kwenye kura za maoni kwenye majimbo yao?
Tusubiri kuona mtifuano mkali baina ya wale "wateuliwa maalum" wa nafazi za ubunge wa Mwenyekiti na wale ambao watakuwa ndiyo chaguo la wapiga kura majimboni mwao