TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
[h=5]Ifuatayo ni Nukuu kutoka kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Urithi wa kizazi na kizazi Cha Watanzania, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, akihusia jambo juu ya aina ya Muungano, kuulinda na kuuendeleza.
Muunge mkono Mwalimu Nyerere kataa Serikali tatu, Dumisha Muungano wa Serikali Mbili.[/h]
"Ni ulevi tu hasa ulevi wa madaraka, mna nchi moja mnaleta leta mambo ili kuvunja muungano mpate sehemu nyingi zaidi za kuongoza ni ulevi tu. Wakati tunaunganisha nchi hizi Karume alinambia (Serikali moja na wewe Nyerere Rais) nikamwambie Sheikh Zanzibar muwadogo nyie mtapoteza utambulisho wenu. Tukakubaliana tuwe na Muungano wa aina yake duniani ambao Zanzibar watakuwa na Serikali yao kwa mambo ya Zanzibar.[/h][h=5]
Ukiwasikiliza Zanzibar utakubali kuwa tungalikuwa na Serikali moja wakati ule wangetokea watu wakutaka kujitenga haraka na ndio maana hoja zao zote leo zinathibitisha niliyomwambia Karume wakati ule juu ya utambulisho wa Zanzibar sasa wanao, wanatafuta nini watu hawa..?
Kwakuwa bara ni kubwa zaidi kwa watu na jiografia, Serikali yake itakuwa ni Serikali ya Muungano ambayo itahusika na mambo yote ya bara na yale ya muungano, Utaratibu huu umetusaidia hapa tulipofika Taifa la Amani na Udugu wa mfano Duniani. Viongozi muwe wakali kulinda Muungano huu kwa kuwa wapingaji watakuwapo tu! Akitokea kiongoz anadhamira yakutugawa afungiwe pahala atulie tu aone kama kutengwa kunamsaidiaje basi.
Wakati ule wakaanza kujitokeza watu ambao wanaona hawakubaliki Zanzibar na wanataka Urais wakaona hapa Tanganyika ikiwa na Serikali yake tunaweza kuongoza (watu wa ovyo hawa maana hata hilo jina Tanganyika mimi sijui limetokea wapi..? Nimetafuta sana sijajua na silipendi kwakuwa tulibatizwa na wanyonyaji.
Na kule Zanzibar wakawepo watu wanataka kuongoza hawakubaliki bara wakafikiri kukiwa na Serikali ya nchi bila bara watakuwa marais na jeshi na bendera na nini na nini.
Uhuu ni uroho tuu hasa uroho wa madaraka.
[/h][h=5]CCM na Watanzania watakuwa wanafanya makosa sana wakikataa aina hii ya Muungano wa Serikali mbili kwa sababu wanazotengeneza kila kukicha. Tukayaweka hayo kwenye katiba ya 1977. Wapuuzi hawakosekani tu watakuwapo hata mkiwa na Serikali 4 watataka 5 mtakuta mwisho mnaserikali ya Kaskazini maana wapo watu wanatamani hilo "
Muunge mkono Mwalimu Nyerere kataa Serikali tatu, Dumisha Muungano wa Serikali Mbili.[/h]