Ni Muungano wa Serikali mbili, it's Mwalimu Legacy...!

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
[h=5]Ifuatayo ni Nukuu kutoka kwa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Urithi wa kizazi na kizazi Cha Watanzania, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, akihusia jambo juu ya aina ya Muungano, kuulinda na kuuendeleza.

"Ni ulevi tu hasa ulevi wa madaraka, mna nchi moja mnaleta leta mambo ili kuvunja muungano mpate sehemu nyingi zaidi za kuongoza ni ulevi tu. Wakati tunaunganisha nchi hizi Karume alinambia (Serikali moja na wewe Nyerere Rais) nikamwambie Sheikh Zanzibar muwadogo nyie mtapoteza utambulisho wenu. Tukakubaliana tuwe na Muungano wa aina yake duniani ambao Zanzibar watakuwa na Serikali yao kwa mambo ya Zanzibar.[/h][h=5]
Ukiwasikiliza Zanzibar utakubali kuwa tungalikuwa na Serikali moja wakati ule wangetokea watu wakutaka kujitenga haraka na ndio maana hoja zao zote leo zinathibitisha niliyomwambia Karume wakati ule juu ya utambulisho wa Zanzibar sasa wanao, wanatafuta nini watu hawa..?

Kwakuwa bara ni kubwa zaidi kwa watu na jiografia, Serikali yake itakuwa ni Serikali ya Muungano ambayo itahusika na mambo yote ya bara na yale ya muungano, Utaratibu huu umetusaidia hapa tulipofika Taifa la Amani na Udugu wa mfano Duniani. Viongozi muwe wakali kulinda Muungano huu kwa kuwa wapingaji watakuwapo tu! Akitokea kiongoz anadhamira yakutugawa afungiwe pahala atulie tu aone kama kutengwa kunamsaidiaje basi.

Wakati ule wakaanza kujitokeza watu ambao wanaona hawakubaliki Zanzibar na wanataka Urais wakaona hapa Tanganyika ikiwa na Serikali yake tunaweza kuongoza (watu wa ovyo hawa maana hata hilo jina Tanganyika mimi sijui limetokea wapi..? Nimetafuta sana sijajua na silipendi kwakuwa tulibatizwa na wanyonyaji.

Na kule Zanzibar wakawepo watu wanataka kuongoza hawakubaliki bara wakafikiri kukiwa na Serikali ya nchi bila bara watakuwa marais na jeshi na bendera na nini na nini.

Uhuu ni uroho tuu hasa uroho wa madaraka.

[/h][h=5]CCM na Watanzania watakuwa wanafanya makosa sana wakikataa aina hii ya Muungano wa Serikali mbili kwa sababu wanazotengeneza kila kukicha. Tukayaweka hayo kwenye katiba ya 1977. Wapuuzi hawakosekani tu watakuwapo hata mkiwa na Serikali 4 watataka 5 mtakuta mwisho mnaserikali ya Kaskazini maana wapo watu wanatamani hilo "

Muunge mkono Mwalimu Nyerere kataa Serikali tatu, Dumisha Muungano wa Serikali Mbili.
[/h]
 
...

Hii kitu ni muhimu sana kupata maoni ya Mzee wetu Mohamed Saidi na wahafidhina wengine wa Kariakoo na Zanzibar. Ritz, tafadhali fikisha ujumbe kwa members.

CCM bana, kumtukana Mwalimu matusi ya rejareja indirectly kupitia wahafidhina hamjambo bali linapokuja suala lenye maslahi kwenu ndipo mnapomwona wa maana. Kweli akili ndogo.

CC: Yericko Nyerere.
 
Leo hii ndo mnamkumbuka Mwl Nyerere, kwa sababu mmeshikwa pabaya na wimbi la mabadiliko.
Nyie ni watu wanafiki sana, tena wala hampaswi kuungwa mkono hata kidogo.....WEHU KABISA NYIE!
 
Hilo ndilo umeliona ni hoja ya kuchangia hapa. Hivi nyie chadema bila kutukana mnajihisi hamtaweza kulipwa posho zenu.
 
CCM Bila Muungano wa serikali mbili haiwezi kuishi kamwe, itakufa , ndio maana inajitahidi sana kupinga maoni ya wananchi walioona ni busara kuwa na serikali tatu, sasa nyie CCM mnapingana na wananchi mnaotaka kuwaongoza?

Hoja za muungano wa Serikali mbili mo dhaifu sana , hazina mashiko .........Tanganyika iwepo kwanza.
 
Is it a search for tanganyika..? Or the quest for tanzania bara. hoja zako ni juu ya serikali tatu ama uanzishwaji wa serikali ya tanganyika,ambayo ni hoja tata kuliko hata hoja ya katiba mpya.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa na dhamira ya dhati ya kupeleka nchi yetu katika mema, lakini alikuwa na mapungufu yake makuu matatu katika muktadha wa uongozi wake kwa taifa letu, moja ya madhaifu ya mwalimu ni kuhimiza suala la serikali mbili ndani ya muungano wa mataifa huru mawili; This vision was flawed and will remain so....
 
Hii kitu ni muhimu sana kupata maoni ya Mzee wetu Mohamed Saidi na wahafidhina wengine wa Kariakoo na Zanzibar. Ritz, tafadhali fikisha ujumbe kwa members.

CCM bana, kumtukana Mwalimu matusi ya rejareja indirectly kupitia wahafidhina hamjambo bali linapokuja suala lenye maslahi kwenu ndipo mnapomwona wa maana. Kweli akili ndogo.

CC: Yericko Nyerere.
Huyu unaye CC: hana lolote na ametapeli watu kwa kuwadanganya kama yeye ni mtoto wa Mwl. Nyerere wakati hata uhusiano wa mbali na familia ya Mwl. Nyerere hana.

Huyu niwa kupuuzwa kama walivyo crafty wengine.
Nipo Butiama sasa hivi. Naulizia kuhusu huyu Yericko,lakini bado sijampata mtu anayemfahamu. Bado naendelea kuulizia. Nimemtuma mtu afanye uchunguzi.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-tanganyika-na-zanzibar-220.html#post6607884
 
Mkuu TandaleOne , Amani iwe nawe

Vp Lakini Kuhusu issue ya Familia yako.

Ok, Hivi Nyie CCM, Mbona Mnapenda Sana kuchagua Baadhi ya Speech za Mwalimu Nyerere Kwa Maslahi yenu na Kuziacha Nyingine.
Kuna ile quote ya Mwalimu Nyuma ya Mabango yenu

Bila CCM Imara Tanzania itayumba

Hivi hamuonagi aibu na Kusutwa na Nafsi Mkiona ule Ujembe ???

Ok, Hebu now tujikumbushe Baadhi ya Quotes za Huyo huyo Mwalimu Nyerere ambazo kila Uchwao Mko Mstari wa Mbele Kuzivunja

"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?
Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995

Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?

Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.

Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.

Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....

Acheni woga! Mwalimu this! Mwalimu that! HOGWaSH!

Kwani Malimu ni Mungu?

Acheni mabadiliko yaje. Tunaitaka Tanganyika yetu. Na msije na hoja mfu kwamba Serikali tatu ni gharama. SMZ wamejitawala tangu Muungano. Tanganyika iliuwawa kuipisha Serikali ya Muungano. Sasa Serikali ya Tanganyika na irudi. Muungano ubakie, sawa, lakini Tanganyika irudi!

Ndio maana mkasheherekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika Bara. Kwani Tanganyika Bara ni NCHI?
 
Wakati Mnaendelea Ku M quote Julius Nyerere, acha na sie tuwa Quote kama Ifuatavyo, ila Siko Sure kama haya Kweli yalisemwa ama kuna watu wanawalisha Maneno

"Kina mama pia endeleeni kuzaa wasichana wazuri kwani katika miaka hii miwili hata kwenye mashindano ya urembo duniani tumetamba."
***********************

Ikiwa tutaruhusu wasichana waliojifungua kurudi mashuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa darasani"
***********************

"Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi" Hapa mbunge Chitalilo aliyegundulika kuwa kughushi vyeti vya elimu yake akitetewa
***********************

"Nafikiri imefika wakati Tuwaombe Rafiki zetu wa Scandinavia,Watufundishe kuandika na Kusoma Mikataba haswa ya MADINI,kwani sie hatuna wataalamu hao" -May'2007

Huyu unaye CC: hana lolote na ametapeli watu kwa kuwadanganya kama yeye ni mtoto wa Mwl. Nyerere wakati hata uhusiano wa mbali na familia ya Mwl. Nyerere hana.

Huyu niwa kupuuzwa kama walivyo crafty wengine.

Mkuu Mbona hata Mwenezi wenu Inasadikika kuwa Hana hata Chembe ya Uhusiano na Marehemu Brigedia !!!
 
Tandaleone,

Wengi wetu ni waumini wakubwa sana wa Baba wa Taifa Mwalimu nyerere, lakini kama binadamu wengine, alikuwa na mapungufu yake; Sasa iwapo tunazingatia kanuni ya chama alichokiasisi (CCM) kwamba "kukosoa na kukosolewa ndio silaha ya mapinduzi", basi kwetu sisi wachache, njia moja nzuri ya kumuenzi Mwalimu ni kwa kufuata kanuni muhimu kama hizi na nina maeneo mengi ya kumkosoa mwalimu juu ya muungano,lakini kwa sasa nianze kama ifuatavyo:

Nikirudi kwenye mada husika, katika mazungumzo yake na gazeti la The Observer la Uingereza Aprili 20, 1968, mwalimu alitamka yafuatayo:

"Iwapo umma wa zanzibar bila ya kushawishiwa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha;Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea kuwepo iwapo washiriki wake wataamua kuukana."

Kwanza, ni muhimu ukafahamu kwamba muungano wetu haukuletwa na ASP wala TANU bali uamuzi wa marais wawili (nyerere wa tanganyika) na (karume wa zanzibar), sio vyama vyao (ASP na TANU), ambapo hata ingekuwa hivyo, vyama hivi vilikuwa bado havina mandate kwa wananchi wote wa pande husika; kwanza, TANU ilikuwa bado changa sana na haijasambaa ipasavyo, na kwa upande wa ASP, hiki hakikuwa chama pekee cha siasa Zanzibar as of 1964; Pamoja na haya yote, katika kutumia mamlaka waliyonayo kwa niaba ya "wananchi wao", Nyerere na Karume ndio walioamua kuunganisha nchi hizi mbili; Sasa Mwalimu anaposema miaka minne baadae (1968)kwamba muungano hautakuwa na maana iwapo washiriki wake wataamua kuukana, ni washiriki wepi hao, wananch? Ni wanachama wa TANU na ASP? Viongozi waasisi? na kwanini Zanzibar pekee ndio walikuwa na potential ya kuukana na sio Tanganyika? Hivi kweli hatuoni such flaws katika muungano wetu ambazo kama kweli tuna nia ya dhati ya kuuimarisha kwa vile tayari upo na una mizizi, tuurekebishe kwa manufaa yetu sote?

Pia ni muhimu ukumbuke kwamba muungano uliodhamiriwa ni ule per articles of the Union, 1964, na sio kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ambayo ndio ilipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la articles of the union (1964);

Tandaleone, iwapo unapata jukwaa kujenga hoja yako ya kumuenzi mwalimu katika muktadha wa muungano, hoja yako ni tuulinde muungano upi haswa, je muungano, kwa mujibu wa mkataba wa muungano 1964 au Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)?

Bila ya wewe kutoa ufafanuzi kwa swali hili la msingi, kamwe hautakuwa na hoja yenye mashiko zaidi ya kututafutia tu ubaya na baba wetu wa taifa mbele ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kufikiri na kuchambua suala hili sawa sawa;tukubali tu kwamba mwalimu alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, na moja ikiwa ni suala zima la mfumo wa muungano - nasisitiza, tatizo la mwalimu sio nia ya muungano, bali tatizo ni ni mfumo, na ni suala hili la mfumo wa muungano ndio limekuwa ni chanzo kikubwa cha mgogoro uliodumu kwa miaka zaidi ya 30 sasa;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hata kujilimbikizia mali haikuwa sera ya Nyerere...what legacy are you advocating now?
 
Akili za Nape ni za kupuuzwa, ni kujipotezea muda wako bure kudebate na mtuanayechaguwa legacy anazozitaka yeye, hapa anamaanisha Nyerere aliacha Legacy ya Rushwa na ufisadi.

By the way siyo Mungu si lazima kila alichoamini yeye basi wote tuamini, hapa ni Serikali moja au Serikali tatu, habari ndio hiyo.
 
Tandaleone,

Wengi wetu ni waumini wakubwa sana wa Baba wa Taifa Mwalimu nyerere, lakini kama binadamu wengine, alikuwa na mapungufu yake; Sasa iwapo tunazingatia kanuni ya chama alichokiasisi (CCM) kwamba "kukosoa na kukosolewa ndio silaha ya mapinduzi", basi kwetu sisi wachache, njia moja nzuri ya kumuenzi Mwalimu ni kwa kufuata kanuni muhimu kama hizi na nina maeneo mengi ya kumkosoa mwalimu juu ya muungano,lakini kwa sasa nianze kama ifuatavyo:

Nikirudi kwenye mada husika, katika mazungumzo yake na gazeti la The Observer la Uingereza Aprili 20, 1968, mwalimu alitamka yafuatayo:

"Iwapo umma wa zanzibar bila ya kushawishiwa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha;Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea kuwepo iwapo washiriki wake wataamua kuukana."

Kwanza, ni muhimu ukafahamu kwamba muungano wetu haukuletwa na ASP wala TANU bali uamuzi wa marais wawili (nyerere wa tanganyika) na (karume wa zanzibar), sio vyama vyao (ASP na TANU), ambapo hata ingekuwa hivyo, vyama hivi vilikuwa bado havina mandate kwa wananchi wote wa pande husika; kwanza, TANU ilikuwa bado changa sana na haijasambaa ipasavyo, na kwa upande wa ASP, hiki hakikuwa chama pekee cha siasa Zanzibar as of 1964; Pamoja na haya yote, katika kutumia mamlaka waliyonayo kwa niaba ya "wananchi wao", Nyerere na Karume ndio walioamua kuunganisha nchi hizi mbili; Sasa Mwalimu anaposema miaka minne baadae (1968)kwamba muungano hautakuwa na maana iwapo washiriki wake wataamua kuukana, ni washiriki wepi hao, wananch? Ni wanachama wa TANU na ASP? Viongozi waasisi? na kwanini Zanzibar pekee ndio walikuwa na potential ya kuukana na sio Tanganyika? Hivi kweli hatuoni such flaws katika muungano wetu ambazo kama kweli tuna nia ya dhati ya kuuimarisha kwa vile tayari upo na una mizizi, tuurekebishe kwa manufaa yetu sote?

Pia ni muhimu ukumbuke kwamba muungano uliodhamiriwa ni ule per articles of the Union, 1964, na sio kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ambayo ndio ilipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la articles of the union (1964);

Tandaleone, iwapo unapata jukwaa kujenga hoja yako ya kumuenzi mwalimu katika muktadha wa muungano, hoja yako ni tuulinde muungano upi haswa, je muungano, kwa mujibu wa mkataba wa muungano 1964 au Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)?

Bila ya wewe kutoa ufafanuzi kwa swali hili la msingi, kamwe hautakuwa na hoja yenye mashiko zaidi ya kututafutia tu ubaya na baba wetu wa taifa mbele ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kufikiri na kuchambua suala hili sawa sawa;tukubali tu kwamba mwalimu alikuwa na mapungufu yake kama binadamu, na moja ikiwa ni suala zima la mfumo wa muungano - nasisitiza, tatizo la mwalimu sio nia ya muungano, bali tatizo ni ni mfumo, na ni suala hili la mfumo wa muungano ndio limekuwa ni chanzo kikubwa cha mgogoro uliodumu kwa miaka zaidi ya 30 sasa;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

please improve your ending: what direction would you like us to go--at the end, please!?
 
Sina uhakika kama nimeelewa swali lako lakini nitajaribu kujibu kwa kusema kwamba - Tunahitaji Katiba ya Tanganyika na Serikali yake huru na yenye mamlaka kamili kama ilivyokuwa siku mkataba wa muungano ulipokuwa unatiwa sahihi (1964); Hii itatoa fursa kwetu kurekebisha makosa tuliyofanya, hasa ya kuteka nyara suala la muungano nje ya makubaliano ya muungano, 1964 ambapo ingawa nia inawezekana ilikuwa njema, nia hii imezaa tatizo nililo jadili hapa and elsewhere ambalo ni la mfumo wa muungano, sio nia ya muungano; Tukipata katiba yetu Tanganyika, sasa ndio watanganyika watakuwa sio tu na fursa bali pia "mamlaka" kamili ya kuingia katika mchakato wa kura ya maoni kuchagua aina ya muungano wanaoutaka, au iwapo kuna haja ya uwepo wa muungano all together; Wananchi wakitaka muungano, suala ambalo naamini litatokea, basi katiba ya Tanganyika ndio iwe ticket yetu katika hilo ambapo itasema ni masuala yepi yawe surrendered for muungano na yepi yabakie kama ya Tanganyika kama ilivyo kwa zanzibar kwa mujibu wa katiba yao ya sasa;

Huu ni mtizamo sahihi, ingawa mtizamo huu una overlook significance ya elimu kama kigezo cha maamuzi yatayowezesha muungano kuwapo baada ya katiba ya Tanganyika kuhuishwa, na Tanganyika yenyewe kuhuishwa. Tunaotetea serikali moja miongoni mwetu tumechagua NIA ya muungano kuwa ndo kiwe kitu cha kutetea. Wewe umechagua MFUMO wa muungao kiwe ndo kitu cha kutetea.

Tatizo ninaloliona ni kwamba wale wanaochangua mfumo wa muungano kuwa iwe ndo njia ya kuenda kutoka hapa tulipo watatoa mwanya kwa muungano kufa kwa sababu wateja wa huu muungano si wote wana elimu ya kutosha kujua umuhimu wa muungano. Na kwa maana hiyo, mi nadhani njia sahihi ni kujenga hoja zinazoelekeza kuchangua serikali moja ili kuwabeba wasioelewa umuhimu wa muungano kwa sasa.
 
Nadhani haujanisoma vyema - kama umekuwa unanifuatilia, nimekuwa nikipigania nia ya muungano kwa mujibu wa mkataba wa muungano wa 1964; Kwani wewe unapigania nia hiyo kwa mujibu wa nini, Katiba ya JMT (1977)? kama nipo sahihi, basi hapo ndipo tunapopishana kwani Katiba ya JMT imeinyakua nia ya mkataba wa muungano (1964) kupitia mfumo ambao kamwe hauwezi kufanya kazi; kwa maana hii, kwetu sisi, hatutetei mfumo bali tunaujadili mfumo kwamba haufai hivyo urekebishwe vinginevyo suala la muungano wont work by ignoring suala la mfumo;
 
Back
Top Bottom