Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani haujanisoma vyema - kama umekuwa unanifuatilia, nimekuwa nikipigania nia ya muungano kwa mujibu wa mkataba wa muungano wa 1964; Kwani wewe unapigania nia hiyo kwa mujibu wa nini, Katiba ya JMT (1977)? kama nipo sahihi, basi hapo ndipo tunapopishana kwani Katiba ya JMT imeinyakua nia ya mkataba wa muungano (1964) kupitia mfumo ambao kamwe hauwezi kufanya kazi; kwa maana hii, kwetu sisi, hatutetei mfumo bali tunaujadili mfumo kwamba haufai hivyo urekebishwe vinginevyo suala la muungano wont work by ignoring suala la mfumo;
Nimekuelewa vizuri sana Mchambuzi. Kuna kitu wewe pia unaki-skip. Elimu ya watu wetu kujua umuhimu wa Muungano. Nadhani waliotengeza huu muungano walitumia kigezo hiki pia kufanya maamuzi waliyoyafanya--rightly or wrongly so. Katika Project Management kuna kitu kinaitwa Killer Assumption. Yaani unapanga mpango, halafu kunakuwa na kitu fulani cha kuwa considered; kwamba kama kipo mradi unakufa.
Wewe Mchambuzi una project ya Muungano kuwepo baada ya Katiba ya Tanganyika kuhuishwa. The killer assumption ni kwamba watu watakaoamua huo muungano kuwepo hawana elimu ya kutosha kujua kuwa Internationalism ni factor muhimu katika kuendeleza maeneo; au niseme nchi zinazoweza kujiendesha kwa umoja. Kwa maana hiyo ukosefu wa elimu ya kutosha miongoni mwa watakaoamua kuwepo ama kutokuwepo kwa muungano ni killer factor ya muungano. Serikali ya Tanganyika ikizuka leo Muungano hakuna!
That leaves us with only one option tunaojua faida za internationalism: na hiyo option ni kuleta serikali moja by hooks and crooks! hii ndo inatakiwa kuwa option ya ccm
Sasa nimekuelewa na kuhusiana kuhusiana na option ya serikali moja, lakini unaposema "we are remained with one option", "we" ni nani, CCM?
Pia how do you justify kuimarisha muungano wa serikali moja wa dola mbili huru ambazo zote zina masuala ambayo wangependa wayafanye ya muungano na mengine yabakie yao kwao binafsi?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Ni federalism ninayoingelea hapo Mkuu. Kunakuwapo na dola moja tu, lakini peculiarities zinaweza kuruhusu mambo fulani yakatendeka tofauti tofauti hapa na pale--lakini ndani ya dola moja; hakuna vidola kila kona.
Now, pengine ninakuwa biased na mfumo wa marekani kwa kuwa nimekaa kule. Sikuona shida kuona Michigan wana mfumo tofauti wa Elimu na Florida. Texas wana mfumo wa ulinzi unaotumia Sheriffs tofauti na say Hawaii. Yaani kunakuwa na mambo fulani-fulani yanatofautiana lakini ni ndani ya dola moja. Kila Jimbo linakuwa na viuhuru fulanifulani tofauti na jingine. And it works fine! Ukiangalia vizuri utadhani Nyerere alikuwa anaelekeza tuende huko.
Kwa hiyo ninachoongelea hapa kwa upande fulani ni uhuru limited ndani ya majimbo yaliyopo katika dola moja. Zanzibar inakuwa Jimbo tu katika federal state inayoitwa Tanzania. Uelewa uliopo sasa (na hapo sasa linakuja lile tatizo la elimu), wapo watakoliita hili Zanzibar inamezwa. Eee wacha imezwe. Mbona Shinyanga, Mwanza na Tabora vilishamezwa siku nyingi? Mbona Mbeya na Iringa vilimezwa! Kwa nini Zanzibar isimezwe! sisi si walewale tu!? Where is the problem.
Ningependa nikuulize maswali makuu matatu kuhusiana na hoja zako hapo juu:
(1) Hivi unajua zanzibar walipata uhuru wao mitaani kwa kumwaga damu, na sio lancaster hall kama sisi kwa suti, tai na kahawa? Unaimezaje dola ya namna hii kwa kuifanya kama vile ni historia yake ni kama ya Mbeya au Tabora?
(2) Hivi unajua kwamba Zanzibar huko nyuma iilikuwa ni himaya yenye uchumi mkubwa kuliko Tanganyika na na ilikuwa ina control uchumi mpaka Dar-es-salaam na maeneo mengine?Unageuzaje eneo hili kuwa ni kasehemu tu kama Mtwara, na mbaya zaidi, kupora maamuzi yake kisiasa, kiuchumi na kijamii kutoka mji mkongwe na kuhamishia, sio DSM ambapo kidogo kuna uhusiano na zanzibar ya kale, bali Dodoma?
(3) Mwisho, haupo firm kujadili aina ya muungano - una move back and forth on provincial, unitary and federation systems - je kwa mtazamo wako, muungano wetu ulidhamiriwa kuwa wa namna gani as of April 1964?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
heshima kwako mkuu.Mwalimu Nyerere alikuwa na dhamira ya dhati ya kupeleka nchi yetu katika mema, lakini alikuwa na mapungufu yake makuu matatu katika muktadha wa uongozi wake kwa taifa letu, moja ya madhaifu ya mwalimu ni kuhimiza suala la serikali mbili ndani ya muungano wa mataifa huru mawili; This vision was flawed and will remain so....
Hilo ndilo umeliona ni hoja ya kuchangia hapa. Hivi nyie chadema bila kutukana mnajihisi hamtaweza kulipwa posho zenu.