Ni mwaka sasa tangu ujenzi uanze, sijaona kilichofanyika Bwawa la Rufiji

Mbona hata hiyo SGR yenyewe hamuachi kubeza!
 
Naona ni video ya robo mwaka uliopita, wajitahidi kutoa updates walau kila wiki
Itapendeza ikiwa utachukua hilo jukumu kama priority kwako, wao nahisi watakuwa na vipaombele vyao zaidi ya hicho unachodai wewe. Tatizo unataka wawaze sawa na kichwa chako
 
Hamuoneshwi wewe na nani? kama ni wewe na mkeo funga safari nenda kajionee kwa macho unless otherwise uwe umeajiri mjakazi wa kupiga picha na kukutumia uone.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa unaota, yaani mwaka tu uone sentimita 50!!! Mobilization - maandilizi tu yenyewe yanachukua miezi 6, itakuwa kuinua tuta? Tambua pia kuna kuhamisha mto ili bwawa lijengwe mahali mto ulipo kwa sasa
Mtihani huu tusubiri mvua aje ndio tukutane kijiwe cha kahawa.
 
Mimi ni kati ya wanaofuatilia haya mambo kwa karibu kupitia vyombo vya habari kwa sababu napenda sana Infrastructures, Kuna wana wanafanyia kazi maeneo yote ya miradi mikubwa hivyo napata updates.
Tusubiri tusiwe na haraka, Projects Construction ni Engineering work, time is everything in Engineering.
Subira ndio msingi wa mafanikio. Tusimalize maneno na kuanza kuponda kwani kutawala sio kama kuwa Monitor class C.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Project kubwa kama hizi nasikia ni siri hata kuna mdau alisha andika huku huruhusiwi hata kufika huko na hata gps code hupati
 
Duh huyu ndo mTanzania halisi. Nadhani elimu zaidi inatakiwa juu ya miradi kama hii inavyojengwa. Nakumbuka daraja la Kigamboni nalo wadau walivyoona kuna kidaraja cha tempo kimejengwa kama pale salender sasa hivi lile daraja la muda lilivyojengwa basi bila kuuliza wadau wakalipuka mmeona kadaraja kanakojengwa yaani aibu tupu. Tusikurupuke jamani hii miradi ni kwa faida ya wabongo wote. Mimi ambaye nilianza pata fahamu late 70s na nilisafiri na kuishi sehemu mbali mbali bongo hapa najua umuhimu wa hii miradi. Tulikotoka ni giza nene. Sasa anapotokea kiongozi Mwenye ujasiri wa kufanya mambo makubwa (sio CCM) tumuunge mkono. Wewe unabeza ule mradi lkn wakazi wa maeneo hayo ni neema kwao. Fursa zimefunguka na wao wanaonja matunda ya uhuru. Maendeleo yanafika huko sasa kupitia mradi huo. Barabara inajengwa kwa kiwango cha lami, maji ya bomba yatafika kiulaiiini. Kijijini kwetu mpaka mjini ni km 18 tu unakwenda Town na baiskeli na bodaboda. Miaka yote Barabara imekuwa mbovu sana. Alipokuja Mwamba Magufuli Ameamuru hospitali ya wilaya ijengwe kijiji kimoja kabla ya kufika kijijini kwetu ukitokea mjini na makao makuu ya halmashauri yawe hapo. Obvious miundombinu ya kisasa inajengwa sasa tunavyoongea na Barabara ya lami soon mkeka unawekwa. Sasa wakati Wa barabara mbovu tulitumia nusu saa mpaka dk 40 kufika kileji mkeka ukiwekwa 20 minutes tutatumia. hiyo ni private car.
Ukiwa Dar na itikadi zako negative huwezi jua wabongo wenzio wananufaikaje na Mambo Ya Jembe Magufuli (sio Ccm nasisitiza) najua ana mapungufu yake lkn kwenye huduma za kijamii ameweza
 
Natamani nikueleze kwa urefu jinsi hii kazi ilivyo ngumi ila nipo bussy.

Kwanza nakushauri siku moja Nenda hata tour kutembelea kituo kimoja cha uzalishaji wa umeme wa majii...
Utajionea mengi sanaaaaa
Utashangaa sanaaaa
hutaaamini kuna vitu km vinafanyika hapa bongo..
Nakushauri nenda tuu Pangani New HEP.....
Hii ilijengwa na Wa norway,dermak na finland mwaka 1991- 1995,
Imagine kituo kidogo km kile kimejengwa kwa miaka mitano tena kwa ushirikiano wa nchi zilizoendelea zaidi ya tatu....

Kaka unapoona yale maji yamesimama pale juu



Aisee cheka tuuu ila kuna shughuli pevu sana inaendelea huko chini..



Yale maji unayoona yanatiririka



Wala usiumize kichwa, wala hayahitajiki na hayana kazi...

Maji yenyewe yanayohitajika kukupa wewe umeme hutoyaonaaa yanapitishwa chini chini





Yakifika huko ndio kazi yake sasa ya kuzungusha



Turbines(aisee hapa kuna sayansi ndefu siwezi weka).

Generator na transformer zitafanya kazi ya kuzalisha, ku control na kuongeza nguvu ya umeme


Kumbuka huko underground pia ndio kuna makazi ya watu na ofisi za uendeshaji na ku kontrol mitambo, magari vyote vipo humoo



Hivi vyote inabidi vitengenezewe njia yao kubwa sanaa




Matokeo yake ndio haya


Na ukifika ndani ndio hivi sasa


Kwaio ndugu unapoona nje kuna kimya
Jua wenyewe wapo ndanii

Mwishooo
Mtu unaweza kumjibu mwenzako jibu kwa hoja sio panic na vijembee...

Kama hujasoma physics tumia hata geograph au macho kuelewa hiki
 

Attachments

  • Screenshot_2019-12-31-10-49-05.jpeg
    30 KB · Views: 2
Umemjibu vyema kabisa.

Love and peace
 
We jamaa hua unapenda sana utani, ila ukifika kwenye analysis km hizi hua nakuamini sana Asante sanaaa
 

Hapo nilipoongeza FONT SIZE na BOLD kuna hitajika uthibitisho ILI wahusika waweze kujirekebisha.

Ahsante
 
Ni vizuri umeweka kwa faida ya wengi, ila i hope hukudhani kwamba sijui haya..
 
April 7, 2020
Rufiji, Tanzania

LIVE MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA UMEME RUFIJI
Jamaa huyu mhandisi msimamizi mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) a.k.a Stiegler's Gorge anapata shida sana ,anajikanyaga sana pia uoga umemjaa kutetea mradi huu, nini anaficha? Awe wazi kama yule wa SGR Reli Mpya ambaye kitaalamu ametuambia bila kupepesa macho SGR Reli kumalizika yote itachukua miaka 15.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…