Ni mwaka wa tano sijaenda kanisani ila nasali na kusaidia watu naowambea Mungu awasaidie, Kanisani nitarudi iwe kama sehemu ya kusocialize zaidi

Jf kila mtu ni tajiri, sasa tajiri unapata wapi muda wa kuandika sana au ni kazi ya machawa.
 
Sawa, kwenda kanisani kuna umuhimu lakini sio kwa makanisa haya ya sikuhizi, Ymaepoteza kabisa asili
Achana na ASILI focus na MUNGU ninachoamini MIMI ukiwa mtu wa Rohoni kweli kweli umemshika Mungu bila janja janja huwezi kuacha kwenda kusali kisa mambo ya hovyo yaliyoshamiri makanisani sasa hivi hizi ndizo nyakati zilizotabiriwa za Mwisho hivyo ni kuendelea kujihadhari (Ufunuo wa Yohana 22:11,Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

Mfano jana nimeenda kanisani kuna style imechezwa na wana kwaya ni style ya hovyo kabisa na wala mchungaji hakuikemea(binafsi mimi hilo swala lilinikwaza) lakini je, nikache kwenda kanisani kisa hayo? Ninachojua mimi naenda kumtafuta Mungu hayo mengine wahusika watayatolea hesabu wenyewe
 
Sawa, kwenda kanisani kuna umuhimu lakini sio kwa makanisa haya ya sikuhizi, Yamepoteza asili

Hata kiboko ya wachawi alikuwa na kanisa
Hao wanaoenda kwa kiboko ya wachawi ukiwauliza kuwa hayo ndiyo makanisa ambayo wamejengewa msingi kutoka kwa wazazi wao watajibu ndiyo? au ni wale wanakusanyika ili kutafuta miujiza na siyo kumtafuta Mungu.
 
kwani unafikiri UKRISTO ni kwenda kanisani?je unafikiri mtu ataiona pepo kwa kwenda kanisani kila j2???
Kwenda kanisani ni moja wapo ya kigezo cha kuitwa mkristo bila hivyo makanisa yalijengwa ya kazi gani? Kwenda kanisani kila jpili siyo guarantee ya kwenda mbinguni lakini ni ticket kubwa ya kumjenga mtu kiimani na kumfanya ikiwa amepata neema kwa Mungu aache mambo mabaya na kutenda mema apate kibali cha kwenda mbinguni.. Huwezi kujichimbia tu ndani unaacha kwenda kwenye nyumba za ibada eti unategemea kwenda mbinguni...mimi sijihesabii haki na sijui mwisho wangu kama nitaenda mbinguni au sitaenda ila jambo ni nalojua ni kuwa ni muhimu kwenda kanisani.
 
Uko vizuri, but don't judge....
 
Haya Bwana
 
Unachofanya ni kizuri pia
Lakini itakuwa vyema zaidi kama utahudhuria kanisani
Kanisani ni nyumbani Kwa Mungu, ona uzito wa kwenda nyumbani Kwa Mungu( kanisani)
Mungu ni omnipresent
 
Huhitaji kwenda kanisani/msikitini ili kuwa na utu na kusaidia wahitaji msaada.
Ni 'common sense'.

Epuka dini. Ni chanzo cha sonona na hofu juu ya mambo yasiyo na hakika.
 
Hata papa akiwa shoga wewe nenda kanisani kama kawaida.
 
Kunaupotoshaji mkubwa unaendelea kudhani kusaidia wasio jiweza nk bila kujumuika na wenzako usali inatosha hapana,pia kunaulazima Sala za Jumuiya ushiriki
 
Kanisani Ni sehemu ya kujumuika ( kusocialize) pale kila mtu anayake sasa ukiwa serious na mambo ya kanisa utachoka mwenyewe, muhimu zingatia juiya na kanisani jpili makorokoro mengine achana nayo, sijui kwaya, sijui uzee wakanisa, sijui mtunza azina, sijui maombi ya nyumba kwa nyumba ( tena hii ndio kihama na utachukia kanisa lenyewe) na makorokoro mengine, wewe jpili nenda kanisani pita hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…