Ni mwaka wa tano sijaenda kanisani ila nasali na kusaidia watu naowambea Mungu awasaidie, Kanisani nitarudi iwe kama sehemu ya kusocialize zaidi

Jf kila mtu ni tajiri, sasa tajiri unapata wapi muda wa kuandika sana au ni kazi ya machawa.
 
Sawa, kwenda kanisani kuna umuhimu lakini sio kwa makanisa haya ya sikuhizi, Ymaepoteza kabisa asili
Achana na ASILI focus na MUNGU ninachoamini MIMI ukiwa mtu wa Rohoni kweli kweli umemshika Mungu bila janja janja huwezi kuacha kwenda kusali kisa mambo ya hovyo yaliyoshamiri makanisani sasa hivi hizi ndizo nyakati zilizotabiriwa za Mwisho hivyo ni kuendelea kujihadhari (Ufunuo wa Yohana 22:11,Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.

Mfano jana nimeenda kanisani kuna style imechezwa na wana kwaya ni style ya hovyo kabisa na wala mchungaji hakuikemea(binafsi mimi hilo swala lilinikwaza) lakini je, nikache kwenda kanisani kisa hayo? Ninachojua mimi naenda kumtafuta Mungu hayo mengine wahusika watayatolea hesabu wenyewe
 
Sawa, kwenda kanisani kuna umuhimu lakini sio kwa makanisa haya ya sikuhizi, Yamepoteza asili

Hata kiboko ya wachawi alikuwa na kanisa
Hao wanaoenda kwa kiboko ya wachawi ukiwauliza kuwa hayo ndiyo makanisa ambayo wamejengewa msingi kutoka kwa wazazi wao watajibu ndiyo? au ni wale wanakusanyika ili kutafuta miujiza na siyo kumtafuta Mungu.
 
kwani unafikiri UKRISTO ni kwenda kanisani?je unafikiri mtu ataiona pepo kwa kwenda kanisani kila j2???
Kwenda kanisani ni moja wapo ya kigezo cha kuitwa mkristo bila hivyo makanisa yalijengwa ya kazi gani? Kwenda kanisani kila jpili siyo guarantee ya kwenda mbinguni lakini ni ticket kubwa ya kumjenga mtu kiimani na kumfanya ikiwa amepata neema kwa Mungu aache mambo mabaya na kutenda mema apate kibali cha kwenda mbinguni.. Huwezi kujichimbia tu ndani unaacha kwenda kwenye nyumba za ibada eti unategemea kwenda mbinguni...mimi sijihesabii haki na sijui mwisho wangu kama nitaenda mbinguni au sitaenda ila jambo ni nalojua ni kuwa ni muhimu kwenda kanisani.
 
nalifikira na kulitathmini jambo hili.

Tatizo makanisa mengi yamepoteza originality, Leo hii unaenda kanisa la Anglikana au Roma viongozi wameruhusu ushoga lakini maaskofu wetu hawajajimegua, why ??? ni tamaa za vyeo , pesa, ?

Unaenda kanisani wanawake wanakuja wamevaa vinguo vya kuwachoresha maumbo wanaruhusiwa tu kuingia, sio kama zamani ilikuwa marufuku.

Ukienda kwa wasabato nao wanaanza kupoteza originality wanaruhusu wachungaji wa kike, wachungaji wao wanapiga panki, n.k.
Uko vizuri, but don't judge....
 
Utaratibu wangu mara mbili au tatu kwa wiki nikitoka kazini mida ya jioni huwa napaki gari maeneo kadhaa kwa dakika 10 hadi nusu saa naanza kuzunguka nikiona bibi anauza karanga nampa elf 5 ntachukua karanga za mia sichukui chenji, mtoto anaeuza ndizi ntampa elf 2 naweza nisichukue ndizi, mwanafunzi kiatu kimegaribika ntampa elf 10, watoto wa mutaani ntamsaidia elf 3, n.k. kwa mwezi naweza kutumia elf 80 hadi laki 1 na elf kadhaa si haba japo kipato changu kidogo, Sheria yangu sipendi watu wanijue hivyo nafanya kwa kificho, sipendi kurudi sehemu moja hadi mda upite, siwezi kumsaidia mtu wakati wengine wananiona, n.k. ni kwa ulinzi wangu pia.

Sisaidii kusema kwamba nategemea baraka, kufutiwa dhambi, kujihakikishia kwenda mbinguni. NO ! NO ! HAPANA !! misaada unayotoa haiwezi kuwa rushwa, God cant be bribed !! nafanya kibinadamu tu lakini hata kwenye maombi yangu navyofikia kusema "Mungu wasaidie na watu wenye shida mbali mbali" basi nami najua kwa mbali sana nimeweza kutoa chochote ila narudia tena "bila mategemeo ya kupewa baraka"

Nasali kila siku, sijawahi kulala bila kusali, kula bila kusali, kuomba msaada wa Mungu napokuwa na shida, n.k. lakini kuhusu kwenda kanisani sijaenda kwa miaka 5 tangu 2019,

Sababu zangu za kuacha kwenda kanisani ni kwamba makanisa yanazidi kupoteza asili yake / originality mbaya zaidi hayakemei kama zamani, ni kweli tumeambiwa tusali kwa kukusnyika lakini ni vema kuitathmini
sehemu unayokusanyika.
  • Leo hii tunajua ni wazi kabisa kanisa la Roma likiongozwa na papa wake lina waraka wa kusapoti mahusiano ya jinsia moja, Ukienda anglikana viongozi walisharuhusu mapema haya mambo, kwanini haya makanisa yasijimegue ? maaskofu wanathamini zaidi vyeo na maslahi ?
  • Sikuhizi makanisani wanawake wanavaa wanavyotaka, magauni yanayowabana shepu zinachoreka, migongo wazi, vifua vimeachwa, n.k. sio kama zamani walikuwa wanazuiwa getini, utawasikia kinachoangaliwa ni roho.
  • Wanawake wanahubiri makanisani, makanisa kama lutheran yanaruhusu wanawake lakini haikuwa hivyo hapo mwanzo
  • Migogoro ya maslahi, Kanisa kama Kkkt limekuwa na migogoro mingi sana, ukichunguza chanzo ni maslahi na vyeo
  • Wasabato nao wanazidi kubadilika kila kukicha, wachungaji wanachonga panki, vijana wao wengi wana watoto bila ndoa, kuruhusu wachungaji wa kike, n.k.
  • Huko kwa walokole ndio kabisaaa, siwezi fikiria hata kukanyaga, ndio wanaofanya zaidi ukristo uonekane ni kutuko, yamegeuka kuwa makanisa ya kutajirisha wachungaji, miradi ya familia kwa kuuza huduma kama kumuona mchungaji, Mafuta ya upako, keki za upako, na takataka nyingine, hivi majuzi tu Kiboko ya wachawi kawacheka sana waliokuwa wanampa pesa awaombee

Kanisani naweza kurudi lakini wala nisiwe mnafki nitarudi zaidi kwajili ya mambo ya kusocialize
Haya Bwana
 
Huhitaji kwenda kanisani/msikitini ili kuwa na utu na kusaidia wahitaji msaada.
Ni 'common sense'.

Epuka dini. Ni chanzo cha sonona na hofu juu ya mambo yasiyo na hakika.
 
Hata papa akiwa shoga wewe nenda kanisani kama kawaida.
 
Kunaupotoshaji mkubwa unaendelea kudhani kusaidia wasio jiweza nk bila kujumuika na wenzako usali inatosha hapana,pia kunaulazima Sala za Jumuiya ushiriki
 
Kanisani Ni sehemu ya kujumuika ( kusocialize) pale kila mtu anayake sasa ukiwa serious na mambo ya kanisa utachoka mwenyewe, muhimu zingatia juiya na kanisani jpili makorokoro mengine achana nayo, sijui kwaya, sijui uzee wakanisa, sijui mtunza azina, sijui maombi ya nyumba kwa nyumba ( tena hii ndio kihama na utachukia kanisa lenyewe) na makorokoro mengine, wewe jpili nenda kanisani pita hivi
 
Back
Top Bottom