JokaKuu, mojawapo ya mambo mabaya sana ambayo yametokea na yanaendelea kutokea ni hii imani kuwa migogoro ya kisiasa mwisho wake ni ubaya tu. Demokrasia hujengwa kwa migogoro, kupingana na wakati mwingine huokolewa kwa jasho na damu. Hakuna nchi iliyojenga demokrasia ya kweli bila mivutano, misuguano, na hata minyukano. Sasa minyukano si lazima kwa demokrasia, lakini mivutano ni lazima. Tusiogope hii mivutano vinginevyo itakuwa ni kujaribu kuahirisha kisichoepukika. Hofu yangu tunajaribu kuchelewesha kinachotakiwa kufanyika.
Look here, kuna baadhi ya mambo serikali hii inafanya ni mazuri na hata wapinzani wanakiri. But call a spade a spade. Kinachoendelea nchini sasahivi siyo "mivutato" tu. Ni full-blown dictatorship. Marufuku inatangazwa na ukienda kinyume unakamatwa unawekwa ndani. Au unabambikiwa mashtaka yasiyo na dhamana. Ukiwa una bahati mbaya zaidi, utakutwa tu mahali ukiwa umepigwa uko hoi au hutaonekana kabisa. Umeshawahi kujiuliza kwanini hakuna kesi hata moja ya watu kuokotwa wakiwa wameumizwa, kupotea, kupigwa risasi ambayo imekuwa resolved awamu hii? Rais anazungumzia mpaka magomvi ya watu binafsi jukwaani lakini hazungumzii matukio ya kutisha yanayowatokea wananchi wake? Hujifunzi kitu chochote tu hapo, au ni makusudi?