Uchaguzi 2020 Ni Mwaka wa Uchaguzi Mkuu 2020: Kuthibitisha au Kutengua Maamuzi ya 2015?

Taja mikoa na majibu ambayo CDM ilishinda. Hii ya kila uchaguzi kuwa CDM ilishinda ni strategy za kijinga ili wakuu wa Sacco's wasichukuliwe hatua za kichama. Nyumbu wanafuata bila kuuliza maswali magumu. Long way to go
Kwa ujumla mgombea wa UKAWA alipata zaidi ya kura mil 10 , Mgombea wa ccm alipata kura mil 3 unusu tu , Kinana , January , Kapilimba na JK wanalifahamu hili , haikuwa rahisi kwa mtu mwenye akili timamu kumchagua Magufuli .

Na hii laana ya kuiba kura ndio inayowatafuna akina Kinana , January na Kapilimba , bado Kikwete naye yake yanaandaliwa mwaka huu
 
Wewe Mzee inaonekana umepata bwana mpya, babu la kizungu.

Una unafiki uliokomaa na kuvuka mipaka
 
CCM itaendelea kuendesha nchi kwa miaka yote, sababu hakuna upinzani makini na mahiri wa kuweza kushindana na chama dola kwa hivi sasa, vyama vya upinzani vimetezwa nguvu na watanzania wengi ni watu wa maslahi, kura zao zinanunuliwa kwa thamani ndogo za fedha na wengine huhadaiwa kwa lugha nzuri za ahadi zisizotekelezwa, tumeona jinsi ya wabunge na baadhi ya watu waliyo hamia CCM kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za raisi Magufuli, wangeweza kumuunga mkono kwa juhudi anazozifanya raisi bila ya kuhama vyama, lakini kwa jinsi tulivyokuwa wadhaifu ndiyo maana hatuwezi kujenga upinzani madhubuti. Inavyoonyesha watanzania hawajali sana mambo ya siasa ndiyo maana ni watu wachache waliyoandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ukilinganisha na idadi ya watu wa Tanzania, elimu ya siasa na hata ya uraia ni tatizo kwa wananchi wengi, na hata hao wachache wenye ufahamu wa elimu hizo bado kuna changamoto za utekelezaji wa elimu hizo. Cha msingi watanzania waamke na wajiulize nini wanataka na wapi wanataka kwenda na nini ni vipaumbele vyao.
 
Nami namsubiri hapa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nanye Go,
Siasa hazijazuiliwa bana; usiamini sana maneno hayo. Siasa zinafanyika na ni jambo baya kukubali kuwa siasa zimezuliwa. Sasa kama hakuna siasa uchaguzi utafanyikaje?
Makatazi ya kufanya siasa yapo na ushahidi upo. Zanzibar Maalim Seif alisababisha Naibu waziri wa mambo ya ndani , Masauni kumuagiza IGP kumchukulia hatua RPC wa mkoa wa Pemba kwa kushindwa kudhibiti mikutano ya Maalim Seif.

Kule Hai hata KUB na mwenyekiti wa CHADEMA taifa kaamriwa kuongelea mambo ya Hai tu, siyo ya Tanzania nzima.

Tumemuona Bashiru na wenzake ccm wakichanja mbuga kila kona ya Tanzania,
Kwangu Lugola waziri wa mambo ya ndani alisema washughulikiwe bila huruma wote watakao bainika kufanya siasa wakati wakifahamu mikutano ya siasa imezuiliwa lakini hatujasikia Polepole na Bashiru wakishughulikiwa.

List ni ndefu, unataka nikuamini wewe?! Vipi hawa viongozi wenye dhamana?!

Labda ulitaka kusema, siasa za ccm hazijazuiliwa, lakini tutachaguaje ikiwa ccm pekee ndiyo wanaweza kuruhusiwa kufanya siasa?!
 
Kalamu1,
Hivi, wakati wa Kikwete upinzani uliruhusiwa sana kufanya siasa bila vizingiti vyovyote? mbona siasa zilifanyika pamoja na songombingo zote za kisiasa?
Mzee Mwanakijiji, ukweli mbona uko wazi mkuu, tofauti ya kufanya siasa wakati wa Kikwete na wakati huu wa Magufuli.

Hili nalo kweli ni jambo la kupotezea muda kulijadili hapa? Hapana, tusipoteze muda.
 
JokaaKuu, yote hayo ya Kampeni za kudumu zilizofanywa na Magufuli huku akiwazuia wapinzani wake hata kule kuitisha tu mikutano ya hadhara ili wazungumze na wanachama wao.

Kama Magufuli anajiamini kwamba Kampeni alizofanya zimemsaidia, aachane na kuvuruga kura wakati wa uchaguzi; wananchi wachague kwa utashi wao wenyewe.

Kama kampeni zake alizofanya zimewakoga nyoyo, si watamchagua yeye? Hofu ya kuingilia na kuvuruga kura za wananchi anazitoa wapi tena.

Hilo la Kampeni sasa ni historia, hatuwezi tena kurudi nyuma. Aachie timu B nao sasa wajifue ipasavyo kabla ya kuingia uwanjani, na uwanja uwe sawa pande zote mbili.

Hili ndilo lililo mhimu, na anajua hawezi kuruhusu iwe hivyo kwa hofu kubwa aliyonayo.

Ataanguka vibaya sana!
 
85%+ inamhusu Rais Magufuli, hakamatiki na sioni wa kupambana naye,time will tell.
Hana wa kushindana nae kwanini?
1. ndani ya chama kuna watu watashindana nae
2. tume ya uchaguzi sio huru
3. sio mwanasiasa ni mbabe
 
You earn a lot of respects when you stand in these profoundly true lines.

What makes you vacillate?
 
Kwenye tume huru ya Uchaguzi na vyombo vya dola vikiwa pembeni Magufuli hawezi kushinda hata akishindanishwa na Bata.
 
Kiranga, hili ni suala la strategy; what should they do? fight a losing battle, or fight a battle that they could win or even draw?
How do you define losing?

If the opposition increases its vote in parliament and the percentages of votes against Magufuli, relative to the last election, that is not losing, that is gradual winning.

Complaining about 2025 constitutional violations by "president Magufuli" when we haven't even voted him for the presidency in 2020 is sending a psychological message that the opposition considers the presidency a lost cause.

If you want to fight a battle you could win or draw, you don't start with a message that will demoralize your soldiers, proclaiming imminent defeat.

Yani kwetu ni vituko kuanzia serikalini mpaka upinzani.
 
Kiranga, hili ni suala la strategy; what should they do? fight a losing battle, or fight a battle that they could win or even draw?
Siku upinzani ukishika nchi CCM ndio ita define kwamba what it did to oposition was right or wrong.
 
Unaposema, je, tuendelee na Magu au la una maanisha kuna uchaguzi. Hivi kwako ni kweli kuna uchaguzi Tanzania siku hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…