Ni Mwambe au Kikwete yupi muongo kuhusu mkataba wa Bagamoyo?

Si kuna watu wa mjini walilipwa fidia? Sasa ilikuwaje watu wakalipwa fidia bila mkataba? Mbona tunadanganyana?
 
Ulikuwa unamuamini kweli mtu yule?
 
Si kuna watu wa mjini walilipwa fidia? Sasa ilikuwaje watu wakalipwa fidia bila mkataba? Mbona tunadanganyana?
Watu mbona mnachanganya mambo, sasa watu kulipwa fidia kea eneo kutaka kutwaliwa ndio kunahitaji mkataba wa ujenzi wa Bandari? Hiyo inaweza kuwa sehemu ya roadmap ya utekelezaji tu haina connection na mkataba wa ujenzi wa Bandari. Tafadhali msichangaye mambo.
 
Na jiwe la Msingi mlilozindua? Napo mkataba ulikua bado? Acheni uongo bana
Huwezi kuweka na kuzindua jiwe la Msingi ikiwa hamjakubaliana
Yanaanza makubaliano(mkataba) ndio inafata kuweka jiwe la Msingi, alafu ujenzi ndio unaanza.
Yaani kabisa uanze kufyeka na kuweka mipaka ya shamba kabla ya kulinunua?
 
Mkuu hata una uandishi mbaya kiasi hiki? Hauzijui Nomino?

Ona huyu nae,hizo nomino ndiyo zimefuta mantiki ya hoja zake? Nilidhani unasoma hoja zake kumbe umeng’ang’ana na nomino kama mwalimu wa kiswahili darasa la nne.
 
Kama JPM alikuwa anasema yaliyokweli kwann na yeye huo mkataba wa bandari ya bagamoyo hakuuweka wazi. Mbona na yeye alikuwa anaingua mikata ya Siri Hadi leo wananchi hatuijui? Kizazi kilekule cha Panya ila ndio viongozi tofauti hamna jipya
Huwa nawadharau sana watu walikuwa wanamuamini Magufuli, hili lazima niliweke wazi. Magufuli aliponda mikataba ya Bandari ya Bagamoyo na Gesi ya Mtwara bila kuiweka wazi. Lakini MAGUFULI huyo huyo akatumia Matrilioni ya fedha za walipa Kodi wa Tanzania kujenga miundombinu mikubwa na isiyo na tija wilayani Chato bila idhini ya Bunge.

UKIWA na AKILI huwezi kufanya reference kwa kauli za MAGUFULI. He was jealous and a diasaster. Nafuu ALIKUFA mapema kabla jajatupeleka pabaya sana
 
Mradi gani uliojengwa kwa matrillion chato? Tafadhali naomba unitajie
 
Mradi gani uliojengwa kwa matrillion chato? Tafadhali naomba unitajie
Jumlisha gharama za kujenga Chato Airport, CHato Referral Hospital, Chato Burigi National Park, VETA Chato, Chato Stadium, Chato Port etc
 
Jumlisha gharama za kujenga Chato Airport, CHato Referral Hospital, Chato Burigi National Park, VETA Chato, Chato Stadium, Chato Port etc
Unaijua trillion? Burigi national park?national park toka lini ikajengwa?
Chato stadium? Hizi story huwa mnazitoa wapi?
Chato port? Hata huko chato.unapajua kweli?
 
Unaijua trillion? Burigi national park?national park toka lini ikajengwa?
Chato stadium? Hizi story huwa mnazitoa wapi?
Chato port? Hata huko chato.unapajua kweli?
Wewe ndiyo hujui kitu. Nimekutajia vitu alivyo peleka kwako bila idhini ya bunge. Kisha nikasema tafuta gharama mwenyewe ulete hapa. Badala ya kuzileta gharama unaniuliza kama naijua Trilioni.

Wakati Kalemani anasema atajenga Stadium wewe ulikuwa wapi?
 
Alitumia trioni ngapi mangi
 
Acha ujinga kama huna kitu kichwani jifunzi kuuliza na kusoma comment za wenzako htuopungikiwa na kitu
 
17/10/2015 Kikwete akaweka jiwe la Msingi!
Hapa kumbuka Kikwete alikuwa amebakiza siku 7 za kukaaa Ofisini kumpisha Rais ajaye/Magufuli. Alichofanya ni mbinu za kimedani kuhakikisha Rais ajaye hakwepi huu mradi
 
Ungetwambia kuna mkataba fulan uliofungwa katk utawala kikwete ungeeleweka, na sio jiwe, hilo ni jiwe sio mkataba, ebu turidhishe basi kwamba kina mkataba tayr ulisainiwa
 

Mradi wa kimataifa unatolea mfano wa miradi ya mbio za mwenge maajabu hayataisha nchi hii. Yote kwa yote jiwe la msingi huja baada ya hatua zote za awali ikiwemo feasibility na mkataba..ni sherehe ya kuadhimisha mwanzo wa utekekezaji...
 
Serikali imekanusha kutokuwepo mkataba kati ya Tanzania na mwekezaji kutoka China wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo,huku kumbukumbu za hotuba za Rais @jmkikwete zikionyesha mnamo 14/10/2015 alizindua mradi huo wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo,je alizindua bila kuwepo mkataba? https://t.co/32rk2rLeLE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…