Ni Mwanayanga mwenzangu lakini kwa hili nimemdharau sana

utoto mwingi.. plus nati moja lazima ilegee kidogo linapokuja swala la uweledi haswa ukiwa mshabiki kindakindaki wa hizi timu mbili.
 
Hakuna uadui wowote wa Simba na Yanga. Huo ni uoga wako tu. Ulishawahi ona derby ya AFC Leopards na Gor Mahia? Ule ndo uadui maana hadi wanaumizana. Changamoto za kwenye utani hazikosekani. Bila Simba na Yanga tutarudi kwenye mambo ya siasa na ukabila. Kuna nchi jirani nimeona wananchi wanalalamika eti timu ya taifa ya mpira wa miguu imewekwa watu wa kabila moja!!!... Simba na Yanga ni zawadi ya Mungu kwa watanzania.
 
Nimemkumbuka Dismass Ten jamaa alikuwa mweledi sana lakini yanga ikadorora
.boss wangu Bumbuli pia alikuwa mweledi lakini akaletewa Nugaz ili kuchagizwa .
Watu wa hovyo huongozwa kihovyo hovyo
Dismass ten alikuwa ana elimu. Bumbuli alisimamia profession akaemda tafutiwa mtu wa kuropoka ropoka.
 

Hadi hili la uadui unataka kubishana nalo? Uadui sio lazima watu wapigane. Uadui ni hali ya kutokubali, kutopenda (kuchukia) lolote lile ambalo mwenzie litamfanya asonge mbele na kutokuwa tayari kushirikiana katika jambo fulani. Sio siri hapa Yanga ilipofikia kuna watu wana tamani isingefika hapo na hata hiyo kesho wapo tayari kufunga na kuomba ili Yanga isiwe bingwa. Na hiyo hali haipo kwa mashabiki wa Simba pekee bali hata wa Yanga walitamani Simba isiingie hata hatua ya makundi. Hizi zetu mbaya zimejengeka kutokana na mifumo iliyowekwa ya kuona Simba na Yanga ni maadui.

Embu fikiria tu kitu kimoja, hizi timu mbali na kukutana katika mechi za mashindano hauwezi kukuta wenyewe kwa wenyewe wana panga kucheza mechi za kirafiki za kujiandaa labda na mashindano fulani au hata tu viongozi kukutana katika ku share mambo kwa maslahi mapana ya taifa.
 
LAZIMA ATAPATA ADHABU KWA MUJIBU WA KANUNI 7

KIFUNGO CHA MIEZI MITATU NA

FAINI YA SHILINGI MILIONI MOJA.
 
Huyo dogo enzi zake hadi PM Majaliwa alikuwa anaupigia chepuo uchambuzi wake tena bungeni kumbe ni kajinga tu.

Azam Fc wamewahi kuwa na afisa habari akiiwa Somebody Maganga wana la kujifunza kutoka kwake.
 
Badala ya msemaji awaombe watani waje watoe sapoti kwenye jambo la kitaifa yeye analeta matamko ya kilimbukeni na viashiria vya utengano. Vitu kama hivi alikuwa akivifanya Haji Manara alipokuwa Simba na kuwafanya wanayanga wawe wanaenda kuipokea timu ngeni kule Airpot na kuwasaidia ulozi ili mtani asishinde.

Ni muhimu sana tutoke kwenye ushabiki wa hivi. Tunakuwa chanzo cha kuwatia hasira na chuki watu wengine ambazo hazikuwa na ulazima.
Kauli kama hizi zitatoa viashiria vya laana na kupelekea Yanga kufungwa.
 
Wewe jamaa unafurahisha sana... sasa Simba na Yanga wakutane ili nini? Wao wanatakiwa kukutana uwanjani sio kwenye mambo yenye harufu ya siasa. Maslahi mapana ya taifa yashughulikiwe na TFF, BMT na wizara kwa ujumla. Arsenal na Man huwa zinakutana ku-share mambo kwa maslahi mapana ya England? Huo unaonekana uadui ndo unanogesha ligi na kuleta ushindani mkali.
 
From one of the best pundits to one of the worst ever spokesmen we have had in Tanzania
 
Ukiwa na timu yenye uongozi mzuri na wachezaji wakaperfom vizuri uwanjani huna haja ya kuwa na Msemaji mwenye mdomo mchafu. Eti ahamasishe watu waingie uwanjani. NONSENSE!!
Inafika mahali mnadhalilisha hadi utu wa mtu halafu mnajificha kwenye kichaka cha Utani Wa Jadi. Wazembe Sana!

Matokeo na performance ya timu ndio itachangia viwanja vijae, brand ya timu ikue.
Matusi na majibizano yasiyo na msingi waachiwe mashibiki, kiongozi inabidi acheze nafasi yake kama kiongozi.

You wanna be a Pro, You gotta think like a Pro, Do Like a Pro, Act Like a Pro.
 
Ally Kamwe alikuwa kijana Bora sana kipindi yupo pale Azam Tv akichambua soka,Cha kusikitisha Young Africa imepoteza akili zake zote amebaki hohehahe.
 
Nadhani angetania timu na sio mtu binafsi,ni utoto wa hali ya juu,sema asamehewe tu kama ashaomba radhi.
 
Dogo niliwahi kuskia kua ni shoga , wenye habari kamili tupeni basi

Wnaliwa na nani huyu dogo ??
 
Hata mimi kanikera sana credibility yake kwangu imeshuka, yule ni kama mzazi wake isitoshe Mgunda Hanaga shida na Yanga.

Anyway ujana ni maji ya moto, anaendelea kujifunza
 
Hata mimi kanikera sana credibility yake kwangu imeshuka, yule ni kama mzazi wake isitoshe Mgunda Hanaga shida na Yanga.

Anyway ujana ni maji ya moto, anaendelea kujifunza
Mgunda ni coach mmoja yupo peace sana. Huwa namweshimu hana maneno ya kiswahili swahili. Dogo anakosa akili sana.
 
Mgunda ni coach mmoja yupo peace sana. Huwa namweshimu hana maneno ya kiswahili swahili. Dogo anakosa akili sana.
Binafsi hata kama ilifungiwa nitaona poa tu huenda akajifunza jinsi ya kuongea kwa heshima na Adabu, shida kubwa naiona kwa hawa wasemaji wanajaribu sana kuvaa viatu vya Manara wasichojua ni kubwa kila mtu ameumbwa kwa hulka na jinsi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…