Ni mwezi wa pili sasa tumenuniana mi na mke wangu

Ni mwezi wa pili sasa tumenuniana mi na mke wangu

Mwanaume hanuni ,wewe ndiyo kichwa cha familia unapaswa kusolve matatizo ya familia ,ndoa nyingi sasa hivi kwa sababu wanaume hawasimami katika nafasi zao,ndiyo maana tunapata watoto na Taifa lisilo na maadili kwa sababu ya wanaume kama ninyi
Nani kakuambia mwanaume hanuni, wanaume wananuna sana tu sikuhizi...siiti kununa, ila kukaa kimya. Unapigiwa buyu hadi ushangae.
 
Mwanamke anayekupenda kabisa akae miezi miwili bila kukutafuta...kuna kitu hakiko sawa hata kidogo.
 
Pole mkuu,

Kamwe usiishi Kwa kushindana na mwanamke.

Wewe endelea na mambo yako, jua kwamba Yule ni mama Yao hawezi kuwatupa wala kuwapa Sumu.

Akikumiss au akiwa na shida atakutafuta.
Mzee wa hall V, umeongea km baba na mume wa mtu.
[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
img_1_1741769627686.jpg
 
Wewe ndowakumaliza tatizo sio yeye jua nafasi yako kama mume na kumbuka kadri unavyomueka mbali nawe humkomoi bali unamtengenezea usugu wa moyo
 
Aisee pole sana muda wote huo na hajakutafuta🤐yaan hata kwenye mawazo yake haupo duh.
Mtafute labda mjaribu kuongea kama ataelewa na atakuwa tayari kubadilika
 
Ndoa Ndoano
Ni mke wangu wa ndoa na tuna watoto copy yangu kabisa
Kutokana na migogoro ya hapa na pale tulitengana ila tulikua tunawasiliana kujua hali za watoto
Mara zote mimi ndo nilikua napiga simu kujua hali zao
Sasa kuna tukio alifanya ambalo lilinikata mood kabisa ya kuendelea kumpigia pigia simu hivyo nikaacha na nilitegemea atapiga kuomba msamaha kwa tukio alilonifanyia na tuweze kujadili ili kuweka mambo sawa
Ila ni mwezi wa 2 sasa unaisha hakuna mawasiliano nami nimeamua nimpotezee mazima hadi pale atakapokuja kudai talaka.
Mke ni mwajiriwa mkoa jirani na ninapoishi so yupo huko anakofanyia kazi
Je nimtafute au nikomae tu na harakati zangu za maisha??
watoto wanakaa na nani??
 
Unavyozidi kumpotezea ndivyo unazidi kumuweka mbali. Jishushe okoa ndoa yako then set standards na uhakikishe anazifuata.
Hivi unajua gharama ya mwanaume kujishusha kwa mwanamke?. Akirudi tu dharau zitazidi zaidi sasa hizo standard ataziwekaje?. Alafu inaonekana hujaoa wala kukaa na mwanamke kwa muda mrefu. Bado yamkini mke wako ajafunua kucha zake anakuangalia akasema hiii!. Siku moja uingie anga zake akutende.
 
Back
Top Bottom