Ni myonge, sina kauli na sina hamu ya kwenda nyumbani tena nilipo zaliwa

Tatizo mababa wengi wakipachika mimba na kukimbia, wajomba ndio huwa wanalea. Ukifuatilia scenerios nyingi utagundua watoto waliotelekezwa walilelewa na wajomba zao kwa sababu huwa ni nadra wao kutupa watoto wa dada zao ndio maana wakasema "mjomba ni mama".

Sasa mkuu umefanya uharibifu ukaondoka, baada ya muda unarudi na unategemea aliyekulelea mtoto wako asiwe na sauti?..
 
Mhhh mbona kuna utata

Unamaanisha wazazi walimkataa mchumba wako na mahari zake?
Mleta mada(OP) ni mtoto wa nje ya ndoa.
Anayedhaniwa kuwa baba mzazi wa OP alienda kwa wazazi wa mama wa OP kulipa mahari na gharama zingine kukomboa mtoto(OP) enzi hizo akiwa mdogo nadhani.
Ndugu au wazazi wa mama wa OP wakakataa na kumfukuza huyo baba wa OP.
 
Mbona anamtihani mkubwa
 
Hii story kama huna mawazo ya kausha damu wala betting inaeleweka sana tu,

Mtoa mada ni mtoto wa nje ya ndoa, mama ake hakumwambia baba ake kua ana mimba, mtoto akazaliwa akakua, baba ake baada ya kupata habari kua ana mtoto akaenda kupeleka Ng'ombe na Fedha ili kumgomboa mtoto, babu na bibi wa mtoa mada wakamtimua, kuanzia hapo maisha ya mtoa mada yamebadilika maana kijijini kila mtu anamzungumzia yeye,

Ushauri wake kwa wadada, wasizae nje ya ndoa na kama wakibeba mimba wawajulishe wakina baba mimba wao ili yasitokee yaliyomtokea yeye.

Swali kwa mtoa mada,
Mama yako bado yupo hai?
 
Una umri gani tuangalie namna ya kulea mtoto huyo bidada
 
Hamna mkuu labda ulisoma tu kichwa cha uzi. Ila mleta mada analalamika ya kuwa wazazi wake walikataa mahali.
Mahali ya nanani? Maana story imejichanganya.
 
Sema huu ni upumbavu kumnanga mtoto kwa vile hana kosa kabisa ,hili ishu inatokea sana .
 
Mtoa mada yeye sasa ndiyo amtafute baba yake maana kesha kua mtu mzima na hakuna atakae mzuwiya!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ