Ni namna ipi nzuri ya kuishi na mwanamke anayependa kuelezea mambo yenu ya faragha kwa marafiki zake?

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
5,603
Reaction score
14,183
Habari zenu wakuu..

Duniani hapa kuna mambo ya kustaajabisha sana. Huenda labda kwakuwa kila mmoja na hulka yake ndio maana mambo ya kustaajabisha yanazidi kutokea kila uchwao.

Nina huyo wife, sijajua sababu ya furaha zake au vinginevyo, au kutaka aonekane bora kwa wenzake basi mambo mengi ya sirini kati yetu hupenda kuyatoa kwa rafiki zake huko. Sikuwahi kujua before.

Leo majira ya asubuhi aliniaga anatoka kwenda hospitali kumpeleka mtoto kwakuwa ana dalili za homa, ila hakuondoka na simu yake kubwa akabeba kisimu kadogo. Kwakuwa nilibaki peke yangu, ikabidi nianze kupekua huku na kule kunako simu yake kwakuwa pattern yake ni nyepesi tu.

Katika kuzunguka huku na huko nikaenda Whatsapp kwake kuona kuna nini cha zaidi. Nikaanza kupitia chattings baadhi. Nikakutana na messages akiwa kachat na watu kama watatu ambao ni marafiki zake. Mmoja nilifanikiwa kumtambua kwa DP yake, huwa anafanya biashara za uwakala.

Mambo niliyokuta humo ni ya ajabu ajabu tu, nimeona majadiliano ya kuhusu sisi waume zao. Yule kaeleza mambo yake humo kuhusu mumewe na huyu wangu kamwaga mambo kibao tu ambayo huwa tunayafanya ya faragha ikiwa pamoja na anapelekaje moto, maumbile na mengine mengi kama hayo. Imenishangaza sana na sikutegemea wakuu. Ukizingatia ofisini kwa huyo dada huwa naenda mara kadhaa kupata huduma, kuna utani huwa anaufanya kwangu nauchukulia kawaida ambao leo ndio nimeunganisha dots na kuelewa kuwa unatokana na hayo mazungumzo yao.

Binafsi huwa sipendi habari zangu za faragha kusambaa kwa watu hasa ambao wapo mazingira ninayokuwepo, sababu ni kama kuvuliwa nguo. Sijamueleza chochote wife kuhusu hilo, ila ningependa kupata busara kwa wajuzi waliowahi kukumbana na kadhia kama hii, mliwezaje kudeal na hili au kuwaeleza wahusika ukizingatia mimi nimekagua simuni mwake pasipo ridhaa yake?

Imeniumiza sana..
 
Kama hiyo ndio hulk yake na umeongea nae hajakuelewa basi.... tambua kwamba huyo ndio alivyo na mengine sioni kama inafaa kukushauri maana yapo ndani ya uwezo wako.
Yaani namaanisha niwewe ndie mwenye kufaham kama unaweza ukavumilia hiyo tabia yake ama hauwezi ukavumilia and the rest itabaki kua historia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…