Habari zenu wakuu, hongera kwa kila anayewajibika muda huu pia kwa wanaopumzika katika staili zao wajuazo wao.
Naomba nisivute muda na wakati muhimu kama huu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, naomba jadiliane ni namna gani nzuri ya kutoa fungu la kumi?
Je, ni lazima kanisani, au hata kusaidia watu kwa ile asilimia kumi ni sawa? Na kwanini tunatakiwa kutoa fungu la kumi kanisani.
Sina ushahidi wa namna yoyote ya kutoa fungu la kumi kwa kutumia maandiko ya biblia ila nataka kujua kwa wanaojua tujuzane umuhimu katika kujua namna sahihi ya kumtolea bwana Fungu la Kumi.
Karibuni wote.
Somo la matoleo au sadaka limerugwa sana maana ndipo zilipo ofisi za wahusika hapo.
Kifupi kabisa ni kuwa, Mungu amefanya kazi na wanadamu kwa namna nyingi na amekuwa akibadili utaratibu mara kwa mara.
Hapo zamani kabla ya Yesu, wayahudi waliamriwa kutoa matoleo ya namna mbalimbali na kila matoleo yalikuwa na kazi mahususi. Yalikuwepo fungu la kumi, ahadi, malimbuko(mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu, mnyama, ndege na mazao) sadaka za unga, za dhabihu na mengine mengi.
Waisrael waliamriwa kutoa yote na ilikuwa amri kutoa yote hayo.
Lakini mara baada ya Yesu kuja, Mungu alimtoa mwanae kuwa sadaka ya pekee ili kuzifuta sadaka nyingi zilizotolewa na waisrael nyakati zile.
Hivyo ni kusema, nyakati za Yesu hakuna fungu la kumi, hakuna zaka, hakuna ahadi, hakuna malimbuko, hakuna sadaka za dhabihu n.k.
Kitu pekee kilichosalia ni michango/sadaka kwa kadri mtu alivyofanikiwa kwa ajili ya kusogeza mbele injili ya Kristo. Imeandikwa katika 1kor16:1-3. Changizo ni kwa ajili ya watakatifu na si vinginevyo.
Na watakatifu inafanyika kwa namna mbili.
1. Wapo tayari watakatifu ambao lazima hukutana kwa ajili ya Bwana. Ili shuguuli mbalimbali za kumwabudu Mungu zifanikiwe, ni changizo ndiyo hutumika. Lakini pia, miongoni mwa watakatifu, iwapo yeyote ana shida, basi kanisa kupitia changizo lapaswa kumsaidia.
2. Namna ya pili ni ya kitume zaidi. Kuwatafta watakatifu zaidi. Kutoa kwa yatima na wajane au yeyote mwenye kuhitaji ni kuhubiri na ni chanzo cha watu kumrudia Mungu. Kufadhili shughuli za uinjilist ndio kazi kubwa tuliyoachiwa.
Kifupi ni kuwa, sisi sote tu makuhani wa Bwana Yesu. Iwapo wote ni makuhani, haipaswi mtu yeyote aishi kwa jasho la mtu mwingine. Inatakiwa kila mtu afanye kazi ya kumpatia kipato ili awe na uwezo wa kumtumikia Mungu kwa nguvu, akili na moyo pia. Siyo kusubiri michango ya waumini kujilipa posho au mishahara.
Imeandikwa, mchungaji wa mshahara, huyo si mchungaji.