Somo la fungu la kumi ama Zaka ni pana sana ,hasa kwa kipindi hiki ambacho mafunuo mengi yanatokea.
Fungu la kumi lina zama tatu ambazo zote,Mungu anazikubali
1. Kuna kipindi cha kabla ya sheria,enzi za akina Adam,Kaini na Abeli,ilikuwa mtu anatoa kwa kujisikia na Mungu alikuwa anaweza kukataa ama kuikubali zaka yako.
2. Kipindi cha pili ni kipindi cha Musa,Ama wana wa Israel..Walitengenezewa Sheria kuhusiana na matoleo ikiwemo na Zaka yenyewe..ambapo ndio lile neno la "leta zaka kamili"linapatikana sababu ilikuwa na kiwango aina ya mtu na nafasi yake.hivyo ilikuwa tayari kuna kiwango.
3.Zama za 3 ni baada ya Kristo kuja hizi ni zama za Neema,hakuja kuitengua torati ila kuitimiliza yaani hakuja kuivunja sheria ila kuitimiza,hapa utoaji unapewa kipaumbele kwa neema,yaani amri kuu tuliyoachiwa "Upendo" ikiwa na maana ukimpenda jirani yako utamsaidia,utamshauri na kufanya vyote kwa huo upendo.hata katika utoaji ukitoa kwa upendo unabarikiwa zaidi,sasa huku kwa ishu ya zaka ni kwamba unatoa kwa jinsi ulivyobarikiwa na kuvuviwa rohoni mwenyewe na Bwana ataipokea na kukubariki kwa kiwango chako,(Nijaribuni katika matoleo) hii ikimaanisha toa kwa moyo na uaminifu nae atakubairikia zaidi.
Sasa senario ya zaka kikanisa kwanza iko tofauti,kulingana na hali na zama zaka imefanywa kuwa pesa ndio zaka,lakini ukiiangalia kwa umakini zaka ni 1/10 ya kazi za mikono yako (mwili wako)...hivyo zaka sio pesa tu kwanza pesa ni matokeo ya kazi za mikono sio kazi ya mikono yako.Kama ni mwalimu fundisha kanisani pia hiyo ni zaka,kama ni mshauri shauri kanisani pia hiyo ni zaka...tenga muda wa kazi inayokuingizia kipato kuifanya kanisani ni zaka yako halisi,lakini kulingana na hali ya maisha na hakuna sheria ya ulawi kanisa limeipeleka sana kwenye pesa ili zisaidie kuhudumia kanisa.
Hivyo usifungwe na zama tuko kipindi cha Neema,toa kwa moyo Mungu atakubariki baraka zako zitaendana na sadaka yako.Lakini pia rohoni ukinuia kuifanya kwa mtindo wa sheria 1/10 ya kazi za mikono pia Bwana atakubariki kwani ni agano lako kwake.
Mbarikiwe na Bwana.