Ni namna ipi nzuri ya kutoa fungu la kumi?

Kwahiyo unataka kusema tukate Biblia

Agano la kale liwe peke yake agano jipya oia liwe peke yake?
Tutumie agano jipya peke yake na sio Biblia yote?
Ni swali tu
 

Pitishia mshahara wako kama wewe ni mfanyakazi au malipo yako kama wewe ni mfanyabiashara kwenye akaunti ya Kanisani.
 
Wakristo hawapendi kujifunza Neno, yaan shetan kabana Fikra ktk hili,
Tunapenda kubishana kuliko kukaa na kusikiliza.
Kumbuka huwez jua kila kitu, unachojua wewe mwingine hajui, na anachojua mwingine wewe hujui

Tuwe tunatafuta muda wa utulivu na kusoma Maandiko hii mikanganyiko ya sadaka isingekuwepo

Fungu la 10, ni la walawi waliambiwa watakula madhabahuni.
Huko yatima wajane tafuta sadaka nyingine upeleke na sio fungu la kumi

Na katika fungu la kumi hakikisha hutoi hata sent moja ukaila ukasema nitairudisha
MUNGU anasema leteni zaka kamili ghalani mwangu

Kamili na sio nusu, ukipeleka nusu sawa sawa na zero

Shida tumeweka watumishi wanakula na hii ni kwasababu ya wachache wanao tumia mlango wa dini vibaya
Lakin ukikaa na Mungu vzr utajua hapa ni sahihi ama la?
Sipo kuhukumu watumishi wa Mungu, Mungu ndio atawahukumu kwakuwa nI watu wake
Lakin ukitoa sadaka usiitupe ipeleke na Neno ndani yake iombee hutoona hasara ya kumrudishia Mungu alichokupa

Zaka ni sadaka yenye ahadi
Katk zaka ndipo ambapo Mungu anasema nijaribu uone kama sitofungua madirisha
Ktk baraka kuna baraka nyingi
Katika zaka Mungu analinda hata ulicho nacho kisipukutike kisiharibike
Wala muharibu asiharibu unachopatia pesa

Soma malaki 3
Ukila fungu la 10 ni laana, tena inatoka kwa Mungu

Unaweza ukapigwa kwenye uchumi sana
Utamkemea shetan kumbe hausiki

Ktk fungu la kumi usipo itoa Mungu anakuita mwizi umemuibia
Fungu la 10 sio lako haijalishi ni sh ngapi
Hata kama ni sh 10, usiseme ndogo
Tii peleka kwa Mungu, ni bora uzidishe kuliko kupunguza

Mungu awabariki
 
Unamdanganya mwenzio! Hiyo itakuwa ni sadaka! Fungu la kumi au Zaka hupelekwa kanisani!
Kwani fungu la kumi sio sadaka??

Hayo makanisa yenyewe siku hizi yamekazana kwenye kukusanya pesa tuu kitu ambacho si sawa.

Fungu la kumi ni sadaka pia na unaweza kuitoa popote tu na sio lazima kanisani

Huo ndo mtazamo wangu.

Sent from my GT-I9505 using JamiiForums mobile app
 
Na ukijua hichi kitu hatuendi kwa Mungu na kuanza kumwambia Mungu mimi sikutoa sadaka ya fungu la 10 sababu mchungaji wangu alikuwa anatumia pesa vibaya

Hii ni juu ya Mungu kuhukumu,
Timiza cha kwako kilichopo ktk Biblia,
Huyo mwingine Mungu atashughulika naye

Fanya kwa upande wako usiangalie wa kushoto wala kulia sababu kila mtu ana adhabu yake

Kwa Mungu huwez jitetea kuwa niliambiwa hiv na hivi ndio maana sikutoa

Note hichi kitu kila dini ina mafundisho yake
Kwa upande mwingine upande wa pil wao kupeleka zaka kwingine sio kosa kufuatana na imani yao

Ila Wakristo zaka anakula mchungaji wako
Narudia zaka anakula mchungaji wako, na yeye mkitoa hiyo zaka anatoa pia fungu la 10

Damu ya Yesu iwafungue Fikra zenu

Roho Mtakatifu awafundishe

Mimi nawaambia tu anza sasa kutoa fungu la 10 kwa uaminifu kabisa kama utakosa chakula au kama utapungukiwa na kitu
Shida tunatupaga sadaka hatumwambii Mungu, umeahid hii na hii ktk fungu la 10, na mimi leo Baba nakujaribu, nifungulie madirisha ya mbinguni na baraka zangu zishuke
Mungu umesema wewe sio muongo na mimi najua utafanya hili sema kwa iman Mungu anasikia halafu uone kama hutoona mabadiriko

Note, anza na toba kwasababu unaweza ona umetoa sadaka vzr kumbe Mungu haoni hivyo na shetan akakukandamiza
Achilia damu ya Yesu ktk sadaka yako ikakunenee
Huwezi peleka sadaka kwa Mungu bila sadaka iliyo juu zaidi, ambayo ni damu ya Yesu
Mungu hana njaa na pesa yako sababu vyote ni vyake

Anahitaji moyo wako na imani yako ndio maana anahitaji urudishe kilicho cha kwake

Na kama huko nyuma hukuwa mwaminifu omba toba mwambie Mungu naanza upya

Nakuhakikishia katika Jina La Yesu anayenitunza hadi sasa hivi muda huu utapata majibu

Toa kwa nia ya kukutana na Mungu na ukuu wake ndipo baraka zingine zitakapo kujia

Toa kwa moyo wa furaha na uliochangamka

Sipo kurumbana na imani au na walioshika maandiko na kukremisha vifungu vyote vya Biblia ili tu watwist watu
Nipo kuwaambia kweli ya Mungu

Mungu awabariki

Simami malaki 3:8-12

Mungu hatokuacha, Nafsi moja imeelewa hapa na imevuka
Heaven Sent ukiwa free naomba hiyo malaki niwekee hapa kuna watu kufungua Biblia ni kazi kwao, naomba msaada wa maandiko Binti Sayuni
 
There is no such thing as Fungu la Kumi katika Sisi tunaoishi katika Kristo. Fungu la kumi ni agizo la Torati
 
...Wasaidie watoto yatima,huko kanisani wamejaa wapigaji tu..
 
EXACTLY..... there you are Mkuu
 
"Kupata riziki kwa njia ya Injili" ni lazima iwe kwenye fungu la kumi?
Kwani mchungaji hawezi kupata Hiyo riziki kupitia Changizo /Sadaka za kawaida?

Unaweza kunionesha POPOTE PALE mitume wa Yesu including Paulo walipopokea Zaka?
 
Mmelishwa matangopori makali Sana mpaka mnatia huruma
 
Namna nzuri ni kufungua account na kusave kwaajili ya watoto wako au kununua usafiri...ni fungu la 10 tosha, mengine ni watu wazima wanataka uwalishe familia zao kisa tu wamekariri mistari ya biblia.
 

Zaka na fungu la kumi ni sawa/kitu kimoja?

Kiwango kilipangwa na watu au kimetoka kwenye maandiko?

Naomba kujuzwa
 
Zaka na fungu la kumi ni sawa/kitu kimoja?

Kiwango kilipangwa na watu au kimetoka kwenye maandiko?

Naomba kujuzwa
Zaka ni sawa na fungu la 10, huwekewi kiwango cha kutoa zaka sababu vipato vinatofautiana

Anayepata elf1, na elf 10 kwa siku huwez waambia watoe kiasi kinacho fanana

Mmoja atatoa sh 100, mwingine 1000

Anayepata laki kwa mwez ni tofauti na anayepata milion kwa mwezi

Ukipangiwa kiasi cha kutoa huo ni mchango na utaratibu wa sehemu husika unayo abudu
Ili wafikie malengo waliyo yaweka kutokana na taratibu za mahali husika

Na ukifika ktk mchango usitoe pia kama unatupa semea neno
 
mkuu hiyo unatowaga sadaka siyo fungu la kumi, fungu la kumi ni sehemu ya MUNGU kwenye mapato yako hivyo ni lazima uipeleke kanisani.
 
Namna nzuri ni kufungua account na kusave kwaajili ya watoto wako au kununua usafiri...ni fungu la 10 tosha, mengine ni watu wazima wanataka uwalishe familia zao kisa tu wamekariri mistari ya biblia.
pole Sana mkuu, MUNGU akusaidie.
 
"Kupata riziki kwa njia ya Injili" ni lazima iwe kwenye fungu la kumi?
Kwani mchungaji hawezi kupata Hiyo riziki kupitia Changizo /Sadaka za kawaida?

Unaweza kunionesha POPOTE PALE mitume wa Yesu including Paulo walipopokea Zaka?
changizo sio zaka. kama mkiamua kufanya changizo ni jambo jema zaidi.
Yesu alipozungumzia zaka alipokuwa akiwaonya mafarisayo hakuipinga ila alipinga unafiki ulionyuma ya kufanya mambo kwa kujionyesha huku wakiwa wamesahau mambo makubwa yaani upendo na adili.

Kuhusu Mitume.
haijaandikwa moja kwa moja.
lkn kumbuka maandiko waliyotumia mitume wakati wao yalikuwa ni agano la kale.
ndani ya agano la kale kulikuwa na mambo vivuli yaliyoishia msalabani na mambo ambayo sio vivuli ikiwemo zaka.
ndiyo maana katika malaki Mungu anawakumbusha kuwa kutotoa zaka kamili ghalani ni WIZI na humuibii mtu bali Mungu.
hii ni baada ya kukaa utumwani babeli miaka mingi na kupoteza au kusahau baadhi ya misingi.


Kama ilivyokuwepo ghala katika hekalu, kunapaswa kuwepo ghala katika makanisa, na kutoka katika hilo ghala watumishi wapate chakula. Ghala hujazwa na Zaka na Sadaka.
soma historia ya matoleo tangu ibrahimu utagundua kutoa zaka ni ishara ya utii kwa Mungu. Na mali ulizo nazo sio zako ni za Mungu, na katika hizo unamrudishia.
ndiyo maana hata hiyo wakorintho inazungumzia ideas za agano la kale.
pia kumbuka zaidi ya mafungu 300 ya agano jipya ni quatation za agano la kale. hakuna new testament bila Old testament. lazima ujue kila kilichofanyika agano la kale na kwa nini kiendelee au kisiendelee.
maisha ya mitume hayajaandika kila kitu, hata walivyoendesha mifumo yao ya ibada haijaandikwa hivyo hiyo isiwe kichaka cha kuhalalisha uchoyo na ubinafsi juu ya mali alizokupa Mungu.
Pia kuna baraka tele katika kumtolea Mungu zaka na dhabihu.
 
Nilivyosema kiwango nilimaanisha 1/10.
Je kimewekwa na watu au?

Na muda wa kutoa zaka/fungu la 10 ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…