#COVID19 Ni nani aliwaambia Wanasiasa wanapaswa kuchanjwa kwanza sisi Wanyonge tutafuata baadaye?

#COVID19 Ni nani aliwaambia Wanasiasa wanapaswa kuchanjwa kwanza sisi Wanyonge tutafuata baadaye?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tunapokuwa na Taifa ambalo viongozi na watu wenye uwezo wanapewa kipaombele kwenye kila kitu tunakuza gap la usawa baina ya wananchi. Tumeleta dozi milioni moja kwa ajili ya watawala na wanasiasa wengi wakiwa ni wale waliopo madarakani na wastaafu kwa kisingizio kwamba wapo kwenye risk.

Naomba kuuliza, mfanyabiashara, kondakta wa daladala, wanafunzi wa vyuo nk ukilinganisha na hao waliopewa kipaombele ni yupi yupo kwenye risk? Huu ubaguzi ndio unaopelekea Mwenyenzi Mungu anashughulika na daraja la kwanza kulipunguza ili maskani waishi kwa amani kwenye nchi yao.

Kumbukeni ninyininyi ndio mliwaamisha maskini na wananchi wa kawaida kwamba corona hakuna, wao wakasafival ninyi mkaondoka kwa kasi, mmeona mnaondoka mmekuja na propaganda kwa ninyi mpo kwenye risk unajiuli Mbunge ana risk gani? Mawaziri wanaoweza kuongoza mkutano kwa video conference Wana risk gani?

Mkimaliza kuchanjwa mnakwenda kukusanya wananchi bila hata kuwaambia wachukue taadhari na hakuja anayeoona kuwa wao ni binadamu kama ninyi. Hakuna binadamu wa daraja la kwanza kwenye Dunia hii mbele ya Muumba.
 
... acheni uzushi usio na sababu! Kwa hili la chanjo, kwa kweli serikali imejitahidi sana sana! Kongole! Vituo vyote vya afya vilivyoteuliwa nchi nzima vinatoa chanjo. Labda ni wewe tu huihitaji au unasubiria uletewe nyumbani; hutaletewa.
 
Beatrice,

Let's be serious bhana....

Hivi chanjo hii hii ambayo propaganda zinasambazwa kwamba zina madhara ndo ulitaka waanze kuchomwa wananchi?!

Hivi hapo si ndo yangefuata maswali "...kama kweli haina madhara, mbona wamewatanguliza kwanza wananchi"!!
 
Kipaumbele kilikuwa watu wa hospitali, wenye umri mkubwa na wenye magonjwa hatari.

Lakini Gwajiboy na slowslow wanaendelea kufanya yao.

Hivyo wanasiasa wamekuwa wakichanjwa kwanza kama moja ya kuhamasisha watu wakachanje. Jaribu kuwa positive.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wachanjwe wao kwanza😂 tunahitaji kuwania zile siti pale kwa mzee Kimbunga Jobo
 
Watz ni mbwa yaani unalilia mpaka hiyo chanjo mtumba ya mabeberu
 
Beatrice,

Let's be serious bhana....

Hivi chanjo hii hii ambayo propaganda zinasambazwa kwamba zina madhara ndo ulitaka waanze kuchomwa wananchi?!

Hivi hapo si ndo yangefuata maswali "...kama kweli haina madhara, mbona wamewatanguliza kwanza wananchi"!!
Hata wangeanza kwa wananchi na kuibuka hayo maswali hata wasingejali kuwajibu kama ambavyo sasa kuna maswali na hakuna yaliyojibiwa, mfano hiyo form unayotakiwa kujaza kabla ya kuchanjwa imeletwa sana maswali ila hakuna aliyejisumbua kujibu.
 
Tunapokuwa na Taifa ambalo viongozi na watu wenye uwezo wanapewa kipaombele kwenye kila kitu tunakuza gap la usawa baina ya wananchi. Tumeleta dozi milioni moja kwa ajili ya watawala na wanasiasa wengi wakiwa ni wale waliopo madarakani na wastaafu kwa kisingizio kwamba wapo kwenye risk. Naomba kuuliza, mfanyabiashar...
Hawa hawapo ajili ya wananchi wapo ajili ya familia zao
 
Hata wangeanza kwa wananchi na kuibuka hayo maswali hata wasingejali kuwajibu kama ambavyo sasa kuna maswali na hakuna yaliyojibiwa, mfano hiyo form unayotakiwa kujaza kabla ya kuchanjwa imeletwa sana maswali ila hakuna aliyejisumbua kujibu.
Hawajali wananchi hata kidogo
 
Tunapokuwa na Taifa ambalo viongozi na watu wenye uwezo wanapewa kipaombele kwenye kila kitu tunakuza gap la usawa baina ya wananchi. Tumeleta dozi milioni moja kwa ajili ya watawala na wanasiasa wengi wakiwa ni wale waliopo madarakani na wastaafu kwa kisingizio kwamba wapo kwenye risk. Naomba kuuliza, mfanyabiashara, kondakta wa daladala...

Beatrice Kamugisha good point

Mbaya zaidi kati yao haya majinga, kuna yaliyokuwa yanapinga chanjo kipindi cha Mwendazake, sasa hivi yamegeuka eti yanaunga mkono chanjo. Pumbavu kabisa, watu wangapi wamepoteza maisha kwa kufuata ujinga na upuuzi wao, wala hayajali manyang'au.
 
Labla ni tabia mbaya kwa wanyonge kupata vitu vizuri kabla ya wakubwa
 
... huko maUlaya wazee wanyonge ndo walioanza kupata chanjo ... lakini sisi, baada ya uhamasishaji hasi za kina Gwajiboy, imebidi viongozi ndio watoe mfano na hivyo kutumalizia tuchanjo tudogo tulitokuja!
1628846956708.png
 
Nyie mnasema chanjo ni mpango wa wazungu kutumaliza waaafrika. Hata hivyo kuanzia jana ruhusa kwa kila anayetaka kuchanjwa aende tu kuchanjwa.
 
Back
Top Bottom