Ni nani aliyeharibu Mchakato wa Katiba Mpya? Tuanzie hapo

Ni nani aliyeharibu Mchakato wa Katiba Mpya? Tuanzie hapo

Katiba iliharibiwa na lile bunge maalum la wahuni (bunge la katiba), wakiongozwa na Mhe. Samweli Sitta. Ukada wa vyama kwenye lile bunge ndio ulioharibu mchakato mzima wa katiba, hadi wakaja na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa pro-Chama tawala.
Hawakutaka serikali tatu. Ubishi na ujuaji uliua ile nia ya katiba. mara nyingine tujifunze kuwa humble. Kuna yaliyokuwa yanawezekana kwenye ile katiba kwa wakati ule. Yale yangefanyika. Yasiyowezekana yangeachwa pembeni ili wakati muafaka ukifika, nayo yapatiwe maamuzi.
Ujuaji na ego za watu ndio zimeharibu
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa? Amepata hukumu gani?

Mwacheni Mama nyie mjifikirie kwa nini mliharibu mchakato wa Katiba na pesa hamkurudisha. Majizi makubwa nyie. Sasa mnakosa pesa mnataka mje zipata tena kwenye Katiba.
Ukiacha uharo mwingine ulioacha hapa, mchakato uliharibiwa na ccm & co akiwemo Samia, Mwendazake, kiwete na mahafidhina mengine miccm. Mwendazake akautumbukiza kaburini. Samia badala ya kuu-rescue, naona ana dalili za kuweka udongo.
 
Waliharibu wapinzani UKAWA kwa vile walitaka serikali 3 badala ya 2 na hivyo kususa kikao kama njia ya kushinikiza. Hapo ndipo walipofanya kosa la kiufundi kubwa. Laiti wangekubali kwenda by peace meal wakaanza na madaraka ya Rais, Tume ya uchaguzi, upatikanaji wa wabunge, mgombea binafsi, nk wakaruka maeneo magumu halafu 5 years later wakayarudia kwa agenda mpya. Pushing by bits. Wangefanikiwa sasa hivi tungekuwa mbali sana. Hii ndiyo mbinu ya majadiliano magumu. You dont push for everything rather moving strategically in win win situation.
Waonaje kama utakuwa mkweli ndugu.
Swala serikali tatu lilianzia kwa wananchi likaja mpaka kwenye Rasimu. Waulize wote hata akina Propesa Kabundi, Chakubanga Polepole etc. Nguvu kubwa ilitumika kuikandamiza rasimu hiyo hata kabla kuingia bunge la Katiba, kwa kuwatumia akina Makonda na vikundi vingine, pamoja na kuwa zoezi hilo kukusanya maoni lilikuwa limetumia rasilimali nyingi.
 
We ulijuaje nchi haitaji katiba? Unanuuliza % ngapi hivi kitu kikiwa kibovu kikamilishwa kwa 199% kitakuwa na mantiki kwel we msukule?
umeulizwa swali jibu swali?....toka lini swali likajibiwa na swali? halafu mtu kama wewe ndio umeshupaza shingo unadai katiba mpya....bila shaka hata hiyo katiba ya zamani huifahamu..
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa? Amepata hukumu gani?

Mwacheni Mama nyie mjifikirie kwa nini mliharibu mchakato wa Katiba na pesa hamkurudisha. Majizi makubwa nyie. Sasa mnakosa pesa mnataka mje zipata tena kwenye Katiba.
ccm kwa ujumla wao
 
UKAWA unawasingizia. Wao waliunda UKAWA baada ya kuona yale maoni ya wananchi kwenye rasimu ya pili ya tume yametupwa yote, instead CCM wamekuja na kitu kipya kabisa ambacho kilikuwa hakibebi maoni ya wananchi. Rejea upya chanzo cha ukawa
Hayakutupwa,,vifungu vilipigiwa kura,kuna vilivyopita,vingine havikupita,,,kwanini ukawa walisusa?
 
Waliharibu wapinzani UKAWA kwa vile walitaka serikali 3 badala ya 2 na hivyo kususa kikao kama njia ya kushinikiza. Hapo ndipo walipofanya kosa la kiufundi kubwa. Laiti wangekubali kwenda by peace meal wakaanza na madaraka ya Rais, Tume ya uchaguzi, upatikanaji wa wabunge, mgombea binafsi, nk wakaruka maeneo magumu halafu 5 years later wakayarudia kwa agenda mpya. Pushing by bits. Wangefanikiwa sasa hivi tungekuwa mbali sana. Hii ndiyo mbinu ya majadiliano magumu. You dont push for everything rather moving strategically in win win situation.
katiba siyo suala la kila baada ya miaka mi5 mi5
 
Hawakutaka serikali tatu. Ubishi na ujuaji uliua ile nia ya katiba. mara nyingine tujifunze kuwa humble. Kuna yaliyokuwa yanawezekana kwenye ile katiba kwa wakati ule. Yale yangefanyika. Yasiyowezekana yangeachwa pembeni ili wakati muafaka ukifika, nayo yapatiwe maamuzi.
Ujuaji na ego za watu ndio zimeharibu
Siyo ubishi,katiba hupigiwa kura,,in this case,ilipigiwa kura kifungu kwa kifungu,,hakuna ubishi hapo,ukawa hawakuwa na majority.
 
umeulizwa swali jibu swali?....toka lini swali likajibiwa na swali? halafu mtu kama wewe ndio umeshupaza shingo unadai katiba mpya....bila shaka hata hiyo katiba ya zamani huifahamu..
Nakuuliza maswali ya kilogic basi Sawa mie katiba ya zamani siifahamu na watz wengine wengi hawaijui, tufanye wanaijua wanaccm wenye madaraka na lissu pekee. Haya swali la kilogic kuna ubaya gani kuipatia nchi katiba bora hata kama raia 99% haiwafahamu ile mbovu ya zamani? Au swali jingine la kilogic wewe kama mzazi kipi ni bora kuipelekea familia yako samaki au Joka hata kama familia ilikuwa haijaomba samaki?
 
Waliharibu wapinzani UKAWA kwa vile walitaka serikali 3 badala ya 2 na hivyo kususa kikao kama njia ya kushinikiza. Hapo ndipo walipofanya kosa la kiufundi kubwa. Laiti wangekubali kwenda by peace meal wakaanza na madaraka ya Rais, Tume ya uchaguzi, upatikanaji wa wabunge, mgombea binafsi, nk wakaruka maeneo magumu halafu 5 years later wakayarudia kwa agenda mpya. Pushing by bits. Wangefanikiwa sasa hivi tungekuwa mbali sana. Hii ndiyo mbinu ya majadiliano magumu. You dont push for everything rather moving strategically in win win situation.
Kwanza hujui historia ya ukawa. Halafu unaposema 'wangefanikiwa' badala ya 'tungefanikiwa' inaonyesha wewe kwa akili yako unaona katiba mpya nzuri haikuhusu. Na hizi ndio akili za wantanzani baadhi wanaolambishwa pipi na ccm wanasahau maslahi mapana ya taifa hili kwa muda mrefu ujao. Vinginevyo ni uzezeta ndio utawezs kumfanya mtu afikiri kuwa ukawa walikwamisha mchakato wa katiba, wakati wao ukawa walikuwa wanapinga kuchakachuliwa kwa maoni ya wananchi. Well, tufanye (let's assume) uukawa walikwamisha: Je unafikiri hatuhitaji katiba mpya sasa au tuuzime kabisa mchakato ili kuwaadhibu ukawa? Does ukawa exist now?
 
Siyo UKAWA.
Je TOR za Rasimu ya Chenge zilitokea wapi? Tume ya Katiba inayotambulika kisheria ilikuwa chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba. Usiwalaumu UKAWA kwa kususia Bunge ambalo liko CCM dominated kwa ajili ya kukidhi masilahi binafsi.

Kwa faida yako nitakuambia leo kwa nini Rasimu ya Katiba ya Warioba ilitupwa. Kulikuwa na kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa yao watakayokuwa wamefanya wakiwa madarakani. Sasa Jakaya aliruhusu na alipokea fedha za Escrow kutoka kwa Harbinder Singh/ Rugemalira.

Wakati huo huo Andrew Chenge naye akiwa ni mnufaika wa Escrow kutoka kwa Rugemalira. Ndipo akamtonya Jakaya kuwa kama Rasimu ya Warioba itapita basi hicho kifungu cha Marais kuwajibika kwa makosa waliyofanya, basi ajiandaye kushtakiwa na kufungwa.

Jiulize kwa nini Dr Mvungi aliuliwa utapata majibu ya kwa nini mchakato ulikwama.

Ndipo Jakaya Kikwete akaelewa na kuamua kuuvuruga mchakato wa Katiba kwa kuogopa kuja kushtakiwa.
 
Siyo ubishi,katiba hupigiwa kura,,in this case,ilipigiwa kura kifungu kwa kifungu,,hakuna ubishi hapo,ukawa hawakuwa na majority.
Ile ya Warioba ilipigiwa kura wapi? Ndio maana nimesema ujuaji unakwamisha kila kitu. We fail to operate strategically. Hii ni Africa naona kama tunajisahau. Mambo yanaenda taratibu sana
 
Ile ya Warioba ilipigiwa kura wapi? Ndio maana nimesema ujuaji unakwamisha kila kitu. We fail to operate strategically. Hii ni Africa naona kama tunajisahau. Mambo yanaenda taratibu sana
Kumbe haukuangalia bunge la katiba..?ilipigiwa kura na wajumbe na ilifail kupita ndo kukawepo rasimu ya katiba ya chenge,,
Ulikua bado hujazaliwa labda...
 
Nchi hii mwenye kupewa lawama ni founder wa msingi wa taifa maana aliona shida kubwa Sana mbele ila mapenzi ya chama chake dhidi ya taifa akakaa kimya uku akijua kaacha kitu Cha hovyo kabisa.
Kwa hili Nyerere anastahili lawama atake asitake.
 
Mchakato wa katiba uliharibiwa na wanasiasa wajinga waliotaka kupenyeza agenda zao ili waingie ikulu kirahisi matokeo yake yakaibuka malumbano na mwisho wa siku wenye mamlaka wakaamua wauzike tu...

Hata hawa wapiga kelele za katiba mpya ukiwauliza agenda zao utaona ni zilezile za maslahi ya kisiasa ili wapate urahisi wa kuingia madarakani lakini ukiwauliza hoja za msingi zenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi hawana...

Ukiwauliza ni lini mmeitisha maandamo ya watu kupewa elimu bure na bora, huduma za afya bure, fao la kujitoa, kuboreshwa kwa pension za wazee wetu nk nk...
Umemaliza mkuu!
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa? Amepata hukumu gani?

Mwacheni Mama nyie mjifikirie kwa nini mliharibu mchakato wa Katiba na pesa hamkurudisha. Majizi makubwa nyie. Sasa mnakosa pesa mnataka mje zipata tena kwenye Katiba.
Hapa kupata Katiba labda ya TFF!
 
Mnakuja msumbua mama bure. Mchakato wa Katiba ilikuaje ukasitishwa? Ni nani alifanya uharibifu ule wa pesa? Amepata hukumu gani?

Mwacheni Mama nyie mjifikirie kwa nini mliharibu mchakato wa Katiba na pesa hamkurudisha. Majizi makubwa nyie. Sasa mnakosa pesa mnataka mje zipata tena kwenye Katiba.

Tatizo katiba mpya ya nchi gani.???

Zanzibar ipo lakini Tanganyika haijulikani imeenda wapi ?? Sasa katiba ya serikali 3, Huyo atayezungumzia serikali ya Tanganyika ni nani ??

na serikali ya muungano haipo kwani ni Batili. Haikuridhiwa na Zanzibar tokea day one. MUUNGANO WOTE NI MATANGO PORI YA LAANATULLAHI NYERERE.

Iliyobaki Tunasubiri kurudishwa kwa kiti cha Zanzibar UN ambacho kipo lakini ulifanywa umafia na Waingereza kwa kushirikiana na Marekani , kukiwekea turubali. Mwelekeo wa kuvuliwa turubali ni mzuri.

Ni muda mchache tu mambo yatajipa.

Hapo ndipo mtakapojitafakari kurudisha Tanganyika na kuongea na Zanzibar kama wananchi wa nchi hizi watakubali kufanya muungano huo utakaoandika Katiba mpya
 
Back
Top Bottom