Kama hayo yaliyo andikwa hapo juu ni kweli, basi Slaa naye hutufai kabisaa.. Kama ametoa takwimu kwa misingi ya dini basi atakua ni chui aliyejificha ndani ya ngozi ya kodoo. Atakua amethibitisha yale madai ya baadhi ya wana CCM kuwa ni mdini na ametumia makanisa katika kampeni zake.
Awe Kikwete au Slaa au mtu mwingine yeyote, atayejaribu kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini (HATUFAI)
Hapa JF wako watu wengi wanaofagilia mambo ya Udini na kushabikia viongozi wadini wanapoingilia mambo ya siasa...Hayo sio mambo ya mzaa kwani mwisho wake ni mbaya kupindukia
Eeh mwenyezi mungu tuepushe na viongozi wanaotaka kutuvuruga kwa misingi ya dini, kabila na rangi.