:thinking:
Ujumbe wake Rais mwenye ushindi wa utata, Jakaya Kikwete, kuulani UDINI ndani ya bunge Dodoma hapo jana (Oktoba 18, 2010) uliwaacha watu kibao vinywa wazi kwa dakika kadha huku wakikosa la kusema juu ya wito huu.
Wanaichi wengi ambao wanaamini ya kwamba Ndg Kikwete ndiye mpali miche ya udini nchini kwa sababu ambazo bado hazijabainika vema kwa taifa hili ambalo halikuwahi kufahamu ubaguzi wa aina yoyote hapo nyuma wamedai JK anapoona hutumia mawani ya UDINI, anapoota huota kwa mrengo wa kidini, hupokea ushauri wale anaowaamini kidini tu, na hata anapoteua watu kazi hutumia vipaumbele unaosimama kwenye jiwe la udini.
Mfano raisi zaidi wa madai hayo mazito hapo juu ulidhihirika (Oktober 17, 2010) siku moja tu kabla ya ugeni wake bungeni ambapo kwenye uteuzi wake wa muhimu na kwa awali kabisa wa wabunge maalum nayo pia ikafwaya mkondo huo huo kwa jicho jicho lake kuangaza watu wa dini moja tu kwa mpigo. Walioteuliwa ni pamoja na Ndg Shamsi Vuai Nahodha, Zakia Hamdani Meghji na Prof Makame Mnyaa Mbarawa. Hata hivyo hili halikusumbua wengi sana kwani wamekwishajizoelea kwamba wakuu wa wilaya , mikoa na mashirika mbalimbali ya umma nao lazima wapatikane kwa njia hiyohiyo kama ada.
Kama hiyo haitoshi, mashirika ya madhehebu ya kidini ambayo nazo zilikwemo katika mali binafsi zilizotwaliwa na serikali mwaka wa 1967 baada ya azimio la arusha kuzaliwa. Hivi majuzi baada ya serikali kurejea mfumo wa soko huria, baadhi ya mali binafsi zimepata kurejeshwa mikononi mwao wahusika japo kwa uchache sasa. Madhehebu mbalimbali sana walipokonywa mali zao zikiwemo shule, hospitali, mijengo ya miofisi na hata makazi. Hapa nako gogoro likaelekezwa kivile vile tu!!
Jambo jingine linalotoa wasiwasi mkubwa kwake JK ama ni unafiki na kejeli tu kuhusu swala hili la udini chini mwetu kwa nako pia, pamoja na unyeti wote na ubichi wa kidonda cha kuporwa uchaguzi kwa misingi hiyo hiyo kama ilivyowahi kubashiriwa na mwandishi mmoja mwandamizi Alhaj Y takriban wiki 6 zilizopita, uchaguzi nao ukaporwa kwa misingi hiyo na kuwatisha wananchi kwa kutumia baadha ya kofia za aina hiyo hiyo jeshini na polisi hata wasipige kura.
Kwa upande mwingine wakilainisha chama fulani Machachari sana nacho kikatulia kama barua ndani ya bahasha kwa kuzingatia mwito huo huo wa udini. Leo nako au kesho, nako ndani ya sheria zetu Mahakama ya Kadhi na kujiunga OIC zote zinakuja tupende tusipende nalo kwa mfumo huo huo.
Sasa, tunasema yetu macho .... japokua swali hapa jamvini ni kwamba je JKkweli kaokoka na kilema chake hichi sote tujue tangu alivyozungumza??????????