Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
waliotoka bunge siyo tu wabunge bali wote tuliwachagua wabunge pamoja na rais wetu wa chadema.Tupo pamoja na wabunge hilo.wamebaki wakijichekesha wabunge wakiozomea rais aliyeanza kuongea,
 
CCM Ndio iliyoanzisha Udini kwenye Utawala wake kwa kupeana Madaraka kwa wakati
CCM Ndio iliyoanza kusema Udini kwenye Uchaguzi wa Mwaka huu

Kwanini wasitupe Mifano?

Chadema kimeshinda Mijini Maeneo ambayo watu wote wanajua kama kuna udini au ni hali halisi ya maisha yao na sio vijijini na maeneo ya vijijini
 
ASANTE SANA mwanakijiji ila inasemekana siku zako zinahesabika , jiangalia brother

Hii biashara ya kutishiana imetoka wapi tena? Wewe umujiunga na hii forum juzi wakati wa kampeni leo unatishia watu? Hebu tueleze zaidi siku zake zinahesabika vipi? Huoni hata aibu?

Tiba
 
Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah.. ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake. Eeenh... moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.

Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge. Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.

Baada ya kususia hafla ya leo asubuhi , hatua ya pili ilikuwa kususia hotuba ya rais, na jambo hilo lilifanyika, na hatua ya tatu ni kususia hafla ambayo inatokea leo usiku, ambayo tulikubaliana pia wabunge wetu wasihudhurie. Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum inje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.

Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza, tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi, tumedai serikali iache kutumia vyombo vya dola hasa polisi na FFU katika uchaguzi serikali haitusikilizi. Kwa hiyo namna pekee ya kudai haki, ukiona mazungumzo ya kistaarabu hayafanyiki basi unapiga kelele. Na hii ni namna mojawapo ya kupiga kelele.Tukumbuke kwamba CHADEMA tumesema hatuhitaji vurugu, hatuhitaji kuwaambia wananchi waende mitaani kwa maandamano - hata kama ni ya amani kwa hatua ya awali - tukitegemea kwamba serikali itatusikiliza, tukae pamoja au ituahidi kwamba itafanya haya marekebisho kabla ya uchaguzi wa 2015. Bila ya kuchukua hatua kama hizi, 2015 tutarejea kwenye mchezo huo huo mchafu, kura zitaendelea kuchakachuliwa, vyombo vya dola vitaendelea kutumika, watanzania wataendelea kunyanyasika, na ukombozi ambao tumewaahidi watanzania hautaweza kupatikana.

Kwa hiyo kimsingi yaliyotokea ni tafsiri ya press conference ambayo tulifanya siku chache zilizopita pale Dodoma, inawezekana Watanzania wengi hawakuelewa ile press conference. Sasa hii ni tafsiri ya ile press conference, na tunawaomba Watanzania watuelewe kwamba tuliposema tutatumia ukumbi wa bunge, na tutatumia eenh.. fora nyingine nje ya bunge, hii ndiyo maana yake. Inje ya bunge tumesusia hafla mbalimbali, ikiwemo hii ya waziri mkuu kuapishwa, kikiwemo ya chakula cha rais, lakini nahafla zingine zitakazoendelea ambapo rais ataendelea kuwa ndiye mwenye hafla hiyo. Eenh, lakini vilevile tumesema kwamba tutakwenda kwa wananchi kuwaeleza sasa ni nini kimetokea.

Kwa hiyo watu wasishangae kwamba tunafanya mikutano yenye sura ya kufafanua zaidi hatua zetu maana yake ni nini, nadhani hii ni kitu ambacho kila mtanzania anaielewa, na kwa simu tulizopokea mpaka sasa hivi, sms ambazo nimekuwa nikizipokea mpaka sasa hivi, watanzania wengi sana wametusifu , wamepongeza wabunge wetu. Ninaomba Watanzania wote wenye nia njema watuunge mkono katika kilio hiki, lakini tukizingatia kwamba yote tunayofanya yawe kwa msingi ya amani, tusitoke mitaani kama tulivyokwishakuwaomba. Watanzania kama wa Shinyanga ambao wamechakachuliwa kura za mbunge wao waziwazi, Watanzania kama wa Mbozi ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, Watanzania kama Segerea ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, tunaendelea kusisitiza kwamba, mazungumzo daima ni njia bora ya kuondoa migogoro. Kwa hiyo tusingependa katika hatua hii eeenh yale yaliyotokea yaendelee kutokea.

Ninawaomba amani, ninawaomba utulivu lakini tuendelee kudai haki zetu kwa njia ambazo zinaweza kuzaa matunda.
 
I have some major issues with Slaa's/ CHADEMA's outlook.
 
Haya ndio mambo ndugu zangu!!! Mwanakijiji, kalitupe hilo jembe mbali sana tu maana umeshakua zaidi ya Mwana-Kinyanambo C kule tunakolimaga vingamba!! Tangu leo wewe Mwanamji kwa kututumia hutuba wa Raisi wa Umma wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Daktari (PhD Darasani ktk Sheria, na Malezi Mema Vijana Tanzania) kwa tchnolojia hii ya hali ya juu. Sema Mwanamji tangu leo.

Mwanakijiji, kwa hakika ujumbe umefika bila kupinda. Nina uhakika watanzania wengi baada ya mwaka mmoja hivi, wataelewa vyema nia y CDM ni nini. Kuna uwezekano wa kuiweka hiyo speech ktk magazeti watu waisome?
 
SHukrani Mwanakijiji kwa kutueleza yaliyojiri. Hivi wakuu hakuna njia ya kurusha hii clip kwenye Radio zetu ili wale wasio na Mitandao wasikie? Ni muhimu sana kama uwezekano upo ifanyike hii itasaidia sana kuwaelimisha watanzania.----Msisahau ku-include hako kawimbo, ni kazuri na kanafaa sana.
 
Excellent Mkuu, we are one, stronger & firm hadi ukombozi uje we are CHADEMA NYAMA,DAMU hadi mifupa, tumechoka na madudu ya ccm
 
Huyu ni rais mshamba sana, amesahau kuwa marafiki zake na yeye ndiyo wanaoeneza udini?

Rashidi shamte alifanya nini kwenye sms alizokuwa anatuma?

Mzee membe alisemaje kuhusu mahakama ya kadhi na jumuiya ya oic

batilda likuwa naongea nini misikitini alipokuwa akiomba kura ya ubunge arusha?

Wale waliosambaza waraka wa makafiri misikitini na nakala ikapatikana jf ni akina nani????

Amechemsha sana huyu mzee na kwa jinsi inavyoonekana baraza lake ni mambo ya kike kama kawa!!!!!

Chadema get set when we say go we mean it................ I say we mean!!!!
 
Asante sana Mwanakajiji. Yaani huo wimbo umeokonga roho yangu hadi niksahau hotuba ya slaa. Bravo!!!
 
Inaonekana wazi kabisa jamaa wa CHADEMA hawakurupuki na hiyo hafla ya leo usiku haikwenda sawa maana presha imekuwa kubwa sana kwa mwizi.
 
Ndugu zangu Watanzania, pamoja na ndugu zangu wote waliokuwa wanafuatilia matukio ya bungeni leo. Aaah... ni kweli nimepata watu wengi wakiulizia, aah ni kwanini wabunge wa CHADEMA walitoka ndani ya ukumbi wa bunge, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano alipoanza kutoa hotuba yake. Eeenh moja ni kwamba CHADEMA ni chama chenye msingi, kinachofuatilia, eenh na kuhakikisha kwamba daima kiko consinstent yaani kinatekeleza kile ambacho kinasimamia, aah kwa kuwa tulikwisha kukataa kutambua matokeo ya uchaguzi, na vilevile baada ya kukataa kutambua matokeo tulikataa vilevile kumtambua rais aliyepatikana kwa mchaka.. eenh kutokana na mchakato huo ambao hatuutambui, basi ni dhahiri kabisa aah matendo yetu yaendane na kile tunachoamini.

Dr., Since umeanza kwa kuongelea consinstency, swali langu mimi ni, kama hamumtambui Kikwete mlipopiga kura pendekezo lake bungeni kwa kiti cha Waziri Mkuu, mlikuwa mnapigia kura pendekezo la nani? Je pale mlimtambua halafu mkashauriana na sasa hamumtambui? Kuna consistency gani hapo ?

Wabunge wetu wapo kwenye forum ambayo inasimamia kile ambacho CHADEMA inakiamini. Bunge ni mahali ambapo wabunge wana nafasi ya kubeba bendera ya CHADEMA, na mahali pa kwanza pa kuonyesha kwamba hatumtambui rais ni dhahiri basi ni kwamba ni ndani ya bunge. Kitendo cha leo kilianzia asubuhi, kwa wabunge wetu kutohudhuria hafla ya kumuapisha Waziri Mkuu, kwa sababu isingekuwa na maana kwenda kuhudhuria hafla ambayo inasimamiwa na rais ambaye kimsingi hatumtambui, lakini vilevile ni ishara kwa watanzania kwamba bado eenh tunataka maelezo ya kina kutoka serikali kuhusu kauli tulizokwishakuzitoa.

Utasemaje unaonyesha kutomtambua rais kwa kutohudhuria hafla ya kuapishwa Waziri Mkuu wakati umehudhuria, kushuhudia na kushiriki upigaji kura zilizompitisha huyo waziri mkuu aliyependekezwa na rais ? Kipi muhimu, kura za kumpitisha au tafrija ya kumpongeza baada ya kupitishwa ? Hivi kweli mnataka tuwachukulie seriously kwa mwendo huu ?

Baada ya kususia hafla ya leo asubuhi , hatua ya pili ilikuwa kususia hotuba ya rais, na jambo hilo lilifanyika, na hatua ya tatu ni kususia hafla ambayo inatokea leo usiku, ambayo tulikubaliana pia wabunge wetu wasihudhurie. Hizi ni ishara muhimu katika siasa, kupelekea kuipeleka kwa serikali kwamba kuna malalamiko ya msingi ambayo tunayo kuhusu mchakato wa uchaguzi, na ni dhahiri kwamba kama serikali ni makini, kama serikali ni sikivu basi itasikiliza kauli hiyo ya wenzetu ambao huko bungeni. Lakini kauli hizo hazitaishia pale, kama tulivyokwishakutoa katika press conference yetu, tulisema tutatumia forum ndani ya bunge, na forum inje ya bunge kupiga kelele mpaka serikali itusikilize.

Muda wa ishara umekwisha, tunataka matendo yenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisheria.

Ni nini tunachokihitaji ? Tunahitaji, aah, demokrasia ya kweli katika nchi yetu, tunahitaji uchaguzi ambao utaendeshwa kwa misingi ya misingi ya demokrasia ya kweli. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Eenh.. tunahitaji sheria mbovu ziweze kurekebishwa, ili chaguzi zisiendelee kuchakachuliwa kama ilivyotokea safari hii. Kwa hiyo haya ni mambo ya msingi ambayo hakuna mtu yeyote atatuambia tusiyadai, kwa sababu tumelalamika mara nyingi juu ya kat.. ya marekebisho ya katiba, serikali imekuwa si sikivu haitaki kusikiliza, tumedai kuhusu tume huru, serikali imekataa kutusikiliza, tumedai marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo ni kandamizi serikali haitusikilizi, tumedai serikali iache kutumia vyombo vya dola hasa polisi na FFU katika uchaguzi serikali haitusikilizi. Kwa hiyo namna pekee ya kudai haki, ukiona mazungumzo ya kistaarabu hayafanyiki basi unapiga kelele. Na hii ni namna mojawapo ya kupiga kelele.Tukumbuke kwamba CHADEMA tumesema hatuhitaji vurugu, hatuhitaji kuwaambia wananchi waende mitaani kwa maandamano - hata kama ni ya amani kwa hatua ya awali - tukitegemea kwamba serikali itatusikiliza, tukae pamoja au ituahidi kwamba itafanya haya marekebisho kabla ya uchaguzi wa 2015. Bila ya kuchukua hatua kama hizi, 2015 tutarejea kwenye mchezo huo huo mchafu, kura zitaendelea kuchakachuliwa, vyombo vya dola vitaendelea kutumika, watanzania wataendelea kunyanyasika, na ukombozi ambao tumewaahidi watanzania hautaweza kupatikana.

OK, kwanza unasema serikali haiwasikilizi, halafu unaendelea kusema unategemea serikali itawasikiliza, au hata inaweza kuwaahidi marekebisho. Wanasema kufanya kitu vile vile na kutegemea matokeo tofauti ni kichaa, sasa CHADEMA mnafanya nini tofauti na nyuma ? Au "mnapiga makelele" tu kama unavyosema mwenyewe mkitumaini CCM wataona haya na kuwapa mabadiliko katika kisahani cha dhahabu? Kama hawana haya na hawawapi mabadiliko je, mtafanya nini ?

Kwa hiyo kimsingi yaliyotokea ni tafsiri ya press conference ambayo tulifanya siku chache zilizopita pale Dodoma, inawezekana Watanzania wengi hawakuelewa ile press conference. Sasa hii ni tafsiri ya ile press conference, na tunawaomba Watanzania watuelewe kwamba tuliposema tutatumia ukumbi wa bunge, na tutatumia eenh.. fora nyingine nje ya bunge, hii ndiyo maana yake. Inje ya bunge tumesusia hafla mbalimbali, ikiwemo hii ya waziri mkuu kuapishwa, kikiwemo ya chakula cha rais, lakini nahafla zingine zitakazoendelea ambapo rais ataendelea kuwa ndiye mwenye hafla hiyo. Eenh, lakini vilevile tumesema kwamba tutakwenda kwa wananchi kuwaeleza sasa ni nini kimetokea.

Again, huwezi kushiriki kumpitisha Waziri Mkuu, halafu ukasusia hafla, halafu uniambie uko serious. This is a big joke.

Kwa hiyo watu wasishangae kwamba tunafanya mikutano yenye sura ya kufafanua zaidi hatua zetu maana yake ni nini, nadhani hii ni kitu ambacho kila mtanzania anaielewa, na kwa simu tulizopokea mpaka sasa hivi, sms ambazo nimekuwa nikizipokea mpaka sasa hivi, watanzania wengi sana wametusifu , wamepongeza wabunge wetu. Ninaomba Watanzania wote wenye nia njema watuunge mkono katika kilio hiki, lakini tukizingatia kwamba yote tunayofanya yawe kwa msingi ya amani, tusitoke mitaani kama tulivyokwishakuwaomba. Watanzania kama wa Shinyanga ambao wamechakachuliwa kura za mbunge wao waziwazi, Watanzania kama wa Mbozi ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, Watanzania kama Segerea ambao wamechakachuliwa kura zao waziwazi, tunaendelea kusisitiza kwamba, mazungumzo daima ni njia bora ya kuondoa migogoro. Kwa hiyo tusingependa katika hatua hii eeenh yale yaliyotokea yaendelee kutokea.

Mimi ningekusifu na kukupongeza zaidi kama ungesusia kila kitu cha rais huyu, pamoja na kupigia kura uhakiki wa chaguo lake la waziri mkuu.

Ninawaomba amani, ninawaomba utulivu lakini tuendelee kudai haki zetu kwa njia ambazo zinaweza kuzaa matunda.

Njia unayotumia wewe haizai matunda, actually ni the worst of both worlds. Wataka mabadiliko wa kweli kama mimi tunakuona haufanyi vya kutosha, wapenda ushirikiano wa vyama vya kisiasa watakuona unawagawa Watanzania kwa misingi ya vyama. Utawapata wafuasi wako hao hao wanaoamini CHADEMA kama dini.

Kama kweli unataka kutomtambua rais huyu itisha migomo na maandamano nchi nzima.

La, mkubali uende kutaka mabadiliko bungeni. Zaidi ya hapo unazua maswali mengi kuliko majibu.
 
ahsante sana mkuu, halafu hawa wadhalimu wanataka kuzusha eti wapiganaji wa CHADEMA wanachochea udini. Mesenja wa mafisadi Pinda keshaanza kutumwa, anapyuka eti chama kinataka kuvuruga amani badala wajiulize kwanini watu hawajajitokeza kupiga kura.
 
I have some major issues with Slaa's/ CHADEMA's outlook.
<br />
<br />
si uzimwage issues ulizonazo? Wakati mwingine ni vizuri kuwapa watu ushauri mapema badala ya kusubiri watu wachukue hatua halafu ndiyo tuonekane mafundi sana wa kukosoa na kujifanya wataalamu wa ku-analyse issues. Haya leta hizo major issues!
 
Mimi namchukia rais anayeongelea issues bila kutoa ushahidi. Kikwete angejaribu ku-support allegation yake ya udini kwa kutoa mfano mmoja tu. Hafanyi hivyo kwa sababu anajua mfano wowote ulio wazi atakaoutoa utatoka upande ule aliofaidika nao.

Sasa asitake kuhamisha kusudi la mpasuko wa taifa hili kwa hoja nyepesi nyepesi za kidini. Tatizo kuu la taifa hili ni genge la wachache (mafisadi) wa ccm waliozipukutua rasilimali za nchi na kuiacha mfupa mtupu.

Sasa kama Jk atataka tuwaze kidini kama anavyotaka kutuaminisha tunaweza kumuuliza swali dogo tu la kijinga, ni kwa nini top five wa nchi hii ni wa dini moja? Je kwa upande wa pili yake ilishawahi kutokea hata mara moja toka uhuru top five hao wa taifa wakawa wa dini ya upande huo tu?

Jamani tunamshauri Jk kwa nia njema tu kwamba tujaribu kujinasua kuwaza kidini, maana itatufikisha mahala pa madai ya kwamba rais akiwa mwislamu basi makamu awe mkristo na rais wa zanziba atoke kwenye dini ya budha makamu wake atoke kwenye dini za asili. Kama rais alikuwa ni suni, basi waziri mkuu awe ni kadiani na kama makamu ni mkatoliki basi jaji mkuu awe ni mluteri, na kama rais wa zanziba ni budha basi mkuu wa majeshi atoke aljamaat na kushuka chini kushirikisha dini zote na madhehebu yote na hata mpaka kuhamia kwenye makabila. Hatutakaa tufike kwa njia hii.

Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba mchomekeaji udini na ukabila katika siasa ni CCM, tuna ushahidi jinsi walivyokisingizia chama cha cuf kuwa ni cha kiisilama na kisha kuhamishia uchafu huo kwa CHADEMA kwamba ni cha kikristo na cha wachaga. Hivyo JK anapozungumzia udini asisite kukikemea chama chake kwamba kikiendekeza tabia yake kitasababisha maangamizi ya taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Utasemaje unaonyesha kutomtambua Waziri Mkuu kwa kutohudhuria kuapishwa kwake wakati umehudhuria, kushuhudia na kushiriki upigaji kura zilizompitisha ? Kipi muhimu, kura za kumpitisha au tafrija ya kumpongeza baada ya kupitishwa ? Hivi kweli mnataka tuwachukulie seriously kwa mwendo huu ?
Mkuu wangu vipi lakini...Labda mimi sikuelewi unacho maanisha. Kuna watu waliopiga kura za urais kutomchagua Dr.Slaa na leo hawamtambui Dr.Slaa kama rais sasa unataka kusema kwamba hawa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa hawakutakiwa kupiga kura toka mwanzo au?
 
<br />
<br />
si uzimwage issues ulizonazo? Wakati mwingine ni vizuri kuwapa watu ushauri mapema badala ya kusubiri watu wachukue hatua halafu ndiyo tuonekane mafundi sana wa kukosoa na kujifanya wataalamu wa ku-analyse issues. Haya leta hizo major issues!

Nizimwage mara ngpi tena? Wakati mwingine ni vizuri kusoma kikamilifu kabla ya kuandika.
 
Mkuu wangu vipi lakini...Labda mimi sikuelewi unacho maanisha. Kuna watu waliopiga kura za urais kutomchagua Dr.Slaa na leo hawamtambui Dr.Slaa kama rais sasa unataka kusema kwamba hawa watu ambao hawamtambui Dr. Slaa hawakutakiwa kupiga kura toka mwanzo au?
Mkandara hii issue ya CHADEMA ni tata saana. Si hivyo tu bado wanaonekana wanaimani na serikali ya Kikwete maana wanasema watapeleka matatizo yao. Hivi kama humtambui baba yako, unawezaje kudai matunzo?
Halafu hawa CHADEMA wanapatikana bungeni na huko watakuwa wanahoji utendaji wa serikali. Serikali ipi wakati hawaitambui? Strategy yao bado inapwaya saana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom