Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Simpendi mtu mnafiki maana hana dini hata kama atajiona ni mfuasi wa dini. Kwa bahati mbaya udini katika Tanzania unaletwa na wanasiasa pale wanapoona wanapoteza mvuto. Kama litatokea la kutokea, wao watabebeshwa mzigo mkubwa sana. JK na wasaidizi wake lazima wajue hivyo. Hi hatari sana kutafuta madaraka kwa mgongo wa dini
 
UFA upo kabisa na asitafute mchawi ni yeye mwenyewe. Kama anajua hilo la ufa wa KIDINI uteuzi wake wa awali wa wabunge 3 na viti maalumu vya CUF vinaashilia mpasuko.
 
I am afraid this is mere fear of unknown or a deliberate effort to divert peoples' thinking from real issues affecting our country at the moment. What are evidencies of the so called UDINI? Hakuna kitu msitupandikizie mawazo ya ajabu ya vitu visivyokuwepo kwenye mawazo yetu.
 
mod please futa hii post; it is sickening, naona huyo alkaida au al=shabab; hafai kwenye hii forum, ban ban ban
 
Tanzania Fact sheet: Christians 30% Muslims 35% Others 35% Source: CIA Website. Choko choko za udini mara nyingi huanzishwa na kundi la pili hapo juu. Nawashauri wasifanye hivyo kwa sababu mwishowe hawatakuja kutawala Tanzania TENA kwa sababu kundi la tatu ni rahisi zaidi kujiunga na la kwanza katika uongozi kuliko kwenda la tatu ambalo mara nyingi huogopwa na wengi. NI USHAURI TU, NAWAKILISHA.
Ujinga mtupu...
 
Pengine hamkumbuki history ya tanganyika, mahakama ya kadhi ilikuwepo kabla ya uhuru na miaka ya mwanzoni mwa uhuru. sio kitu kigeni, kama wakoloni waliruhusu na hawakuwa waislam, je sisi watz wenyewe. Fuatilieni Mahakama ya kadhi ni nini na inafanya kazi zipi. Baada ya hapo toa hoja. Tusiingize Ushabiki wa Simba na Yanga. Tujadili Mafisadi awe Muislam, Mkristo au Kama kingunge.

Pamoja na kuwa mgeni hoja yako inaelekea kusema watawala wetu walikosea kuondoa Mahakama ya kadhi. Lakini toka tupate uhuru mtawala ni TANU a.k.a CCM (Chakachua). Kwa hiyo JK akizungumzia udini ana maslahi nao. Mimi udini sijui ni kitu gani kwenye familia yangu ndogo yenye kila mtu na dini yake na tunaishi bila kuulizana dini.
 
I am afraid this is mere fear of unknown or a deliberate effort to divert peoples' thinking from real issues affecting our country at the moment. What are evidencies of the so called UDINI? Hakuna kitu msitupandikizie mawazo ya ajabu ya vitu visivyokuwepo kwenye mawazo yetu.

I agree with you. Udini upo kwa wanasiasa wakiwahamasisha watanzania wenye upeo mdogo wa kuona mambo au wasiokuwa na elimu kubwa ya kutambua yapi ni matatizo ya kweli ya Tanzania. Udini sio tatizo Tanzania. Ni tatizo la wanasiasa waroho wa madaraka.
 
Ili kuonesha kuwa jambo la udini linamkera kutoka moyoni anatakiwa kuwafukuza wasaidizi wake wote waliotumia propaganda za udini katika kumpatia JK advantage ya kisiasa. Na kuanzia awafukuze wakurugenzi wa IKULU waliofadhili tangazo la udini kisha ashuke kwa vilaza wake kina Tambwe Hiza.
hivi ni tangazo gani hilo la kidini walilolitoa huko ikulu??
 
useless anaongelea udini kupindisha ukweli, CCM has no policy, only ufisadi, sisi tunaona uchafu wa CCM, TAKUKURU, CHENGE, Meghji, sasa kuwapotezea wananchi eti UDINI, stop lying JK na ndio maana ulikosa kura yangu na ulishindwa mkaiba kura, udini, udini, udini, JK ndio mdini mkubwa
 
Hawa si ndio walidhamini tangazo la udini kupitia Ikulu kama ilivolipotiwa na raia mwema?
Alafu huu udini wanaohubiri mbona hawatoi evidences watu wanaishia kusema udini udini bila kusubstantiate where

Ndo maana nkasema yeye ndo mhubiri na mtendaji mkuu wa udini nchini!
 
Jamani labda mjamaa alikuwa anajikemea; si unajua tena kuji-hit directly huwa ngumu. Maana yeye ndiye mwanzilishi na mwendelezaji; sasa anamkemea nani kama si yeye mwenyewe? Mbona asiseme kwa mkazo ufisadi na yale ambayo watanganyika wangependa kusikia:
 
Ni magazeti gani yalikuwa ya kwanza kuandika habari za kwamba Slaa katumwa na Kanisa? Nakumbuka magazeti ya Uhuru, Rai, Alnuur, Alhuda na Mtanzania ndiyo yaliyolikalia bango jambo hilo. Haya magazeti ni ya nani? Na je ni magazeti gani yaliyoandika waziwazi kwamba Waislamu wawachague Waislam wenzao. Kwa kumbukumbu zangu ni Al huda na Al nuur. Je ni hatua gani zilizochukuliwa hadi hivi leo dhidi ya magazeti haya? Sikuwa kusikia popote pale, CHADEMA wakiongelea suala la udini. Sasa iweje leo anayakemea aliyoyaanzisha yeye mwenyewe.

Tunataka Kikwete achukue hatua kubwa zaidi ya kukemea kwenye hotuba, tunataka awakamate wahariri wa magazeti ya Al nuur na Al huda, pia Mtanzania na Uhuru. kwa kuchochea udini nchini. Hii itasaidia sana kupunguza idadi ya wahariri wahuni kama hawa wa CCM ambao wanataka kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini.
 
Asante Lukolo, hapo umenena!!! Wasione watu wajinga na wasio na kumbukumbu
 
Mwanakijiji, tafadhali usiweke wimbo huu tena kwenye Video zako bila kuweka maelezo mapema maana imebidi niache kula na kusimama na nilipotaka kushika Moyo, nikakumbuka kuwa nakula Mzinga wa Panki, duu..... Kasheshe!!!!!!

Asante kwa kutuwekea
 
Hawa watawala wanasahau kabisa wako madarakani kwa ajili ya nani. Hii agenda ya udini inanikera mno maana wanaikuza kwa maslahi yao. Itamsaidia nani? Kweli tunataka kuua utaifa na amani yetu kwa sababu ya miaka mitano ya kukaa madarakani? Where have we lost our minds?

Yes we have forgotten who we are and what God has blessed us with. Tunaanza kushikana mkono na shetani kwenye mambo yatakayotudi bila huruma. Duuh! Tujifunze ya Kosovo na Serbia kabla ya kuanza kupalilia moto msitu wenye majani makavu.
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom