Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Hapa naona kuna watu wapo short sighted..

Kusema kwamba chama flani hakimtambui Rais, it does not mean total dismissal na kususia kila kitu..maana ukitumia basis hiyo utajikuta huna pahali pa ku-break the vicious cycle.

Mi nawasapoti Chadema, kwa muono wao. Na I hope they have smart team to see this through. Tumechoshwa na business as usual.
 
Msaada jamani siwezi kuifungua wala kuisikiliza hiyo audio! hata siioni, ushamba huu nao, hebu nisaidieni nifanyeje?
 

Abdulhalim:

Mimi ni mmoja nipo short sighted. Vyama vya upinzani Tanzania. Havisomi katiba ya nchi. Siku zote wanajaribu kujiingiza kwenye uchaguzi na wakitegemea kubadilisha katiba iwapo watashinda. Hii peke yake ni political suicide.

Wakishindwa ndipo wanatumia haki za kikatiba. Toka 1995-2010, nitajie hoja moja ya kubadilisha katika iliyopelekwa bungeni au mahakamani iliyotaka kubadili katiba. Afadhari Mtikila anatumia mahakama kuliko hivi vyama vingine vinavyoshinda ubunge.
 

Thinker Za10,

Mahakama ni mojawapo tu ya mihimili ya JMT, binafsi sioni ubaya wa Vyama Mbadala(VM) kutumia mhimili wa bunge. IMO naona ni bora zaidi maana vinaonesha kwamba walau vinakubalika na sehemu fulani ya jamii (hivyo kuwakilisha sehemu hiyo). Hii mandate ndio walau inajustify uhalali wa wao kuweka madai kuhusu uendeshaji wa nchi hii. Mtu kama Mtikila anaweza kuwa na hoja huko mahakamani, lakini hana ushawishi wa ksiasa, na hata akipuuzwa watu wataona poa, na ndio maana hafanikiwi. So it is important kuwa politically popular then mambo mengine yafuatie.
 

Chama1:

Unaboronga. Urais unapatikana kwa wale waliotumia haki zao za kikatiba kupiga kura. Hivyo basi hata kama Dr. Slaa angetangazwa kuwa ni mshindi, asingepata kura zaidi ya milioni 5. Na kwa mtaji uliozungumza na yeye asingefaa kuongoza watu milioni 46.

Vilevile unaboronga kusema kuwa katiba yetu ilitungwa na mkoloni. Katiba ya mkoloni ilikuwa inaruhusi wagombe huru. Na ukitaka mifano nitakupa.

Na ukiirudisha katiba ya alioacha mkoloni leo, CCM haikai madarakani zaidi ya mwaka mmoja na JK inabidi atafute kazi nyingine.
 

Kwa hiyo kuna kitu kama kumtambua rais nusu mkuu? Kwamba unamtambua kwenye mambo fulani tu, mengine humtambui?

Mimi ninavyojua kama unamtambua unamtambua, kama humtambui humtambui, sio akileta jina mpigie kura kuhakiki kama Waziri Mkuu mnapiga kura uzuri, akija kuhutubia bunge hamumtambui.

Sasa mlivyopiga kura mlipigia pendekezo la nani? Hii inconsistency, hii immaturity inanifanya nijiulize kwamba hawa CHADEMA kweli wanajua wanachofanya au wana stumble along tu ?

Kama kuna watu shortsighted ni hao wanaokubali kuhalalisha chaguo la Kikwete kama rais, siku mbili baadaye wanatoka bungeni kwa madai kwamba hawamtambui Kikwete.

Mi ningependa kuona watu wanaosema hawamtambui Kikwete wako serious katika hili, sio wana flip flop.
 

Thinker Abdulhalim:

Kama wanafanya hivyo kama tactical battle siwalaumu. Kwa sababu ni lazima waendeleze visibility yao. Pamoja na hayo wawe wanaipitia hile document aliyosaini mzee A. Change inayoitwa katiba.
 

Kwa sababu JK ni zoba tu. Ningekuwa katika nafasi yake ningemteua mtu mmoja mashuhuri kutoka CHADEMA kuwa mbunge maalumu na baadaye niwasikie.
 
 

'Kutomtambua rais' is not in a strict way, kama nilivyosema.

Kitu ninachokiona cha msingi hapa, ni mechanism ya kueka madai yao kwenda kwene ufanikishaji na matokeo yake kwa mustakabali wa taifa.
Bahati mbaya Chadema wanaona kunahitajika marekebisho, mathalan ya muundo wa NEC, wakati vyama vingine vinaona pouwa tu, pengine kwa sababu havikuwa na wagombea wenye ushawishi kama Chadema, sasa huu ni udhaifu wa vyama mbadala, maana it is about the principal not the event or the individuals.

Nakubali kwamba vyama mbadala vina maono na methods tofauti kuhusu uendeshaji wa nchi, lakini kama chama cha siasa hakioni umuhimu wa tume huru ya uchaguzi, na kuipa kipaumbele hii hoja, nadhani huko tuendako ni kiza kinene.
 
Thinker Abdulhalim:

Kama wanafanya hivyo kama tactical battle siwalaumu. Kwa sababu ni lazima waendeleze visibility yao. Pamoja na hayo wawe wanaipitia hile document aliyosaini mzee A. Change inayoitwa katiba.

Thinker Za10,

Ndio maana nikasema ninatumai Chadema wanayo timu nzuri ya kuratibu haya matukio ili kuwepo na realistic goals.
 
Makamanda;

Nitatumia mfano wa hali ya chini sana ili nieleweke.

Mke anapokuwa katika ndoa na akaona mumewe hamtendei haki katika jambo fulani na wala hamsikilizi kwa namna yoyote. Je, mke akimyima unyumba mume, does it mean anything kwa mume? Does it send any message to Mume?

Kitendo cha CHADEMA ni mfano wa kuonyesha kuwa mfumo mbovu na unahitaji mabadiliko. Kitendo cha rais kuduwaa wakati wanatoka, CUF kurukia viti vya mbele, wabunge wa CCM kupagawa na makelele, media kuliongelea hili, na JF nk kukesha hapa na kulijadili ni ushahidi tosha kwamba ujumbe umefika.

What will be next strategy, hicho ndicho ambacho wengi wetu tunakisubiri.

Niliwahi kuandika kuwa CHADEMA wakija na ushahidi na data zisizo na mashaka kuwa kura zilichakachuliwa, then njia ya kuelekea kudai katba mpya itakuwa iko wazi unless kama Bunge letu litakuwa ni Bunge la vichaa.

QED
 
Thinker Abdulhalim:

Kama wanafanya hivyo kama tactical battle siwalaumu. Kwa sababu ni lazima waendeleze visibility yao. Pamoja na hayo wawe wanaipitia hile document aliyosaini mzee A. Change inayoitwa katiba.
Kaka Zakumi,

On that note nipo na wewe, lakini for how long they wish to continue with this political immaturity sort of behaviour. Kesho JK akisema hebu hao Chadema wam-tie na hizo accusation zao at the court of law kama kulikuwa na mkono wake directly on the influence of the presidential results. Ndio wengi tuna amini labda kulikuwa na namna jinsi haya matokeo yalivyokuja na ucheleweshwaji wake.

Is the president responsible yes but indirectly (unaweza sema remotely he could influence through his powers), sasa mtu apati adhabu kubwa for abeiting in the court of law. Kwa hiyo kitendo cha kumsusia Raisi ni pointless. Hila kitu muhimu ni kuhakikisha haya mambo hayajirudii tena. Kwa kuanzia bunge lianze na tume huru ya kuchaguliwa yenye wawakilishi wa pande mbili, uzuri wake kuna wataalamu wa sheria bungeni pande zote za mbili kubwa. Kuwepo na baadhi ya independent lawyers mchakato wa katiba uanze kuirekebisha katiba ya sasa sehemu zenye mapungufu.

Lakini suala la kumsusia raisi wakati amna direct link sioni kama ni la kimanufaa kwa Taifa especially baada ya uchaguzi wakati tension bado ziko juu sehemu nyingine utajikuta unazua mengine. Na sasa kiongozi wa chama ukisema hadharani umtambui raisi what sort of message unamtumia yule uncle wangu kule kijijini kwetu Nyabula ambae amejawa na hasira tayari na uongozi wa CCM, its only a matter of time kabla hajaanza kurusha panga lake.

Chadema wamefanya nini tangia kushindwa (ingawa si kauli waipendayo, labda niongeze baada ya kudhulumiwa) ku-address matatizo waliyoyaona wakati wa uchaguzi. Wao wameamua straight up kumu attack president, wakati katiba mbovu ni tatizo ambalo nimelikuta humu JF wakati najiunga ya kuwa katiba inaitaji marekebisho. Watu walikua wanaimba wimbo inabidi kuhakikisha katiba iangaliwe vizuri kabla ya uchaguzi kuepuka indirect influence wao wapi wanaona litmus paper inaweza jibadili bila ya catalyst. Ni kitu ambacho wengi tulijua CCM itashinda kwa namna yoyote. Sasa kwanini wasianze mchakato muhimu, kulikoni kuja na kauli na matendo ambayo yanaweza amsha hasira za mjomba wangu mwenye uwezo mdogo wa fikra kutokana na elimu yake. yeye ni very vulnarable na emotions zake ndipo hapo napo ona busara aikutumika.
 

Hiyo ni namna ya ktoa hotuba inayoendana na matatizo - kwanza unamvuta mtu kule anakopenda halafu mwisho unambomoa. Hivi akisema kura zimechakachuliwa maana yake ni nini? Sio kunyang'nywa Urais, Ubunge, Udiwani? Kwenye Press Conference ya kwanza/ pili wakati NEC wanaendelea kutangaza matokeo au baada ya kutangaza mshindi Chadema walisema hata kama JK angepata 98% au 50.01% kwa uwazi wala wasingekuwa na shida yoyote.

Wewe unahitaji kwenda shule tena ikiwezekana kuanzia chekechea ili uweze kuelewa philosophical speeches!
 
Hata mbwa koko nao hubweka. Kuna haja ya kufikiria strategy yao upya. Otherwise maswali ni mengi mno!

Strategy ya Chadema ndiyo ''standard'' duniani kote, ndiyo njia ya kistaarabu ya kupinga au kuonyesha kutorishwa na jambo. Kinyume cha njia hii n kuwaita wananchi mtaani jambo ambalo litaleta madhara makubwa kwa jamii yote. Ikumbukwe kuwa mkakati wa CCM kujiimarisha ni pamoja na kuwatega Chadema ili yakitokea tusiyotarajia wapate kauli mbiu, wapinzani ni watu wa vurugu.
Urais ni taasisi [institution] na kwahiyo kususia hotuba haina maana ya kumsusia Kikwete kama Mwanandamu bali kuisusia taasisi inayoongozwa na kikwete.
Serikali si mtu ni chombo chenye kumiliki vyombo vya dola na sheria za nchi. Hata kama Rais wa nchi yoyote ameingia madarakani kwa mtutu au mapinduzi, as long as anamiliki vyombo vya dola huyo ndiye rais. Hii haijengi uhalali wa rais huyo wala serikali yake. Ni kwa mantiki hiyo Chadema wanasema wanapinga uhalali wa Rais.
Dictator Idd Amin au Bokassa au Somoza wote walikuwa ni marais na walipewa hadhi zote kama marais, lakini hiyo haikujenga uhahali wa wao kuwa marais. Rais Mwai Kibaki wa Kenya alipoona kuna dalili za kushindwa uchaguzi alimwita Jaji mkuu haraka haraka na kuapishwa ili kuweza kumiliki vyombo vya dola, hili bado halijengi uhahali wa yeye kuwepo madarakani.
Mimi binafsi nadhani njia wanayotumia Chadema ni sahihi na ya kiustaarabu.
 

Ndugu yangu ninakuonea huruma kwa jinsi unavyotengeza theses zako. sentensi zako mbili kwenye paragraph ya kwanza zinaonesha kwa jinsi gani kuwa ni citizen mwenye political immaturity sort of behaviour kwa sababu katiba inamkataza hata yeye JK kama Rais kuchunguza matokeo ya Urais, sasa itakuwaje afanye hivyo? Si atakuwa amevunja katiba na kosa la kuvunja katiba ni kuondolewa madarakani?

Naomba features/ characteristics za political maturity sort of behaviour kwa kutoa mifano kokote duniani?
 
<br />
<br />

Wanaweka Dr. Slaa
 

Wakati Zitto alipowasilisha hoja kuhusu mkataba wa Buzwagi, aliadhibiwa na Bunge. huku nje akawa shujaa na kuwapa nafasi CHADEMA kuzunguka kwa wananchi kueleza kilichojiri. message ilifika na serikali ilitikisika. Dr. Slaa alipotaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ufisadi benki kuu, alizuiliwa. CHADEMA kilikwenda kwa wananchi na kumwaga yote wazi. kulikuwa na vitisho vingi vya kupelekwa mahakamani na kejeli za kutumia "data za kwenye intaneti" yaani zisizo na ukweli. yaliyofuatia yanajulikana. Tunajua uchaguzi wa 2010 ulikuwa tofauti kabisa na chaguzi zilizopita, kwa maana ya moto uliowashwa na upinzani hasa CHADEMA. CHADEMA wamedemonstrate beyond reasonable doubt kwamba wanao uwezo wa kuongoza mapambano na kuitikisa CCM na serikali yake. CHADEMA ilivyokuwa mwezi may 2010 sio ilivyokuwa Oktoba 2010. kisa? mwezi July waliamua kumsimamisha Dr. Slaa kugombea urais. sasa baada ya uchaguzi CHADEMA wangeweza tu kusema ok, yote yamepita tujiandae na 2015. lakini hawakufanya hivyo. wamepick issue na uchaguzi ulivyofanyika. huu ni umakini. Ndio upinzani. kosa la mwenzio ni mtaji kwako. CHADEMA ni chama cha siasa cha upinzani. that is exactly what they are doing! na wameandikishwa kisheria kufanya yote hayo, kwa mujibu wa sheria. wameshavunja sheria gani? kwa rekodi yao so far, baada ya miezi 6 tunaweza kuzungumzia gains walizopata baada ya action yao ya kuprotest. hii ni protest waliyopanga wao kuifanya. kusema eti haina maana kwa sababu wanadai hawamtambui rais wakati wanashiriki baadhi ya process zake au hii, si hoja ya msingi. matokeo ya protest yao yataonekana muda si mrefu. I bet you will be disappointed!
 


hawezi kemea Yeye ndiye aliye chonga hayo mambo yote ya kumchafua Dr Slaa, indirectly ndio maana kakaa kimya hadi uchaguzi uishe, ana visasi huyu we mwone tu, huoni madudu anayofanya kuwapigia debe, kuteua hata mafisadi like Meghji, he doesn't care, duuuuh
 
recently

the moment Barack Obama was announced the winner by the media, Senator McCaine immediately announced at his disappointed audience my friends 'America has spoken', to ease the tension despite his racial tactics during his campaign he knew his words had huge implications at that moment.

Despite much scepticism on the authenticity of Bush the II first victory, Al gore accepted defeat.

Recently on the UK general election many constituencies which were under the labour government previously had shutted whilst hundreds of voters were still in queues, and had to be turned home, the labour party have decided the incidents need parliamentary revision rather than making it a political argument in the public.

You know why its important to calm the public and how crucial is the statement of the leader, try figure you're the expert.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…