Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Wakati Zitto alipowasilisha hoja kuhusu mkataba wa Buzwagi, aliadhibiwa na Bunge. huku nje akawa shujaa na kuwapa nafasi CHADEMA kuzunguka kwa wananchi kueleza kilichojiri. message ilifika na serikali ilitikisika. Dr. Slaa alipotaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ufisadi benki kuu, alizuiliwa. CHADEMA kilikwenda kwa wananchi na kumwaga yote wazi. kulikuwa na vitisho vingi vya kupelekwa mahakamani na kejeli za kutumia "data za kwenye intaneti" yaani zisizo na ukweli. yaliyofuatia yanajulikana. Tunajua uchaguzi wa 2010 ulikuwa tofauti kabisa na chaguzi zilizopita, kwa maana ya moto uliowashwa na upinzani hasa CHADEMA. CHADEMA wamedemonstrate beyond reasonable doubt kwamba wanao uwezo wa kuongoza mapambano na kuitikisa CCM na serikali yake. CHADEMA ilivyokuwa mwezi may 2010 sio ilivyokuwa Oktoba 2010. kisa? mwezi July waliamua kumsimamisha Dr. Slaa kugombea urais. sasa baada ya uchaguzi CHADEMA wangeweza tu kusema ok, yote yamepita tujiandae na 2015. lakini hawakufanya hivyo. wamepick issue na uchaguzi ulivyofanyika. huu ni umakini. Ndio upinzani. kosa la mwenzio ni mtaji kwako. CHADEMA ni chama cha siasa cha upinzani. that is exactly what they are doing! na wameandikishwa kisheria kufanya yote hayo, kwa mujibu wa sheria. wameshavunja sheria gani? kwa rekodi yao so far, baada ya miezi 6 tunaweza kuzungumzia gains walizopata baada ya action yao ya kuprotest. hii ni protest waliyopanga wao kuifanya. kusema eti haina maana kwa sababu wanadai hawamtambui rais wakati wanashiriki baadhi ya process zake au hii, si hoja ya msingi. matokeo ya protest yao yataonekana muda si mrefu. I bet you will be disappointed!
Kimeenda kikarudi, sawa kutafuta popularity kwa hoi polloi wanajua, na hiyo ni part ya politics. Lakini tukubali strategic thinking bado wanajifunza, wanapapasa njia, wanatunga mambo huku wanaenda, hawajapanga mipango ya muda mrefu.
Wangekuwa makini wasingepigia kura chaguo la Kikwete uwaziri mkuu, halafu hapo hapo wakasema hawamtambui Kikwete kama rais, hii ni point ya embarassment.
CHADEMA wamefanya makubwa kuliko chama kingine cho chote cha upinzani Tanzania bara, lakini hili linaweza kuwa linatokana na fact kwamba hakukuwa na upinzani wa maana kabla.
Kwa hiyo badala ya kubweteka na kuwamwagia misifa kem kem, wanayostahili na wasiyostahili, wapenda mageuzi ya kweli tunataka kuona chama kina mature, kinaleta upinzani wa kweli.
Tunataka Dr. Slaa anavyoongelea "chama kilicho consistent" kama alivyosema leo, tuweze kumuamini, tusione anatuambia politiki tu.
Kwa sababu leo Dr. alivyosema chama kiko consistent nikaona kama vile anatania, chama consistent kinapokataa kumtambua rais hakipigii kura chaguo la rais huyo kuwa waziri mkuu, otherwise kitawa confuse wananchi kuhusu kumtambua/ kutomtambua rais. Na Slaa atakaposema "CHADEMA ni chama consistent" wengine tutasikia anasema "CHADEMA ni chama inconsistent"
Wanasema actions speak louder than words, huwezi ku act inconsistently halafu ukasema una chama consistent halafu ukafikiri unaweza kuwachota watu kwa euphoria ya uchaguzi tu.
CCM tunawajua uozo wao, nasikitika kuona CHADEMA wanataka ku squander an opportunity to show the Tanzanian public a mature alternate party.