Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Wakati Zitto alipowasilisha hoja kuhusu mkataba wa Buzwagi, aliadhibiwa na Bunge. huku nje akawa shujaa na kuwapa nafasi CHADEMA kuzunguka kwa wananchi kueleza kilichojiri. message ilifika na serikali ilitikisika. Dr. Slaa alipotaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu ufisadi benki kuu, alizuiliwa. CHADEMA kilikwenda kwa wananchi na kumwaga yote wazi. kulikuwa na vitisho vingi vya kupelekwa mahakamani na kejeli za kutumia "data za kwenye intaneti" yaani zisizo na ukweli. yaliyofuatia yanajulikana. Tunajua uchaguzi wa 2010 ulikuwa tofauti kabisa na chaguzi zilizopita, kwa maana ya moto uliowashwa na upinzani hasa CHADEMA. CHADEMA wamedemonstrate beyond reasonable doubt kwamba wanao uwezo wa kuongoza mapambano na kuitikisa CCM na serikali yake. CHADEMA ilivyokuwa mwezi may 2010 sio ilivyokuwa Oktoba 2010. kisa? mwezi July waliamua kumsimamisha Dr. Slaa kugombea urais. sasa baada ya uchaguzi CHADEMA wangeweza tu kusema ok, yote yamepita tujiandae na 2015. lakini hawakufanya hivyo. wamepick issue na uchaguzi ulivyofanyika. huu ni umakini. Ndio upinzani. kosa la mwenzio ni mtaji kwako. CHADEMA ni chama cha siasa cha upinzani. that is exactly what they are doing! na wameandikishwa kisheria kufanya yote hayo, kwa mujibu wa sheria. wameshavunja sheria gani? kwa rekodi yao so far, baada ya miezi 6 tunaweza kuzungumzia gains walizopata baada ya action yao ya kuprotest. hii ni protest waliyopanga wao kuifanya. kusema eti haina maana kwa sababu wanadai hawamtambui rais wakati wanashiriki baadhi ya process zake au hii, si hoja ya msingi. matokeo ya protest yao yataonekana muda si mrefu. I bet you will be disappointed!

Kimeenda kikarudi, sawa kutafuta popularity kwa hoi polloi wanajua, na hiyo ni part ya politics. Lakini tukubali strategic thinking bado wanajifunza, wanapapasa njia, wanatunga mambo huku wanaenda, hawajapanga mipango ya muda mrefu.

Wangekuwa makini wasingepigia kura chaguo la Kikwete uwaziri mkuu, halafu hapo hapo wakasema hawamtambui Kikwete kama rais, hii ni point ya embarassment.

CHADEMA wamefanya makubwa kuliko chama kingine cho chote cha upinzani Tanzania bara, lakini hili linaweza kuwa linatokana na fact kwamba hakukuwa na upinzani wa maana kabla.

Kwa hiyo badala ya kubweteka na kuwamwagia misifa kem kem, wanayostahili na wasiyostahili, wapenda mageuzi ya kweli tunataka kuona chama kina mature, kinaleta upinzani wa kweli.

Tunataka Dr. Slaa anavyoongelea "chama kilicho consistent" kama alivyosema leo, tuweze kumuamini, tusione anatuambia politiki tu.

Kwa sababu leo Dr. alivyosema chama kiko consistent nikaona kama vile anatania, chama consistent kinapokataa kumtambua rais hakipigii kura chaguo la rais huyo kuwa waziri mkuu, otherwise kitawa confuse wananchi kuhusu kumtambua/ kutomtambua rais. Na Slaa atakaposema "CHADEMA ni chama consistent" wengine tutasikia anasema "CHADEMA ni chama inconsistent"

Wanasema actions speak louder than words, huwezi ku act inconsistently halafu ukasema una chama consistent halafu ukafikiri unaweza kuwachota watu kwa euphoria ya uchaguzi tu.

CCM tunawajua uozo wao, nasikitika kuona CHADEMA wanataka ku squander an opportunity to show the Tanzanian public a mature alternate party.
 
Ni kweli tanzania kuna udini. Anae ukemea ndiye mdini zaidi. Yeye, makamu wake, rais wa zanzibar, makamu wake wawili ni dini moja. Wabunge wa kwanza wa kuteuliwa na rais baada ya uchaguzi wote watatu ni dini moja - meghji, nahodha, na yule mwingine wa zenj. Anakemea anchokifanya.

Macinkus
 
Kaka Zakumi,

On that note nipo na wewe, lakini for how long they wish to continue with this political immaturity sort of behaviour. Kesho JK akisema hebu hao Chadema wam-tie na hizo accusation zao at the court of law kama kulikuwa na mkono wake directly on the influence of the presidential results. Ndio wengi tuna amini labda kulikuwa na namna jinsi haya matokeo yalivyokuja na ucheleweshwaji wake.

Is the president responsible yes but indirectly (unaweza sema remotely he could influence through his powers), sasa mtu apati adhabu kubwa for abeiting in the court of law. Kwa hiyo kitendo cha kumsusia Raisi ni pointless. Hila kitu muhimu ni kuhakikisha haya mambo hayajirudii tena. Kwa kuanzia bunge lianze na tume huru ya kuchaguliwa yenye wawakilishi wa pande mbili, uzuri wake kuna wataalamu wa sheria bungeni pande zote za mbili kubwa. Kuwepo na baadhi ya independent lawyers mchakato wa katiba uanze kuirekebisha katiba ya sasa sehemu zenye mapungufu.

Lakini suala la kumsusia raisi wakati amna direct link sioni kama ni la kimanufaa kwa Taifa especially baada ya uchaguzi wakati tension bado ziko juu sehemu nyingine utajikuta unazua mengine. Na sasa kiongozi wa chama ukisema hadharani umtambui raisi what sort of message unamtumia yule uncle wangu kule kijijini kwetu Nyabula ambae amejawa na hasira tayari na uongozi wa CCM, its only a matter of time kabla hajaanza kurusha panga lake.

Chadema wamefanya nini tangia kushindwa (ingawa si kauli waipendayo, labda niongeze baada ya kudhulumiwa) ku-address matatizo waliyoyaona wakati wa uchaguzi. Wao wameamua straight up kumu attack president, wakati katiba mbovu ni tatizo ambalo nimelikuta humu JF wakati najiunga ya kuwa katiba inaitaji marekebisho. Watu walikua wanaimba wimbo inabidi kuhakikisha katiba iangaliwe vizuri kabla ya uchaguzi kuepuka indirect influence wao wapi wanaona litmus paper inaweza jibadili bila ya catalyst. Ni kitu ambacho wengi tulijua CCM itashinda kwa namna yoyote. Sasa kwanini wasianze mchakato muhimu, kulikoni kuja na kauli na matendo ambayo yanaweza amsha hasira za mjomba wangu mwenye uwezo mdogo wa fikra kutokana na elimu yake. yeye ni very vulnarable na emotions zake ndipo hapo napo ona busara aikutumika.

Bro JC:

Kuna thread nyingi tu humu nime-comment kuhusu katiba. Mimi sio mtaalamu wa sheria lakini katika katiba semantic ni kitu muhimu sana. Kwa kupitia comments nyingi za watu hapa, hoja nyingi zinajengwa kwa emotions, na watu hawajuhi katiba inasema nini au semantic ya ibara ina maana gani.

Kwa mfano: watu wanasema kuwa katiba inasema kuwa NEC ikishatangaza matokeo ya urais, basi hakuna mahakama itakayouchunguza matokeo ya urais kwa hiyo JK kapita. Kuchunguza matokeo ya urais haina maana kuwa msimamizi aliyekiuka kazi zake aachiwe.

Ukweli wa mambo hakuna mahakama inayozuia mtu au kundi la watu kutofungua kesi. Fungua kesi na iachie mahakama iseme hivyo. Pili framing ya kesi unayofungua mahakamani ni kitu muhimu. Kwa mfano ni haki ya mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura kupewa nafasi yake. Hivyo unaweza usishitaki mojamoja matokeo ya urais, lakini ukafungua kesi ya kuonyesha kuwa process nzima sio halali.

Tatu Tanzania inafuata common law, hivyo hukumu za mahakama zina-set a precedent kwa kesi zinazokuja. Hivyo mwanasiasa yoyote anayeshindwa kutumia mahakama namuona na yeye akipewa nafasi atarudia madudu yaleyale anayofanyiwa.
 
Waliokua wanasema Kikwete chaguo la Mungu hawakuwa na udini?
 
Swala la udini kalianzisha mwenyewe na amekuwa akilihubiri wakati wote wa kampeni.Hakuna kiongozi mwingine wa chama chochote alokuwa anazungumzia udini zaid ya JK.Yeye aeleze huo udini aliuonawapi na nani hasa anauhubuiri.Hiyo ni hofu yake kwa kuwa wanazuoni hawakumpigia kura.
 
Nilikua na support hii move ya chadema mpaka nilipomsikiliza Dr Slaa. Labda hakujitaarisha kwa sababu analikoroga kabisa. Anasema huu ni mwanzo tu, ata mobilize people for his personal gains ....MOVE ON SLAA, elections are over, you were defeated, its time you swallow your pride and build this nation. Babadiliko yatafanyika bungeni....Nenda kajipange vizuri 2015...
 
Chama1:

Unaboronga. Urais unapatikana kwa wale waliotumia haki zao za kikatiba kupiga kura. Hivyo basi hata kama Dr. Slaa angetangazwa kuwa ni mshindi, asingepata kura zaidi ya milioni 5. Na kwa mtaji uliozungumza na yeye asingefaa kuongoza watu milioni 46.

Vilevile unaboronga kusema kuwa katiba yetu ilitungwa na mkoloni. Katiba ya mkoloni ilikuwa inaruhusi wagombe huru. Na ukitaka mifano nitakupa.

Na ukiirudisha katiba ya alioacha mkoloni leo, CCM haikai madarakani zaidi ya mwaka mmoja na JK inabidi atafute kazi nyingine.

Naomba unikumbushe mwaka gani baada ya kupata uhuru tulitengeneza katiba mpya baada ya uhuru? Kilichofanyika ni bandika bandua tu haikuwa katiba ambayo tuliandika wenyewe, kama una muda jaribu kupitia katiba ya mwaka 1961 baada ya uhuru, katiba ya 1965 na katiba ya mwaka 1977 kilichofanyika si kubadili katiba bali kubadilisha baadhi ya vipengele vilivyomo ndani ya katiba ili kukipa chama madarakani; chamsingi tu katiba iliyopo imepitwa na wakati, kwa hiyo kama katiba ya mkoloni iliruhusu wagombea binafsi sasa hivi tunaogopa kitu gani? Umeongea maneno mazuri sana unaposema Raisi anapatikana kwa wale wanaotumia haki yao kimsingi je hawa wananchi zaidi ya mil. 10 ambao walitumia haki yao ya msingi kuchagua Raisi mbona wamedhulumiwa?
 
Baada ya Kikwete kukemea udini imebidi nianze kufuatilia alikuwa anamaanisha nini:::-

Rais wa Jamhuri ya Muungano :: Jakaya Mrisho Kikwete
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano :: Ghalib Bilal
Rais wa Zanzibar :: Ali Mohammed Shein
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar :: Maali Seif Sharif Hamad
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar :: Seif Iddi

Rais Kivuli :: Rostam Aziz
Rais Kivuli wa Pili :: Ridhwan
Chief of Staff of TPDF :: Abd Shimbo
IGP :: Said Mwema
Director of TISS :: Othman Rashid

Mwenyekiti wa CCM :: Yussuf Makamba
Makamu Mwenyekiti wa CCM :: Amani Karume
 
Bro JC:

Kuna thread nyingi tu humu nime-comment kuhusu katiba. Mimi sio mtaalamu wa sheria lakini katika katiba semantic ni kitu muhimu sana. Kwa kupitia comments nyingi za watu hapa, hoja nyingi zinajengwa kwa emotions, na watu hawajuhi katiba inasema nini au semantic ya ibara ina maana gani.

Kwa mfano: watu wanasema kuwa katiba inasema kuwa NEC ikishatangaza matokeo ya urais, basi hakuna mahakama itakayouchunguza matokeo ya urais kwa hiyo JK kapita. Kuchunguza matokeo ya urais haina maana kuwa msimamizi aliyekiuka kazi zake aachiwe.

Ukweli wa mambo hakuna mahakama inayozuia mtu au kundi la watu kutofungua kesi. Fungua kesi na iachie mahakama iseme hivyo. Pili framing ya kesi unayofungua mahakamani ni kitu muhimu. Kwa mfano ni haki ya mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura kupewa nafasi yake. Hivyo unaweza usishitaki mojamoja matokeo ya urais, lakini ukafungua kesi ya kuonyesha kuwa process nzima sio halali.

Tatu Tanzania inafuata common law, hivyo hukumu za mahakama zina-set a precedent kwa kesi zinazokuja. Hivyo mwanasiasa yoyote anayeshindwa kutumia mahakama namuona na yeye akipewa nafasi atarudia madudu yaleyale anayofanyiwa.
Kaka Zakumi,

Hali kadhalika mi pia si expert huko, ndio maana kuna maloya wa siasa nchi za wenzetu. Lakini nnacho jua mimi the basis of balance and check ni independence between the executive, legislature and judiciary. Sasa NEC can not be above mihimili ya uongozi, ndio maana Rev Mtikila ana elewa ni nini maana ya mahakama.

Tatizo kubwa so far pia ni namna hii katiba ilivyo na jinsi uteuzi wa majaji unavyopatikana, kwani huko nako mkono wa executive unafika kwenye uteuzi na kuondoa the meaning of independent autonomy, hilo nalo ni tatizo. Lakini NEC ki sheria hawana nguvu zaidi ya mahakama wao si tawi la uongozi kati ya hayo matatu makubwa kikatiba any way hivyo ndio UK navyojua mimi.

Sasa ki kwetu ingawa kuna kijimfanano fulani na UK, lakini kuna raisi ambae anachaguliwa independently ambapo kwa kweli hapo ndipo katiba ya Tanzania uanza kunipiga chenga madaraka yake na nguvu zake siyajui vyema hila inaonekana ni too much. Lakini in practice the judiciary should be independent and able to intervene whenever necessary its the whole point of balance and checks, therefore i dont see why NEC should have any final say as its not part of the government main body.
 
recently

the moment Barack Obama was announced the winner by the media, Senator McCaine immediately announced at his disappointed audience my friends 'America has spoken', to ease the tension despite his racial tactics during his campaign he knew his words had huge implications at that moment.

Despite much scepticism on the authenticity of Bush the II first victory, Al gore accepted defeat.

Recently on the UK general election many constituencies which were under the labour government previously had shutted whilst hundreds of voters were still in queues, and had to be turned home, the labour party have decided the incidents need parliamentary revision rather than making it a political argument in the public.

You know why its important to calm the public and how crucial is the statement of the leader, try figure you're the expert.

Mimi huwa nawaambia watu siku zote this Slaa guy is bogus!

Kwani angekubali matokeo akasema mwaka huu tumeshindwa tunajipanga upywa tunarudi stronger 2015 angepoteza nini??
 
Kwa tafakari fupi, mimi naona raisi wetu anataka kututoa katika tafakari ya ufisadi na ubabaishaji katika serikali yetu. Kwa hakika dini inaweza kutupumbaza kabisa tukaacha kufuatilia mambo ya kimaendeleo na tukajikuta kwa miaka mitano ijayo tunatafakari kuhusu udini na nchi yetu ikafisadiwa kisawasawa. Naombeni tulimpuuze suala la udini kwani halina mizizi na si msaada kwetu.
Chonde chonde wana JF acheni kulijadili kwani kwa kufanya hivyo tutagawanyika, tutapata waislam na wakristo, wakatoliki na waprotestanti, wasuni na wahabi. Makundi haya yatatufanya tusifuatilie kwa pamoja masuala ya maendeleo na uwajibikaji wa viongozi wetu. Mungu awabariki mwelewe nisemacho.
 
recently

the moment Barack Obama was announced the winner by the media, Senator McCaine immediately announced at his disappointed audience my friends 'America has spoken', to ease the tension despite his racial tactics during his campaign he knew his words had huge implications at that moment.

Despite much scepticism on the authenticity of Bush the II first victory, Al gore accepted defeat.

Recently on the UK general election many constituencies which were under the labour government previously had shutted whilst hundreds of voters were still in queues, and had to be turned home, the labour party have decided the incidents need parliamentary revision rather than making it a political argument in the public.

You know why its important to calm the public and how crucial is the statement of the leader, try figure you're the expert.

You need to be more serious! US and UK are the most democratic countries in our modern world, their elections are based on fairness to both parties involved, more to that they respect their constitutions, incumbents don`t riggs elections to stay in power, they always respect will of the peoples thats why we see smooth transitions of power, Do we do the same in Tanzania? Hell no! Nyerere never failed us, we failed him, JKN was honest and man of the peoples
 
Hivi ni lazima kwa uongozi wa Chadema kusema wanamtambua Kikwete kama Rais ili apate uhalali wa kura Rais? Sote tunajua tume imemtangaza kuwa ni Rais na kisheria ni Rais; lakini hakuna mahali ambapo Mtanzania analazimishwa kumtambua kwani kumtambua au kutomtambua hakumfanyi asiwe Rais. Lakini dhamira safi ikisema haimtambui ni kwa ajili ya dhamira hiyo.
 
Tafsiri ya kikatiba ilikwisha kutolewa na Mahakama zetu kuwa matokeo yanayotangazwa na NEC yaweza kuhojiwa mahakamani endapo tu kama kuna ushahidi NEC haikuzingatia sheria katika kuyatangaza....................

Na hapa NEC haijazingatia sheria kwa kutangaza matokeo kutoka kibindoni kwake badala ya kufuata yale yaliyotangazwa kwenye zaidi ya vituo 52, 000 nchi nzima................................

Chadema bado wanapaswa kwenda mahakamani ili kuibua pia uozo uliopo kwenye mahakama zetu kuwa nazo haziko huru na zahitaji kutinduliwa na kusukwa upya..........i.e total overhaul................kwa sababu haziwezi kumtendea raia haki................................

Bila ya kuyafanya haya..........................Chadema itakuwa imejikaanga kwa mafuta yake yenyewe................chaguzi za 2015 zitafanyika kwa mfumo huu huu wa dhuluma kwa wananchi na kamwe wananchi hawatakuwa na sauti ya kuzima dhuluma...................kwa sababu raia hawatakua na uwezo wa kuwaadabisha viongozi bomu pale wanaposhindwa kukidhi matarajio yao..............................
 
Chama cha Demokrasia Makini wanahaki ya kumtomtambua Mkwere...cha maana Mkwere asitumie mabavu na asikilize malalamiko ya Chadema kama chama kikuu cha upinzani Tanzania kwa sasa. Asifikiri ni kelele za mlango ambazo hazimfanyi mwenye nyumba kukosa usingizi asije akaipindua CHI CHI EMU kuwa chama kisichonamuelekeo cha maana akubali kwamba alichakachua na aunde SERIKALI YA MSETO.

HAKI SAWA...ASIYEPENDA HAKI...NGANGARI KINOMA
CHADEMA JUUU..JUU ZAIDI
 
Thanx sana Mwana nimeridhika na maelezo ya mweshimiwa Raisi na wimbo umenikumbusha kampeni sito rudi nyuma kamwe nilisha chagua na mwamini na nitaendelea kumwamini kwani ametufungua akili na kutuonyesha jinsi tunavyo kandamizwa na wachache.
 
ameanza udini JK,angalia uteuzi wake wa wabunge kumi alivyouanza,wote watatu that is zakhia,mnyaa na vuai ni wa dini yake
 
Nadhani bado sheria ya uchaguzi haijaeleweka sana, hasa urais. Dr Slaa akiongelea kujipanga kwa 2015 yuko sawa maana hamna kinachoweza kubatilishwa na sheria nyingine. Sana sana zitakuwa porojo zisizo na tija. Tiyari JK ni rais, kama urais wake ni batili katika sanduku la kura na bado kaapishwa hiyo imetoka. Sasa ni kufanya kazi ya kubadili sheria na kanuni kandamizi zenye kulinda maslahi ya wachache. Tujitahidi kuuona ukweli na hali halisi ya sheria zetu, lakini bado tusiwe mamuma wa kukubali kila jambo hata kama si sahihi-ndiyo mzee!
 
Makamanda;

Nitatumia mfano wa hali ya chini sana ili nieleweke.

Mke anapokuwa katika ndoa na akaona mumewe hamtendei haki katika jambo fulani na wala hamsikilizi kwa namna yoyote. Je, mke akimyima unyumba mume, does it mean anything kwa mume? Does it send any message to Mume?

Kitendo cha CHADEMA ni mfano wa kuonyesha kuwa mfumo mbovu na unahitaji mabadiliko. Kitendo cha rais kuduwaa wakati wanatoka, CUF kurukia viti vya mbele, wabunge wa CCM kupagawa na makelele, media kuliongelea hili, na JF nk kukesha hapa na kulijadili ni ushahidi tosha kwamba ujumbe umefika.

What will be next strategy, hicho ndicho ambacho wengi wetu tunakisubiri.

Niliwahi kuandika kuwa CHADEMA wakija na ushahidi na data zisizo na mashaka kuwa kura zilichakachuliwa, then njia ya kuelekea kudai katba mpya itakuwa iko wazi unless kama Bunge letu litakuwa ni Bunge la vichaa.

QED
copy that mkuu!
The Following User Says Thank You to Superman For This Useful Post:

Baba Gift (Today)​
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom