Jamani,hivi udini ambao mr. prezzo ametangaza mbele ya bunge kwamba tz imeanza kugawanyika kwa udini, upo wapi uo udini? ktk uchaguzi udini ulikuwa wapi?, si angemention tu kama kidonda kipo kipone?...kwasababu hatujaona watu wakimchagua mtu kwa udini wake, bali kwa sera, hasa ukichukulia vijana wengi wakristo kwa waislam walimpigia Dr.slaa au Lipumba. udini uko wapi? ange mention chama basi tujue.
kwasababu kama ni udini, ccm haina balance kabisa ya dini, basi ccm ndo alikuwa anaiongelea kuwa ni ya kidini. pili, uteuzi wa wabunge wale wa mwanzo wote walilalia upande wa dini moja, kuanzia zakia mehgi ambaye wananchi hawampendi lakini kikwete anampenda. wale wawili za zenji pia mtu mwingine angefikiri kuwa ni udini, lakini hakuna mkristo hata mmoja aliyelalamika kuhusu udini, kwasababu tz hatujali sana udini kwenye selikali.
angalia, mbona rais, makamu wa rais mara zote mbili ni wa dini moja, lakini hilo haliko mioyoni mwa watu, udini ni tatizo kweli hapa tz kiasi cha president kulitangaza mbele ya bunge?
Nijuavyo mimi, yaliyomjaa mtu moyoni ndiyo atakayoyaongea. kama mtu ni mdini, ataongea sana udini tu. pia, wakati mwingine, hata kama wananchi hawakuwa wadini, sasa kwasababu mr.president amelitangaza, atawa alart wananchi waanze kuwa wadini. hivi mr. president anajipanga kwanza kabla ya kuongea hotuba kweli au anazima moto?
Zanzibar ni lini hata siku moja Mkristo alishawahi kushika madaraka, kwani zenji hakuna wakristo? lakini sisi wakristo hatulalamiki...NITAJIENI KIONGOZI YOYOTE HATA WAZIRI TU WA KIKRISTO AMBAYE ALISHAWAI KUPEWA MADARAKA ZANZIBAR. ukinitajia nakupa laki hapahapa...hayupo