Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Kelele za mlango hazimsitui mwenye nyumba. Mchana mtasema usiku mtalala, JMK ndio Rais wa nchi hii, MGB ndio Makamo wa Rais, MS ndio Rais wa Zanzibar na S double ndio makamo zake.

Kama unaweza panda juu nenda ukazibe!
 
Udini, ukabila na ubaguzi wa aina nyingine upo pale inapotokea upendeleo kwa sababu ya dini, kabila n.k. Kama kuna watu tunaojua wanauwezo zaidi lakini hawajapata kazi au kuna mtu kapewa cheo bila sababu za msingi basi hapo ndipo watu waanza kusema mambo ya dini
 
Wadau naomba mnieleweshe juu ya hili huyu kiongozi wa nchi hii amekua akizungumzi suala la kuwepo mpasuko wa kidini hapa nchini tangu wakati wa kampeni, siku ya kuapishwa na hata jana alipokua akizindua bunge. Sijasikia mtu mwingine akiongelea suala la udini zaidi ya rais kikwete, kinana, mwinyi, mkapa na baadhi ya viongozi wa ccm. Naomba ufafanuzi rais anamaanisha nini anaposema kuna nyufa za kidini hata kuwataka viongozi wa dini wachukue hatua! maana mimi na washkaji zangu kibao wakristu tunaishi kwa amani lakini sasa naona wameingiwa na wasiwasi kufuatia kauli hizo za kiongozi mkuu wa nchi ambaye ni dhahiri ameanza kutugawa bila sisi wenyewe kupenda. NAOMBA KUWASILISHA.!
 
Sio udini tu, hata ukabila. Na kibaya ni kwamba, udini na ukabili unapoanza, ni vigumu mhusika kujua kwamba anatenda.
 
Ni hatari kwa kiongozi wa nchi kuanza kupandikiza fikra za kidini vichwani mwa watu. Nahisi ni kama JK huwa hajui athari ya maneno yake anayoyaongea. kuna wakati aliwahi sema takrima haiepukiki, wakati tayari kuna sheria ya kuzuia takrima
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Wewe subiri utaelewa baada ya kuona matokeo ya haya yanayotokea. Na faida ya matokeo hayo ni ya taifa na si ya kichama.
 
Binafsi namshangaa JK. Kama ana ushahidi wa udini mbona sheria za nchi zipo wazi kabisa? Si amwambie tu msajili wa vyama, Bwana Tendwa akifute hicho Chama? Na kama hana ushahidi kwa nini anaropoka hovyo??? Analeta propaganda kila mahali, ndo maana watu siku hizi wamechoka kumsikiliza. Wanasema analeta story za kijiweni.
JK tuambie chama gani kina UDINI la sivyo wewe nawe ni mzushi
 
It was an ACT of confidence that is very true but for how long is this going to last? Mwisho wa siku sie wananchi tutaumia sana kusipokuwa na umoja huko bungeni, we are damned!!

Unataka wawe na umoja wa kuhujumu wananchi au wasielewane kwa faida ya wananchi? Ni afadhali bunge likavurugika kuliko likawa na umoja wa kukubali kila aina ya upuuzi bila kuhoji. We bwana vipi?
 
Walio karibu nae chonde chonde jamani mwambie mkwere asitake kutugawa udini anaosema mbona hatuuoni?
 
Ni jana tu tumemsikia raisi wa JMT akieleza kuwa tatizo la udini ni kubwa katika taifa letu.kauli hii ni nzito na ya kwanza kuwahi kutolewa na kiongozi wa kitaifa mwenye cheo cha Jk.nimefikiri na kujiuliza ni raisi yupi katuletea tatizo hili la udini?jibu nimekosa.je ina maana maraisi wa awamu zilizopita hawakuliona?je limetokea au limeongezeka wakati wa utawala wa jk?kwa nini iwe sasa?nini kimetokea chini ya Jk?au yeye kaamua kuwa muwazi?mimi sijui labda wana jamvi mnatambua!
Nawakilisha or sorry nawasilisha!!!
 
Udini upo tena mkubwa tu. Na anayehubiri huo udini siyo mwingine bali........... Jakaya M. Kikwete. Mtakuja jua siku JK atakapolifufua suala la mahakama ya kadhi, akisaidiana kwenye OIC na mdogo wake aliyeshare naye baba. ( Bernad Mrisho Kikwete. a.k.a. Membe). Nimemchoka huyu jamaa nyie acheni!
 
Wamejaa washabiki ya chadema JF, uwezi kupata mjadala wenye matiki hapa....

Tupo wanaccm, tunachotaka ni Raisi muwajibikaji kwa wananchi wake, wanaccm tumechoshwa na Raisi huyu hana jipya la kutuambia alichobakisha ni kutafuta sympathy kwa wanaccm kwa kujiangusha ovyo kwenye mikutano ya hadhara ya ccm, kama ana kifafa mbona hajaanguka kwenye mikutano ya AU na UN? Wajibu Chadema kwa nguvu za hoja, Raisi anashindwa kuziba mpasuko ndani ya chama ataweza kuziba mpasuko wa kitaifa?
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkuu wa nchi anaeneza propaganda zisizo na tija kwa taifa. Kutokana na wimbo huu wa udini ambao kikwete amekua akiuimba kila anapopata nafasi ya kuongea mbele ya hadhara watu wengi sasa wameanza kuamini kwamba tanzania kuna udini. Huu ni uchochezi wa hali ya juu tena unaoenezwa mkuu wa nchi. HII NI HATARI KUBWA HAKIKA RAIS ANALIPELEKA TAIFA PABAYA NAWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAMKEMEE MARA MOJA!
kwi kwi kwikwi kwi viongozi gani wa dini wanaoweza kumkemea? Thubutu! hutasikia yeyote akinyanyua mdomo! Labda Mnishi:teeth:
 
Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!

Nawaunga mkono kwa kauli yenu hii kwamba CHADEMA walizuga maana walienda kumsikiliza kwenye TV sehemu nyingine.

Basi iwe ni mwiko kwa hotuba zote serikali kufanya ufisadi wa kupoteza petroli, per diem kwa ajili ya kuhudhuria hotuba za Kikwete. Angekaa huko ikulu akatoa hotuba wakati wabunge wote wako vyumbani mwao au seating room.

By the way siku hizi unaweza kusikia au kuona hotuba ukiwa maliwatoni.

Viva CHADEMA kwa kufanya jambo moja lililochokonoa mambo elfu.
 
Mimi sikatai kwamba kuna haja ya protest, kuna haja ya mabadiliko. Nimesema hayo hapa mara nyingi.

Ila naona kama CHADEMA wana squander an opportunity. Dr. Slaa katuambia CHADEMA ni chama consistent, consistency yenyewe ndiyo hii ya kumtambua rais Kikwete kwa kushiriki katika kura ya kumhakiki Pinda, halafu baada ya hapo kutoka nje ya bunge kwa kusema hawamtambui Kikwete kama rais ?

CHADEMA wana a clear strategy au wana improvise as they go ? Kikwete akiteua mawaziri, mawaziri hawa wakija bungeni, wabunge wa CHADEMA watafanya kazi na hawa mawaziri? Watachangia mijadala?

Wakichangia, watachangia kwenye serikali inayoongozwa na nani? Watachangia miswada ya wizara zinazoongozwa na mawaziri walioteuliwa na nani?

Hii habari ya kutomtambua rais CHADEMA wana strategy gani long term? Wanataka ku sit out the rest of this 5 years au watarudi bungeni? Kama watarudi bungeni ni kwa misingi gani? Kama wata sit out watawaambia nini wananchi waliowatuma wawawakilishe bungeni?
Kiranga hii inakusumbua wewe tu. FYI sisi tuliopiga kura ni sisi hawa hawa tutawarudisha maana tunajua nini wanafanya. Nyie ambao hamkupiga kura/mlipigia vyama vingine ndio mnajaribu kujifanya hamtawapigia Chadema next election? Ohhhhhhhh wacha kupoteza muda wako kufikiria haya maana mwaka 2015 omba Mungu uwepo na ushangae jinsi mabadiliko ya uongozi yatakavyokuwa makubwa. Na chadema watakuwa 100 bungeni.
 
:angry:

HAKUNA UDINI TANZANIA, WANASIASA WAACHE PROPAGANDA HIZI KWANI NI UDANGANYIFU MKUBWA SANA, CCM INADANGANYA WANANCHI BILA SABABU ZA MSINGI.

NDUGU ZANGU, KAMA KUNA MTU ANA DATA KUWA KULIKUWA NA UDINI KIPINDI CHA UCHAGUZI ATHIBITISHE HAPA, KWANI NAONA KAMA TUNADANGANYWA NA KUTAKA KUDANGANYIKA.

CCM ACHENI UZUSHI HUU, LA SIVYO TUTAANDAMANA KUPINGA HILI, TUMECHOKA KUBURUZWA.



:behindsofa:
 
yeye ndo mwenye kuleta udini kwani tumeshuhudia dini yake ikiwaambia waumini wake kuwa kuliko kuchagua kafiri bora kula ya zao apigiwe lipumba, sasa huo udini nani anauleta? Hapohapo anamtumia membe kuwaletea watanzani mahakama ya kadhi wakati hilo si swala la kitaifa bali ni swala la dini ya kislamu,huyu mkwere hana jipya aende zake msonga akauze machungwa

Huu ni wakati muafaka wa kuelezana ukweli dini si kiini cha matatizo ya Taifa letu, tumeishi miaka yote bila kuwa mitafaruku ya kidini, usichukue maoni ya mitaani ya muislam ama mkristo mmoja kuyafanya ni maoni ya watu wote, mafisadi wanatumia dhana ya udini ili tupoteze muda kujadili dini, kitu kitakacholeta mfarakano Tanzania ni matabaka ya walioanacho na wasionacho, kimsingi watanzania inabidi tufungue macho, dini zetu zipo kwenye misingi ya amani na upendo tusikubali kulaghaiwa na kauli hizi za kidini, NJAA NDIYO ITAKAYOTUFANYA TUCHAPANE FIMBO dini inatumiwa kwa maslahi ya wachache, angalia Somalia wote ni waislamu mbona wanashindwa kupata amani ama Northern Ireland wote ni wakristo lakini amani hakuna. Haya matabaka walioanzisha kina Kikwete ndiyo yanayohatarisha amani yetu. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Inasemekana George Bush Jr alianzaisha vita ya Iraq ili kuongeza rating baada ya kuanguka sana. Kuna pia conspiracy theories kwamba September 11 ni kazi ya ndani iliyopangwa ili kuongeza umaarufu wa Bush. Kitu cha kuelewa ni kuwa wanasiasa will stop at nothing kuendelea kubaki madarakani. Hii ya udini nilishasema imeanzishwa na CCM baada ya kuona JK umaarufu umeshuka.

Kama ambavyo vita ya Iraq ilianza, tuwe macho kwani JK anaweza kutoa kafara waTZ ili kubaki madarakani. Aidha, anatumia udini ili ku-divert attention from the vote rigging scandal. TUSIDANGANYIKEEEEEEEEE.

Ningefurahi sana kama hao viongozi wa dini anaokutana nao wangemuuliza, hizo dalili ni zipi, nani kazianzisha lini na kwanini. Wampe Black and white kuwa ni CCM na yeye wanaowapeleka wananchi pabaya. Hii ni kwa kuwa hakuna chama kingine kinacholalamikia udini na kila chama kimejitahidi kuwahadharisha wananchi na udini ISIPOKUWA CCM ambao wanaendelea kupiga ngoma ya udini. Nani mkosaji???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom