Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Mkandara,
Thanks. Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kui spin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomb kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.
i) Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Ni kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa.Hata hivyo,baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:
i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari. ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724 = Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450(iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252 hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 ( Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445 = Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 ( iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137. Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
Hivyo basi kutokana na Dosari hiyo kubwa mgombea yeyote anayekubali kupokea matokeo atakuwa mwendawazimu. Ndiyo maana nikakataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo hayo.

2:Tarehe 15 November, katika Press Conference iliyofanyika Dodoma, Dr. Slaa, alikabidhi rasmi majukumu kwa Chama kwa kuwa kazi ya Mgombea Urais imefikia mwisho wake Baada ya Rais kutangazwa kwa mujibu wa Katiba (Mbovu) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa chombo ambacho kilikasimiwa madaraka na Kamati Kuu ya Chama ( Sekretariat) mbele ya Wabunge wa Chama. Chama kilipokea majukumu na kuelekeza utekelezaji na ufuatiliaji maazimio hayo ya kukataa matokeo na kumkataa Rais kufanyika kuanzia siku hiyo na Vyombo mbalimbali na ngazi mbalimbali za Chama, na Wabunge wa Chama. Hivyo kilichotokea Bungeni ni utekelezaji wa maamuzi ya Chama hadi pale ngazi za juu za Chama zitakapobariki au kubadilisha msimamo huo. Ni dhahiri basi, i) Wabunge wetu wala Dr. Slaa, hawakuhitaji kurudia madia ya msingi ikiwa ni pamoja na kurudia uchaguzi. Madai ya Mabadiliko ya Katiba au Katiba ya Wananchi na kudai Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kujiuzulu na Kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ni madai yaliyotolewa katika Press Conference ya Tarehe 15/11. Hata hivyo, msisitizo wa awali ni kwa kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi ambayo inaweza kutupelekea kwenye yote hayo. Mtu yeyote asiyemakini kufuatilia mtiririko huo anaweza kupotosha na kusababisha vurugu na uchochezi ambao Chadema, pamoja na jitihada zake za kudai haki zake na za wananchi waliochakachuliwa kura zao inapenda kufuata njia za kistaarabu na za amani. Ni vema yeyote anayetaka kufanya analysis ya hatua za Chadema kwanza akajielimisha vizuri badala ya kuweka hisia zake ( hakuna sababu ya kuandika na mate wakati wino upo), na wakati wowote Chadema tuko tayari kutoa ufafanuzi utakao hitajika, isipokuwa ule unaopaswa kupitia kwenye vyombo vyetu vya maamuzi kama chama cha kidemokrasia.

Eeeeeh Mwaka huu kazi ipo!..shukran Dr.Slaa tumekuelewa sana, lakini natatizwa kitu kimoja tu - Ujumbe huu hasa unamlenga nani? Yaani nani hasa anayeweza kuleta mabadiliko hayo...?
 
Huyu mkuu wa nchi amekemea udini baada ya uchaguzi lakini ukiangalia uteuzi wa wabunge watatu wa mwanzo tu umejaa udini mtupu. sasa sijui anafikiri watz ni vipofu au.
ukiangalia serikali yote ya Muungano kuanzia rais, makamu, rais wa zanzibar, makamu wake wote wawili. Sasa hapo hakuna udini kweli??
JK nafsi yake inamsuta.................kwa sababu ni mdini mno....Hebu muulizwe kwa nini amelifuta jina lake la Khalfani....na anajaribu kutumia vitisho vya udini ili tuogope kuhoji maamuzi yake mbalimbali ya kifedhuli.............kama ya kutuibia kura zetu.......................itafika mahali JK atadai kuhoji serikali inayoongozwa na muislamu ni udini, kumwonea wivu na chuki binafsi hata kama yeye na swahiba wake wa karibu wanafuja mali ya umma isivyo halali na kinyume cha sheria................................

Usishangae kuwa anafahamu wakristu karibu wote hatukumchagua na afikiri ni udini ili kufunika uwezo wake mdogo kiutawala............Hana hata shukrani ya kura zetu za 2005 alivyomroho wa madaraka.....

Kipimo cha udini wa JK kitakuwa mahakama za kadhi na nchi hii kujiunga na oic......................yakifanyika hayo basi mdini wetu ni JK hatuna mwingine....................
 
lets wait and see!!jinsi atavoshughulikia "ilo swala"alilolisema

Hawezi kushughulukia swala ambalo halipo hata kidogo. Huyu jamaa anataka kutupoteza kutoka kwenye uchakachuaji wa Matokeo.

Mtu anayejiita raisi wa TZ anasema nchi haitawaliki kama huu udini usiposhughulikiwa, inachekesha hii kabisa hata kwa mtoto mdogo ukimwambia kuna udini, JK aelewe kuwa kampeni zimeshakwisha tayari hivyo aache kutumia sera zake za maji taka alizokuwa anahubiri kwenye kampeni. Watanzania wengi hivi sasa wanaelewa si watu wa ndio mzee
 
Wangekuwa makini wasingepigia kura chaguo la Kikwete uwaziri mkuu, halafu hapo hapo wakasema hawamtambui Kikwete kama rais, hii ni point ya embarassment.

CCM tunawajua uozo wao, nasikitika kuona CHADEMA wanataka ku squander an opportunity to show the Tanzanian public a mature alternate party.

Naona mkuu unatatizo sana na kushiriki kwa CHADEMA katika kupiga kura kwa waziri mkuu. consistency ya CHADEMA ni kwamba protest yao imekuwa defined around Kikwete directly, siyo indirectly. nadhani haina maana kudeal na kikwete indirectly, maana hatimaye utaquestion kushiriki kwao bungeni anyway, maana kama wasemavyo wengine, Rais ana nafasi muhimu katika bunge, au wengine wanasema hata ukipitisha muswada inabidi utiwe saini na rais ili uwe upate nguvu ya kisheria. na mwisho unaweza hata kusema ardhi unayoishi inamilikiwa na Kikwete, rais, kwa mujibu wa sheria ya Tanzania sasa hivi. kwa hiyo ukimkataa labda uhame Tanzania! No, inabidi kudefine unachotaka kufanya na ukifanye kwa mujibu wa definition yako. that is what CHADEMA are doing, na binafsi naona wako sawa tu. Waziri mkuu ndio mkuu wa shughuli za serikali bungeni, na kwa kuwa wameamua kushiriki shughuli za bunge kikamilifu, haiingii akilini kupick issue na waziri mkuu. ila kushuhudia akiapishwa na Kikwete - No, lakini kufanya naye kazi bungeni - Yes. ni kujiwekea mipaka ili ufikishe ujumbe wako bila mwenyewe kujiwekea masharti yatakayokusumbua mwenyewe.

tahadhari: kuwa focused on Waziri mkuu inaweza kukufanya ukakosa big picture ya kile CHADEMA walichofanya jana, protest kwa Rais tena mbele ya "wadau wa maendeleo", na dignitaries wengine wengi tu, on live TV tena channel nyingi tu zinaonesha. inawezekana kwa watanzania wengi wasitambue umuhimu wake, lakini Kikwete anayetegemea sana fadhila za nje, ambaye amezoea kupata heshima kubwa, atakuwa ameumizwa sana na action ile.

mwisho, protest yoyote, however patchy, ina effect ya kuendeleza agenda ya uchaguzi, kitu ambacho CCM inataka hayo yasahauliwe, ili ifiche machafu yake
 
Asalaam aleykum,

Jana nilikuwa miongoni mwa mamilioni ya Watanzania tuliokuwa tukiangalia TV mida ya saa 10:30 jioni kuona mambo yanayojiri Bungeni.

Lengo la kuangalia ilikuwa si kusikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni, bali ni kushuhudia ni uamuzi gani ambao wabunge wa Chadema watachukua.

Kulikuwa na tetesi kuwa Wabunge wa Chadema hawatahudhuria Bungeni kama ambavyo hawakuhudhuria kwenye utangazaji wa matokeo ya uchaguzi wa Rais, uapishwaji wa Rais na kuapishwa kwa waziri mkuu.

Nilipata taarifa kuwa kulikuwa na jitihada kubwa zilizofanywa na Kikwete kuhakikisha kuwa wabunge wa Chadema watahudhuria hotuba yake Bungeni.

Jitihada hizi ni pamoja na Kikwete kutuma wajumbe kuongea na Chadema na kuwasihi wahudhurie hotuba ya Bungeni.

Wajumbe waliotumwa na Kikwete kuongea na Chadema ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa (ni ajabu lakini kweli) na Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye CCM wamepanga kumtumia ipasavyo kama rubber stamp baada ya kumfukuza kazi Samuel Sitta.

Pia zilifanyika jitihada za kuwaweka sawa baadhi ya wabunge wa Chadema ambao wako karibu na vigogo wa CCM ili kukwamisha mpango huu.

Naelewa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa ndani ya Chadema, huku baadhi ya wabunge pengine kwa mtazamo wao huru au kuwekwa sawa na vigogo wa CCM walipinga wazo la ku walk out.

Hivyo basi, ilipofika saa 10:30 jioni ambapo Kikwete aliingia Bungeni, nilipata hofu kubwa sana kuona kambi ya upinzani ya Chadema ikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge nikajua kuwa mafisadi wamefanikiwa kuwarubuni wamsikilize Kikwete.

Kikwete alisimama, akanywa fundo la maji na kutaka kuanza kuhutubia Bunge.

Ghafla, Freeman Mbowe, kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, akasimama na kuongoza kundi kubwa la wabunge wanaokaribia kufika 50 wa Chadema kuondoka Bungeni.

Hii ilimfanya Kikwete abaki kapigwa na butwaa na kushindwa kuhutubia kwa dakika kadhaa. Wabunge wa CCM wakazomea na wale wa CUF na wengineo wakabaki Bungeni kama tulivyotarajia.

Kwa kweli mwili ulinisisimka kutokana na kitendo cha kishujaa kilichofanywa na Wabunge wa Chadema kuonyesha kuwa hawakubaliani na matokeo yaliyompa Urais Kikwete kwa kutumia wizi mkubwa wa kura ulio bayana.

Kitendo kile kilikuwa na impact kubwa sana na kilimuaibisha Kikwete mbele ya Watanzania na mabalozi wa nchi za nje waliokuwepo Bungeni. Na ni sahihi kabisa kwani amepata Urais kwa njia za kidhalimu.

Kwa faida ya wasiojua the political significance ya Wabunge wa Chadema kutoka nje wakati Rais anaanza kuhutubia, naomba wasome yafuatayo kutoka kwenye mtandano:

A Bunge walkout is the act of MPs collectively leaving Parliament as an act of protest.

A walkout can also mean the act of leaving a place of work, school, a meeting, a company, or an organization, especially if meant as an expression of protest or disapproval.

A walkout can be seen as different from a strike in that a walkout can occur spontaneously, and need not necessarily involve all the workers present, whereas a strike is often voted on beforehand by the workers, giving notification both to all of the workers and to the company affected.

Walkouts have often been staged against the presence of a speaker (muongeaji in this case Kikwete) or the content of an in-progress speech at a meeting.

The protest, which is often a silent, non-violent means of expressing disapproval, is often interpreted as an exercise of the freedom of association while allowing the speaker (mtoa hotuba) to exercise the freedom of speech, albeit with a reduced audience in attendance.
 
Ni nia ya dhati dhidi ya rais wa NEC na vyombo vya serikali. AIBU.
 
Itukuzwe Chadema milele...message SENT and DELIVERED.
 
Sasa tuendelee kuelimisha wenzetu kama tulivyofanya kabla uchaguzi lengo na maana hasa ya haya CHADEMA wanayoyafanya. hakuna kukata tamaa wala kurudi nyuma, endelea kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki na hii mijadala isife kwani 2015 sio mbali!

mapambano bado yanaendelea....
 
mbona unalenga mbali sana? 2015. kazi inaze kwa ajili ya wakati tulinao sasa.
 
mimi nashangaa huo udini anaousema rais kikwete unatoka wapi! huku mtaani waislamu na wakristu tunaishi kwa amani sana lakini mahubiri haya ambayo yamekua yakitolewa mara kwa mara na rais kikwetwe yameanza kutuvuruga na kuanza kuchukiana tukiamini kweli kuna udini. Ukweli ni kwamba mhubiri mkuu wa sera ya udini tangu kipindi cha kampeni hadi sasa ni rais kikwete na baadhi ya wafuasi wake ndani ya chama cha mapinduzi- CCM na kama ataachwa kuendeleakuhubiri kauli hizi za udini bila kukemewa eti kisa yeye ni mkuu wa nchi basi ataipeleka nchi hii pabaya. nawaomba viongozi wa dini zote mkae na muheshimiwa rais na kwa kauli moja mumkemee rais pamoja na baadhi ya wana ccm aache mara moja kuzungumza majukwaani habari za kuwepo kwa nyufa za kidini kitu ambacho hakina ukweli wowote zaidi kuzidi kupandikiza mbegu za udini. chonde chonde rais kikwete nakuomba uliepushe taifa hili na hatari ambayo unajaribu kuipandikiza dhidi ya kauli zako za udini. sisi huku mtaani hatujui kama kuna udini au nyufa za kidini.
 
Aksante saana kwa ufafanuzi ulio makini nadhani wapambe wasiotaka mabadiliko wataelewa.

Asiye jua maana safari hii aambiwe maana. Ujumbe Umefika Mkuu.
 
Sasa tuendelee kuelimisha wenzetu kama tulivyofanya kabla uchaguzi lengo na maana hasa ya haya CHADEMA wanayoyafanya. hakuna kukata tamaa wala kurudi nyuma, endelea kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki na hii mijadala isife kwani 2015 sio mbali!

mapambano bado yanaendelea....

Naaaaaaaam hapo umeongea jambo muhimu mkuu ni kuwapa elimu hawa ndugu zetu ambao wanaangalia lakini hawaoni...
 
Mashujaa ndivyo wafanyavyo. Hongera CHADEMA kwa kuonesha ushujaa wa kusimamia kile mnachoamini.

We are behind you for the best of this country and its next generations
 
Jamani,hivi udini ambao mr. prezzo ametangaza mbele ya bunge kwamba tz imeanza kugawanyika kwa udini, upo wapi uo udini? ktk uchaguzi udini ulikuwa wapi?, si angemention tu kama kidonda kipo kipone?...kwasababu hatujaona watu wakimchagua mtu kwa udini wake, bali kwa sera, hasa ukichukulia vijana wengi wakristo kwa waislam walimpigia Dr.slaa au Lipumba. udini uko wapi? ange mention chama basi tujue.

kwasababu kama ni udini, ccm haina balance kabisa ya dini, basi ccm ndo alikuwa anaiongelea kuwa ni ya kidini. pili, uteuzi wa wabunge wale wa mwanzo wote walilalia upande wa dini moja, kuanzia zakia mehgi ambaye wananchi hawampendi lakini kikwete anampenda. wale wawili za zenji pia mtu mwingine angefikiri kuwa ni udini, lakini hakuna mkristo hata mmoja aliyelalamika kuhusu udini, kwasababu tz hatujali sana udini kwenye selikali.

angalia, mbona rais, makamu wa rais mara zote mbili ni wa dini moja, lakini hilo haliko mioyoni mwa watu, udini ni tatizo kweli hapa tz kiasi cha president kulitangaza mbele ya bunge?

Nijuavyo mimi, yaliyomjaa mtu moyoni ndiyo atakayoyaongea. kama mtu ni mdini, ataongea sana udini tu. pia, wakati mwingine, hata kama wananchi hawakuwa wadini, sasa kwasababu mr.president amelitangaza, atawa alart wananchi waanze kuwa wadini. hivi mr. president anajipanga kwanza kabla ya kuongea hotuba kweli au anazima moto?

Zanzibar ni lini hata siku moja Mkristo alishawahi kushika madaraka, kwani zenji hakuna wakristo? lakini sisi wakristo hatulalamiki...NITAJIENI KIONGOZI YOYOTE HATA WAZIRI TU WA KIKRISTO AMBAYE ALISHAWAI KUPEWA MADARAKA ZANZIBAR. ukinitajia nakupa laki hapahapa...hayupo
 
Kiduchu chadema na viongozi wa ukweli.Mungu awape roho ya ukakamavu.
 
thanx kaka udini anao huyo mkwere viongozi wote wa juu ni waislam kasoro pinda tu,ona kateua wabunge 3 wote waislam nani anaudini hapo?anataka kuwapotosha wananchi waanze kuichukia chadema kumbe manafiki tu
 
Jamani,hivi udini ambao mr. prezzo ametangaza mbele ya bunge kwamba tz imeanza kugawanyika kwa udini, upo wapi uo udini? ktk uchaguzi udini ulikuwa wapi?, si angemention tu kama kidonda kipo kipone?...kwasababu hatujaona watu wakimchagua mtu kwa udini wake, bali kwa sera, hasa ukichukulia vijana wengi wakristo kwa waislam walimpigia Dr.slaa au Lipumba. udini uko wapi? ange mention chama basi tujue.

kwasababu kama ni udini, ccm haina balance kabisa ya dini, basi ccm ndo alikuwa anaiongelea kuwa ni ya kidini. pili, uteuzi wa wabunge wale wa mwanzo wote walilalia upande wa dini moja, kuanzia zakia mehgi ambaye wananchi hawampendi lakini kikwete anampenda. wale wawili za zenji pia mtu mwingine angefikiri kuwa ni udini, lakini hakuna mkristo hata mmoja aliyelalamika kuhusu udini, kwasababu tz hatujali sana udini kwenye selikali.

angalia, mbona rais, makamu wa rais mara zote mbili ni wa dini moja, lakini hilo haliko mioyoni mwa watu, udini ni tatizo kweli hapa tz kiasi cha president kulitangaza mbele ya bunge?

Nijuavyo mimi, yaliyomjaa mtu moyoni ndiyo atakayoyaongea. kama mtu ni mdini, ataongea sana udini tu. pia, wakati mwingine, hata kama wananchi hawakuwa wadini, sasa kwasababu mr.president amelitangaza, atawa alart wananchi waanze kuwa wadini. hivi mr. president anajipanga kwanza kabla ya kuongea hotuba kweli au anazima moto?

Zanzibar ni lini hata siku moja Mkristo alishawahi kushika madaraka, kwani zenji hakuna wakristo? lakini sisi wakristo hatulalamiki...NITAJIENI KIONGOZI YOYOTE HATA WAZIRI TU WA KIKRISTO AMBAYE ALISHAWAI KUPEWA MADARAKA ZANZIBAR. ukinitajia nakupa laki hapahapa...hayupo

ofcourse uko sahihi,tangu uhuru amepatikana waziri mmoja tu anaitwa adam mwakanjuki,naumba laki moja yangu kwanza
 
duh iyo laki itatoka kweli..hivi kweli jamani, kumbe zanzibar kuna wakristo pia, lakini tangu miaka yote huwa sioni wanashirikishwa kwa jambo lolote, kwanini upande huu mmoja wa ccm kunakuwa na ubaguzi wa kidini uliokithiri kiasi hiki? KWANINI ZANZIBAR KUNA UDINI SANA..ubaguzi wa dini?
 
Asalaam aleykum,

Jana nilikuwa miongoni mwa mamilioni ya Watanzania tuliokuwa tukiangalia TV mida ya saa 10:30 jioni kuona mambo yanayojiri Bungeni.

Lengo la kuangalia ilikuwa si kusikiliza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Bungeni, bali ni kushuhudia ni uamuzi gani ambao wabunge wa Chadema watachukua.

Kulikuwa na tetesi kuwa Wabunge wa Chadema hawatahudhuria Bungeni kama ambavyo hawakuhudhuria kwenye utangazaji wa matokeo ya uchaguzi wa Rais, uapishwaji wa Rais na kuapishwa kwa waziri mkuu.

Nilipata taarifa kuwa kulikuwa na jitihada kubwa zilizofanywa na Kikwete kuhakikisha kuwa wabunge wa Chadema watahudhuria hotuba yake Bungeni.

Jitihada hizi ni pamoja na Kikwete kutuma wajumbe kuongea na Chadema na kuwasihi wahudhurie hotuba ya Bungeni.

Wajumbe waliotumwa na Kikwete kuongea na Chadema ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru kutokana na kashfa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa (ni ajabu lakini kweli) na Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambaye CCM wamepanga kumtumia ipasavyo kama rubber stamp baada ya kumfukuza kazi Samuel Sitta.

Pia zilifanyika jitihada za kuwaweka sawa baadhi ya wabunge wa Chadema ambao wako karibu na vigogo wa CCM ili kukwamisha mpango huu.

Naelewa kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa ndani ya Chadema, huku baadhi ya wabunge pengine kwa mtazamo wao huru au kuwekwa sawa na vigogo wa CCM walipinga wazo la ku walk out.

Hivyo basi, ilipofika saa 10:30 jioni ambapo Kikwete aliingia Bungeni, nilipata hofu kubwa sana kuona kambi ya upinzani ya Chadema ikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge nikajua kuwa mafisadi wamefanikiwa kuwarubuni wamsikilize Kikwete.

Kikwete alisimama, akanywa fundo la maji na kutaka kuanza kuhutubia Bunge.

Ghafla, Freeman Mbowe, kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, akasimama na kuongoza kundi kubwa la wabunge wanaokaribia kufika 50 wa Chadema kuondoka Bungeni.

Hii ilimfanya Kikwete abaki kapigwa na butwaa na kushindwa kuhutubia kwa dakika kadhaa. Wabunge wa CCM wakazomea na wale wa CUF na wengineo wakabaki Bungeni kama tulivyotarajia.

Kwa kweli mwili ulinisisimka kutokana na kitendo cha kishujaa kilichofanywa na Wabunge wa Chadema kuonyesha kuwa hawakubaliani na matokeo yaliyompa Urais Kikwete kwa kutumia wizi mkubwa wa kura ulio bayana.

Kitendo kile kilikuwa na impact kubwa sana na kilimuaibisha Kikwete mbele ya Watanzania na mabalozi wa nchi za nje waliokuwepo Bungeni. Na ni sahihi kabisa kwani amepata Urais kwa njia za kidhalimu.

Kwa faida ya wasiojua the political significance ya Wabunge wa Chadema kutoka nje wakati Rais anaanza kuhutubia, naomba wasome yafuatayo kutoka kwenye mtandano:

A Bunge walkout is the act of MPs collectively leaving Parliament as an act of protest.

A walkout can also mean the act of leaving a place of work, school, a meeting, a company, or an organization, especially if meant as an expression of protest or disapproval.

A walkout can be seen as different from a strike in that a walkout can occur spontaneously, and need not necessarily involve all the workers present, whereas a strike is often voted on beforehand by the workers, giving notification both to all of the workers and to the company affected.

Walkouts have often been staged against the presence of a speaker (muongeaji in this case Kikwete) or the content of an in-progress speech at a meeting.

The protest, which is often a silent, non-violent means of expressing disapproval, is often interpreted as an exercise of the freedom of association while allowing the speaker (mtoa hotuba) to exercise the freedom of speech, albeit with a reduced audience in attendance.

Sioni kama ilikuwa ni ushujaa wowote kwa sababu waliondoka ukumbi wa bunge na wakenda ukumbi mwingine kumwangalia kupitia luninga-Is a kindly shameful too!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom