Mkuu,
Umechambua vizuri mada yako.
Kuna msemo huu ,"ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji".
Kwa bahati mbaya watu wengi wakati CUF wanaitwa magaidi, watarudisha usultani na kuisilimisha nchi..tulikaa kimya au hatukuona hatari ambayo CCM wanatuletea kidogo kidogo ya kuigawa jamii ya Tz kwa misingi ya kidini.
CCM wanatumia karata hii kwa chama chochote kinachoinukia kuwa mwiba kwa CCM. Vizuri tunaanza kulijua hili na mategemeo yangu ni kuwa hata Hapa JF wale wapenzi wa malumbano ya dini, wale wanaobeza dini au dhehebu ya wengine,wale wanajaribu kudhalilisha dini za wengine wataona mtego huu wa CCM na kuacha chuki za kidini au kuchochea malumbano ya kidini yanayogawa jamii.
Kuna thread nyingi humu JF zinajaribu kuwachafua waislamu na uislamu. sisi tunaoleta hizi threads au kufanya haya hatuoni kuwa tunameza ndoana ya CCM bila ya kujua ,au tunafanya kwa makusudi? Kwa faida ya nani? au kwa faida gani?
Pia huona wale wanaochangia threads hizo wanapo-defend kundi lao na uislam wao nao hujaribu ku-hit hard.basi hatujifunzi kutokana na wachangiaji wa hizo threads kwa wale wanaokandia na wale wanaohami makundi yao kuwa hali hii inatupelekea huko ambako CCM wanatuelekeza?
Wakuu, tuifahamu hii hali na tuikatae. tubaki na dini zetu kwa wale wenye dini bila kubughudhi wa dini nyengine na tuungane katika kushughulikia mambo yanayotuumiza kama Taifa, ambayo ni mengi.