Ni nani aliyewahi kuuelewa muziki wa Michael Jackson?

Ni nani aliyewahi kuuelewa muziki wa Michael Jackson?

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Za jioni ndugu zangu, kwema?

Michael Jackson enzi za uhai wake alikuwa msanii maarufu na tajiri kuliko msanii yeyote hapa duniani.

Lakini pamoja na hizo sifa mbili kubwa nilizozitaja, kwangu mimi naona kuwa jamaa alibebwa na nyota tu kama ilivyo kwa Diamond, ila kiuimbaji au utungaji jamaa hakuwa anatunga au kuimba nyimbo zozote za maana.

Em fikiria Michael Jackson alikuwa na uwezo gani wa kutunga nyimbo nzuri na za maana kushinda wasanii kama Lionel Richie, Steven Wonder, Phil Collins, au mademu kama vile Whitney Houston, Celine Dion, Shania Twain nk.

Labda aliwashinda kwenye kucheza kama vile kusimamia kucha, kuteleza sakafuni, mabreka nk. Lakini kwenye tungo iwe za mapenzi, kijamii nk Michael alikuwa mweupe tu kama ilivyo kwa Diamond kuonekana anajua na kupata umaarufu wa ndani na nje zaidi ya wakongwe wa mziki kama vile kina Nature, Afande Sele, Kiba, Barnaba na wakongwe wengine mbali mbali.

Sijajua hili linatokana na nyota kweli au kuna namna tu media zinaamua kukubeba kwa lengo fulani.

Kwa kweli mpaka sasa sijauelewa mziki au wimbo uliomfanya Michael Jackson apendwe na kuitwa mfalme. Mwenye uelewa zaidi wa nyimbo zake aje atuambie.

1674152734530.jpeg
 
1. Jamaa ana sauti ambayo kwa kizazi cha sasa ni ngumu kuipata.

2. Anamiliki jukwaa hasa, kama kuna mtu umewahi kumuona anamiliki jukwaa vizuri ktk show, basi elewa hajafika nusu ya michael jackson.

3. Alianza kutoa video dongo zenye kuvutia toka miaka 80 na 90 na mwanzoni mwa 2000. Katafute video zake uone.

Mwisho kabisa, alikuwa na spiritual power nyuma yake, alitengenezwa kuzimuni awe vile alivyokuwa, so sio rahisi mtu kushindana nae. Alianza kutumikia masonic toka akiwa kijana mdogo, alisambaza ishu za kubadili rangi ulimwengu mzima, akaja watoto wa kupandikiza, akaja ishu ya kubadili jinsia.

Mambo yote mazito ya kipepo walianza kumtumia yeye kuwa kama mjumbe wake. Achana na zile ngonjera sijui alibadili dini, zote zile bado alikuwa ktk mission ya masonic.

Apumzike huko anakostahili kupumzishwa.
 
"We Are the World"

"I Just Can't Stop Loving You

"Bad"

"Say Say Say"

You are not alone

Heal the World

Real?????unasema MJ hajui kuandika unajua hizo nyimbo??
Hiyo ya mwisho tu Heal the world ni nyimbo nzuri sana MJ anasema

There's a place in your heart
And I know that it is love
And this place it was brighter than tomorrow
And if you really try
You'll find there's no need to cry
In this place you'll feel there's no hurt or sorrow

There are ways to get there
If you care enough for the living
Make a little space
Make a better place
 
Nakupenda Pia..., Nakutaka Pia Mpenzi We.........

Kuna wakati unaweza kuongelea Fani fulani ukajionesha ni vipi hujui hio Fani..., let alone mapenzi ya Kitu ila ulichosema hapo kinaonyesha ni vipi sio mfuatiliaji.....

Unaongelea mtu mwenye vibao zaidi ya 100; career ya tangia ana miaka 5 kwamba haeleweki?!!! Labda wewe ndio huelewi muziki....

American singer and songwriter Michael Jackson recorded songs for ten studio albums, two posthumous studio albums, seventy two compilation albums, three soundtrack albums, one live album and seven remix albums. He has provided background vocals for songs recorded by other artists, as well as featured on duets.

Jackson debuted on the professional music scene at age five as a member of The Jackson 5. The group set a chart record when its first four singles—
 
Back
Top Bottom