Nianze Kwa kusema “kwa kuwa uliamini hivyo ndiyo Maana hujapata, umechelewa sana kupata au hujapata Ile Ajira unayoihitaji”.
Hapa kwanza tuliza akili ili uweze kupokea kitu, hasa vijana. Napenda utambue kuwa nilikuwa kama wewe.
Ajira zipo nyingi Sana, zinatoka na kutangazwa Kila dakika kutoka serikalini na Kampuni binafsi. Kitendo cha wewe kuamini kuwa hakuna ajira huwezi kuziona au kuamini kuwa unahitaji Refa ili kupata huwezi kuomba Kwa umakini na kwa utaalamu unaohitajika. Ubongo ni kiungo cha ajabu sana na kinachoongoza maisha yote ya binadamu. Ubongo ukifa mwanadamu naye amekufa.
Maisha na mambo tunayofanya yanaongozwa na ubongo. Utendaji wa mwili na Maisha Kwa ujumla hutegemea taarifa zinazotoka kwenye ubongo. Ubongo ukipokea taarifa na kuikubali kuwa kweli utaamrisha mwili kutenda kutokana na taarifa husika. Mfano ukiamini kuwa kupata kazi ni hadi Refa hata ukiomba kazi utaomba ilimradi tuu maana unajua hutapata, unaweza kuambiwa andika barua ya maombi wewe ukachukua barua ya mtu mwingine ukabadili tuu taarifa za anwani na majina, hutaki hata kujieleza ubora wako juu ya hiyo kazi kwenye barua Kwa kuwa unaona ya kazi gani unapoteza muda tuu kazi yenyewe hupati.
Kwanini hupati kazi na kazi zipo nyingi?
(i) Umeamini kuwa kazi hakuna na zilizopo lazima uunganishiwe na refa; Ndugu yangu huu ni ukuta wako. Ukuta huu umeziba kazi unazozitaka usizione na usizipate, Ubongo wako unafanya kazi hadi kwenye huu ukuta hauvuki. huombi Kwa akili tulivu hivyo hupati.
(ii) Huangalii Barua Pepe (email) yako Kila siku;
Majibu mengi ya maombi ya kazi katika miaka hii hutumwa Kwa kutumia barua pepe, kama wewe si mtu wa fufungua barua Pepe Kila siku huenda unapishana na majibu ya kazi au mwaliko wa usahili
(iii) Huangalii ukaisoma, ukaielewa na kuiboresha CV (chapisho la wasifu) yako ; wengi tunapenda urahisi Sana na hii ni kutokana na kuamini kuwa unaomba tuu Ila hutapata basi unachukua CV ya Mtu mwingine unaichapisha kwako kama ilivyo, unabadili tuu namba na jina. Nina rafiki nilimpa CV yangu akatumia kuomba kazi, akafanyiwa usahili wa simu akaulizwa kilichoandikwa hata hajui. Akakosa kazi mara mbili, maana Aliniambia nimwandikie CV ye kazi yake kutuma maombi tuu.
(iv) Kutokujiamini katika usahili; Hii inatokana na wewe kuamini kuwa huwezi kupata hiyo kazi bila refa Kwa hiyo unajieleza Kwa woga katika chumba cha usahili hivyo unapoteza nafasi yako ya ubora.
(v) Kutokutuma maombi Kwa wingi; Kwa kuwa umeaminishwa kuwa hakuna kazi basi umekuwa mvivu wa kutuma maombi ya kazi, kazi zipo ishirini unatuma kampuni moja tuu umechoka unaacha, kwanini? Kwa sababu unaona kuwa unapoteza muda kumbe hiyo pia ni sehemu ya kazi yenyewe, inatakiwa ifanywe Kwa umakini na upendo.
Ufanye nini basi ili upate kazi ya ndoto zako?
(i) Amini kuwa kazi zipo nyingi na zinatoka Kila muda ; Badili mtazamo wako katika Jambo hasi kuhusu ajira uliloambiwa muda mrefu ambalo limepelekea hali unayoiona. Hutapungukiwa kitu we Achilia tuu huo mtazamo.
(ii) Fungua account ya kitaaluma katika mtandao wa kitaaluma wa LinkedIn na kisha uweke taarifa zako zote za kitaaluma na kiutendaji; Huku kazi zinatoka Kila dakika na nyingine hazihitaji hata barua kuomba ni hapo hapo kama unatumia Instagram Yani. Jitahidi uwe unaingia na kuangalia kwenye sehemu ya kazi angalao Kila baada ya masaa ma manne, Mimi huwa naangalia Kila nikikumbuka. hata taarifa za usahili unatumiwa huku huku kwenye meseji mda mwingine.
(iii) Tengeneza CV (Wasifu wako katika maandishi) yako Kwa kuangalia za watu wengine na kisha iboreshe kila mara kulingana na asili na vigezo vya kazi unayoiomba; Hii itakusaidia wewe kujifahamu na kufahamu kuhusu kazi unayoiomba na utakua na majibu mazuri ya kitaalamu muda unafanyiwa usahili.
(iv) Weka mawasiliano yanayopatikana muda wote katika CV, barua yako au sehemu yoyote Ile unayotakiwa kuandika mawasiliano yako iwe namba ya simu, anwani au barua pepe; Hii itasababisha kampuni husika kukupata Kwa urahisi wakikuhitaji Kwa usahili au ajira ya moja Kwa moja.
(v) Tuma maombi Kila mara ukiona kazi inayokufaa; Hii itakuongezea wewe nafasi nzuri ya kuitwa katika usahili na nafasi nzuri ya kupata kazi na kuzoea usahili.
Natumai ya kuwa mmenielewa, niwakumbushe tena mwili unatenda kutokana na taarifa unazozipokea na kuzikubali katika ubongo wako. Angalia Kwa makini taarifa hizo, kama hazikusaidii zinafanya kazi kingine na wewe Acha kabisa.Hata Vitabu vya Mungu vinatufundisha juu ya Imani, ndivyo na saikolojia inavyofanya kazi.
Asante sana Kwa kusoma nakala hii.

Upvote
9