Ni nani anahujumu IP Address za Tanzania?

Uliunganisha computer yako na Wifi wakati ukifanya malipo ?
 
Usiwachukulie poa wabongo, Kuna huu ujinga pia nauona sana Telegram course za corsera na Udemy za bei kubwa unakuta unawapa Elfu 30, wanakuungia package ya mwaka ambayo unakuta ni karibu dollar 120.

Bado Playstore sijui hua wanatoa wapi card za kulipia vijitu vijitu vingi vya online ambavyo ungekua ni hela zao halisi wasi gekua wanalipia.
Hizo courses kwenye hizo platforms mbina zipo tu mkuu? Ni wewe na muda wako.
 
Nimelipia online service moja lakini cha ajabu malipo yamekataliwa na kuambiwa kua IP Address niliotumia kufanya malipo iko katika range ya IP ambazo ziko black listed, na Tanzania iko blacklisted kutokana na constant abusive behaviour mtandaoni.

najiuliza, watanzania hawa hawa wanaokesha Tiktok na insta? Je ni ISP ndio wanachukua low quality IP?View attachment 3188546
Wakati mwingine ni mambo ya fundi mitambo tu pale Pugu road, redio Tanzania dar es salaam. I mean matatizo ya kiufundi na kiusalama inayoweza kusababishwa na mambo kadha wa kadha. Imawezekana Kampuni inayotoa huduma hizo imewekea vikwazo IPs fulan zinazotokea huko sababu ya udanganyifu au uarifu mwingine wa mitandaoni. Siyo kosa lako moja kwa moja, bali ni policies zao zinawaagiza kuchukua hatua hizo wanapo suspect.

Fanya yafuatayo;

1. Wasiliana na customer care

2. VPN inaweza kusaidia kubadili IP yako na kufanya ionekane kama unatoka nchi nyingine isiyokuwa kwenye orodha ya "blacklisted."

3. Tumia "IP Blacklist Checker" ili kuona kama IP yako n miongoni mwa the "blacklisted." kama ndiyo, wasiliana na ISP wako ili kusaidia kuibadilisha IP au kuondoa kwenye list hiyo.

4. Kama inawezekana, jaribu kutumia kadi ya malipo, PayPal, au njia nyingine za malipo zisizohusisha IP yako.

5. Ongea na ISP ili kama tatizo ni IP ya ISP wako, basi akusaidie kubadilisha.
 
Samahani naomba kujuzwa VPN ni nini na IP ni nini,na zinafanyaje kazi?
VPN (Virtual Private Network) na IP (Internet Protocol) ni teknolojia mbili zinazohusiana na mtandao wa intaneti, lakini zina kazi tofauti. Hapa kuna maelezo ya kila moja na jinsi zinavyofanya kazi:

VPN (Virtual Private Network)
VPN ni teknolojia inayotumika kuunda muunganisho salama kati ya kifaa chako (kama simu, kompyuta) na mtandao wa intaneti.

Inavyofanya kazi:
1. Encryption (Usimbaji fiche): VPN huficha (encrypt) data zako unapotumia mtandao, ili mtu yeyote asiyeruhusiwa (kama wavamizi wa mitandao au watoa huduma ya intaneti) asiweze kuona unachofanya mtandaoni.

2. Kuficha IP yako: Inapounganishwa, VPN huficha anwani yako halisi ya IP na kukupa IP ya seva ya VPN. Hii hufanya ionekane kama unatumia intaneti kutoka eneo tofauti.

3. Faida za VPN:

•Kulinda faragha yako mtandaoni.

•Kufikia maudhui yaliyozuiwa kijiografia (geo-restricted content).

•Kulinda data zako unapounganishwa kwenye mitandao ya umma kama Wi-Fi ya bure.

Mfano:
Ukijiunganisha kwenye VPN yenye seva nchini Uingereza, maombi yako ya mtandao yataonekana kama yanatoka Uingereza, hata kama upo Tanzania.

IP (Internet Protocol)
IP ni anwani ya kipekee inayotambulisha kifaa chako kwenye mtandao wa intaneti. Ni kama anwani ya posta ambayo inaruhusu data kupelekwa na kupokelewa kati ya vifaa tofauti mtandaoni.

Aina za IP:
1. IP ya Umma (Public IP): Hii ni anwani inayotolewa na mtoa huduma wa intaneti (ISP) na hutumika kutambulisha kifaa chako kwa ulimwengu wa intaneti.

2. IP ya Ndani (Private IP): Hii ni anwani inayotolewa kwa vifaa vilivyoko ndani ya mtandao wa ndani (kama nyumbani au kazini).

Inavyofanya kazi:
Unapofungua tovuti, kifaa chako hutuma ombi kwa seva ya tovuti hiyo kwa kutumia IP yako.

Seva hiyo hutuma data ya tovuti hiyo kwa kifaa chako kupitia IP hiyo hiyo.

Mfano:
Unapofungua Google, ombi la kufungua tovuti linaenda na anwani yako ya IP, na Google hutuma majibu kupitia IP yako.

VPN inakusaidia kuficha au kubadilisha IP yako, hivyo kulinda faragha yako, Yaani kifaa chako hakitambuliki kwa ile mitandao.itayofungiwa.

IP ni kitambulisho kinachotumiwa kuwasiliana mtandaoni.
 
Nimelipia online service moja lakini cha ajabu malipo yamekataliwa na kuambiwa kua IP Address niliotumia kufanya malipo iko katika range ya IP ambazo ziko black listed, na Tanzania iko blacklisted kutokana na constant abusive behaviour mtandaoni.

najiuliza, watanzania hawa hawa wanaokesha Tiktok na insta? Je ni ISP ndio wanachukua low quality IP?View attachment 3188546
Hapa hakuna nilichoambulia.. Bora ishu za Lissu..

...Ni Hayo Tu!!!
 
VPN (Virtual Private Network) na IP (Internet Protocol) ni teknolojia mbili zinazohusiana na mtandao wa intaneti, lakini zina kazi tofauti. Hapa kuna maelezo ya kila moja na jinsi zinavyofanya kazi:

VPN (Virtual Private Network)
VPN ni teknolojia inayotumika kuunda muunganisho salama kati ya kifaa chako (kama simu, kompyuta) na mtandao wa intaneti.

Inavyofanya kazi:
1. Encryption (Usimbaji fiche): VPN huficha (encrypt) data zako unapotumia mtandao, ili mtu yeyote asiyeruhusiwa (kama wavamizi wa mitandao au watoa huduma ya intaneti) asiweze kuona unachofanya mtandaoni.

2. Kuficha IP yako: Inapounganishwa, VPN huficha anwani yako halisi ya IP na kukupa IP ya seva ya VPN. Hii hufanya ionekane kama unatumia intaneti kutoka eneo tofauti.

3. Faida za VPN:

•Kulinda faragha yako mtandaoni.

•Kufikia maudhui yaliyozuiwa kijiografia (geo-restricted content).

•Kulinda data zako unapounganishwa kwenye mitandao ya umma kama Wi-Fi ya bure.

Mfano:
Ukijiunganisha kwenye VPN yenye seva nchini Uingereza, maombi yako ya mtandao yataonekana kama yanatoka Uingereza, hata kama upo Tanzania.

IP (Internet Protocol)
IP ni anwani ya kipekee inayotambulisha kifaa chako kwenye mtandao wa intaneti. Ni kama anwani ya posta ambayo inaruhusu data kupelekwa na kupokelewa kati ya vifaa tofauti mtandaoni.

Aina za IP:
1. IP ya Umma (Public IP): Hii ni anwani inayotolewa na mtoa huduma wa intaneti (ISP) na hutumika kutambulisha kifaa chako kwa ulimwengu wa intaneti.

2. IP ya Ndani (Private IP): Hii ni anwani inayotolewa kwa vifaa vilivyoko ndani ya mtandao wa ndani (kama nyumbani au kazini).

Inavyofanya kazi:
Unapofungua tovuti, kifaa chako hutuma ombi kwa seva ya tovuti hiyo kwa kutumia IP yako.

Seva hiyo hutuma data ya tovuti hiyo kwa kifaa chako kupitia IP hiyo hiyo.

Mfano:
Unapofungua Google, ombi la kufungua tovuti linaenda na anwani yako ya IP, na Google hutuma majibu kupitia IP yako.

VPN inakusaidia kuficha au kubadilisha IP yako, hivyo kulinda faragha yako, Yaani kifaa chako hakitambuliki kwa ile mitandao.itayofungiwa.

IP ni kitambulisho kinachotumiwa kuwasiliana mtandaoni.
Asante sana mkuu, ubarikiwe.
 
Back
Top Bottom