Ni nani anapaswa kujitathimini Kati ya Jeshi la Polisi na Chama cha Mapinduzi?

Wote ni magaidi tu kwetu
 
Kwanini anaendeshwa na wakati ni mtu mzima?
Ndivyo ilivyo historia ya viongozi wetu wa polisi na Ccm. Mahita alimkung'uta sana mabomu Mrema akapata uaijipii,ile dhambi ikamuingia,akaendelea kuwakung'uta watu misikitini,akaua watu Zanzibar na wengine kukimbia nchi,ccm wakishangilia na kumpongeza aijipii kwa kazi nzuri. Leo hii Mahita amebaki peke yake,ccm wamemkana utadhani hawakuhusika kwenye maamuzi.
Mbunge wa Ccm anamfokea Rpc,mbunge anaamrisha rpc ahamishwe lakini mwenyekiti wa ccm hamkemei mtu wake unataka Siro afanyaje?
Nyumba haijichafui bali huchafuliwa na mwenye nyumba.
Rais aliruhusu rushwa ya kubrashia viatu kwa polisi hadharani,tuwalaumu polisi kwa rushwa?
 
Bila ccm ya hovyo huwezi kupata jeshi la polisi la hovyo. Jeshi la polisi linalofundishwa namma ya kutesa watu kisa si Wana ccm haliwezi kuwa bora.

Inashangaza mtu anayemshupalia Sirro ambaye ni kiroboto tu km alivyokuwa polepole na kushindwa kutambua uozo wa polisi ni mimba walioitunga ccm na serikali Yao. Ccm hawapaswi kukwepa lawama na uovu wote wa jeshi la polisi, wamelitumia na wataendelea kulitumia kama qondom Ili kunufaika katika utawala wao.
 
Wote.

Polisi watimize majukumu yao kulingana na maadili ya kazi zao wakiweka usawa kwa raia wote wa Tanzania bila kujali itikadi zao.

CCM wakumbuke wao ni chama cha siasa, waachane na kujiita chama dola, hilo jina linawaharibu akili mwishowe wanashindwa kutambua haki za raia wa Tanzania kwa kuweka mbele maslahi ya chama chao zaidi ya mengine yote.
 
CCM ndiyo inapaswa ijitathmini. Kwa nini imeigeuza polisi kuwa idara yake ya unyanyasaji wa raia?
 
Umeongea point Sana, niliwaeleza baadhi ya watu kuwa haya yanayotokea sasa yametokea sana kipindi Cha IGP wengine huko akina mahita, mangu,mwema n.k
Tatizo sio IGP, bado haya yataendelea kuwepo mpaka CCM watapoamua la kufanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…