Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Ni nani anastahili kuwa MwanaJamiiForums bora wa mwaka?

Nani Mwana JamiiForums bora wa mwaka kati ya hawa?

  • The Boss

  • Faiza Foxy

  • Mzee Mwanakijiji

  • BAK

  • Pasco

  • Heaven Sent

  • Victorie

  • Technically

  • Mshana Jr

  • Lizaboni


Results are only viewable after voting.
Habari zenu wakubwa,

Matumaini yetu ni kuwa nyote ni wazima wa afya na mnaendelea vema na shughuli zenu ili kuepuka kusoma namba.

Malengo ya uzi huu ni kuweka utaratibu wa kuweza kupata mwanaJF bora wa mwaka hasa jukwaa la siasa, mambo ya kimataifa na mengineyo.

Mambo yafuatayo ndiyo vigezo vitakavyotumika kumpata...
1. Mwenye hoja na uchambuzi mzuri wa masuala yanayohusu taifa letu kwa ujumla
2. Anayechambua mambo ya kisiasa kwa wigo sawa bila kuegemea au kupendelea upande wowote ule, kaka ni CHADEMA au CCM au CUF yuko tiyari kukosoa kwa hoja haijarishi ni chama chake
3. Mwenye nidhamu juu ya majibu anayowapa wengine na mwenye kujibu bila kubagua au kukejeli wengine na kuwadharau au kuwatamkia matusi(makosa yanayopelekea ban)
4. Mwenye michango mingi ya kuelimisha jamii,
5. Asiye mdini au mkabila wala asiyechanbua kwa kupendelea kabila/dini yake na kukashfu za wengie,
6. Mwenye kuheshimu wengine na mamlaka ya nchi haijarishi kamchagua kiongozi aliyeko madarakan au lah.

Orodha yangu ni kama ifuatavyo, ninyi ndio mtapiga kura kwenye poll na kupata mshindi.
1. The Boss
2. Faiza foxy
3. Mzee mwanakijiji
4. BAK
5. Lizaboni
6. Pasco
7. Miss Natafta
8. victorie
9. Technically
10. Ocampor four

Haimaanishi ambao hawajawekwa hawakuchangia hapana wamechangia sana ila kwa mwaka huu hawakufika viwango vya hawa hapa

PIGA KURA YAKO.
Nikitaka kumpigia kura rala1 nafanyaje?
 
Kuna majina mengine kwenye list yako hawakupaswa kuwemo ila anaepaswa ni mmoja,kiasi kwamba wagombea wengi dhaifu sana tena ni aibu kuwakilisha JamiiForums
 
Kwa upande wa females ungeongeza mmoja maana yupo karibu kila jukwaa nahis utakuwa umembania tu kama hakuna sababu.
 
Back
Top Bottom