Hivi karibuni Februari 28, 2026 wakati wa Msiba wa Hayati Polycarp Kadinali Pengo kila mtu anakumbuka kilichotokea kuhusu suala ya kupigiwa au kutopigiwa makofi kwa wanasiasa. Baadhi ya Viongozi wastaafu walipigiwa sana makofi na waaumini lakini wale waliopo madarakani kwa sasa hali ilikuwa tofauti.
Katika tukio hilo Makamu wa Rais, Balozi Emmanuel Nchimbi akatumia nafasi yake ya kutoa neno akasema jambo lililojitokea la wastaafu kupigiwa makofi mengi ni kama deni kwa wa viongozi wa sasa.
Alichosema Makamu Rais awali: Nchimbi: Mimi hata mambo ya kugombana kivyama vyama siyapendi naona ni ujinga tu
Nchimbi aliongeza kuwa Viongozi wa sasa nao wanatakiwa kupambana ili watakapostaafu waje kupata ‘heshima’ kama waliyopata kina Kassim Majaliwa, Anna Makinda, Jaji Warioba na wengine kadhaa.
Kinachoendelea chini kwa chini
Ingawa ilionekana kama ni jambo la kawaida, ila inaelekea kuwa kuna jambo wengi hatujalijua vema.
Taarifa za uhakika ni kuwa clips za Nchimbi akizungumza kuhusu suala hilo la makofi lzilizopandishwa kwenye mitandao mingi ya kijamii na Online TVs (YouTube), muda mfupi baadae kuna baadhi ya kurasa zikaanza kushusha post hizo.
Inaelezwa kuwa watu kadhaa wamepewa kazi maalum ya kuhakikisha clips hizo zinashushwa, kisha wale wote waliokubali kushusha wakapewa kifuta jacho!
Watoa mzigo walifanya hivyo katika ‘Media’ wanazoweza kuzimudu, zile ngumu kwao wakaachana nazo.
Nani msimamizi wa utoaji wa clips hizo?
Vyanzo vya taarifa vinaonesha kwamba baadhi ya Vijana wa ‘Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii’ (JUMIKITA) ndio wanasimamia mchongo huo. Je, wanatumwa na nani? Wanapata wapi fedha za kuwalipa Watu wa online? Ili iweje?
Maswali ya kujiuliza:
Story ya Makamu wa Rais kuzungumza hadharani tena kwenye tukio kubwa kama lile na ujumbe ni mzuri inakuwaje inashushwa? Taarifa zilizopo ni kuwa kuna watu walipewa kazi ya kuhakikisha zinafutwa au kwa lugha nyepesi ya kimtandao kuhakikisha ‘zinashushwa’.
Najiuliza kwanini clip za Nchimbi zinaondolewa kwenye platforms?
Tutambue kuwa siku chache baadaye tuliona Mwigulu akitoa ‘povu’ kuhusu kupigiwa makofi. Kuna kitu kinaendelea? Muda utaamua!
Mijadala mingine:
* JAB yampa Pascal Mayala saa 24 kuthibitisha Dkt. Nchemba aliwaonea wivu Viongozi Wakuu Wastaafu kwenye msiba wa Kadinali Pengo baada ya kushangiliwa
* Dkt Nchimbi: Kuna raha yake kupigiwa vigelegele Vs Dkt. Mwigulu: wanalinganisha makofi, sijaletwa kwa ajili ya kupendwa