Ni nani hasa mmiliki wa UTT AMIS?

Ni nani hasa mmiliki wa UTT AMIS?

Historia ya UTT AMIS ilianza kutoka Umoja wa Dhamana ya Tanzania (UTT). UTT ilianzishwa chini ya Sheria ya Ushirikishwaji wa Wadhamini, Sura ya 318 na ilikabidhiwa shughuli kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na kutengeneza miradi ya uwekezaji wa pamoja; kupata na kuweka katika uaminifu hisa za biashara zilizobinafsishwa na kuhimiza utamaduni wa kuweka akiba kupitia ushiriki mpana katika umiliki wa hisa/vitengo vilivyosambazwa. UTT ilifanikiwa sana katika kuzindua mifumo ya kitengo cha uaminifu tangu mifumo mitano ya uwekezaji wa pamoja ilipozinduliwa na kuvutia wawekezaji zaidi ya 90,000 kutoka kote nchini.
Imeanzishwa na Sheria ya Bunge , na kusajiliwa Brela under TRUSTEES INCORPORATION ACT
 
Zingatia teuzi no. 1 from ikulu!
 

Attachments

  • IMG-20240806-WA0038.jpg
    IMG-20240806-WA0038.jpg
    77.5 KB · Views: 16
Kimsingi UTT ndio zile tunaita Hedge Fund Kwa US, ambao ndio wapigaji wa pesa wa Wall Street na ndio wamiliki wakubwa wa makampuni yote duniani kama Google, Amazon, Hilton, Tesla etc na Asia wako kuanzia Singapore mpaka China, tunahitaji sana makampuni kama UTT maana, capitalism ya ukweli inaanzia na makampuni kama haya ya UTT, hao wananunua share, wanachukua management then pure capitalism inayo focus kwenye profit na hakuna longo longo za ujamaa, hope tupate makampuni 1000 au zaidi kama UTT Kwa Tanzania ili uchumi ukue, bila Hedge Funds US wangekuwa kama sisi tuu, hao wakiingia mfano kwenye Agriculture wanachukua Southern yote mashamba ya mahindi wanasambaza East Africa yote au viwanda vya sukari wangeshachukua zamani sana, ila serikali inabidi iwe na very strong regulatory bodies kusimamia la sivyo gap ya maskini na tajiri itakuwa kubwa sana
 
Ni mfuko wa UWEKEZAJI WA PAMOJA ulionzishwa na Serikali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji.
.
Mfuko huu unawapa fursa wale wote ambao aidha wana pesa kidogo hivyo kushindwa kuwekeza kwenye soko la hisa, au kwenye dhamana za serikali za muda mfupi na mrefu (Treasury Bills & Bonds) au BASI TU hawana uelewa wa kutosha kuhusu mambo ya uwekezaji nao wapate mahali ambapo wataziweka fedha zao.
There is no better answer
 
Nimefuatilia sana hao UTT AMIS wanatoa faida ndogo sana , hata ukiwekeza huko ni kama umezitupa tu fedha zako , Kwa mtaji wa billion Moja utapokea gawio la milioni 60 Kwa MIEZI 6! Sasa ukiweka milioni Moja utapata Nini?
Hiyo 60m gawio la miezi 6 ni kama 12% Kwa mwaka, ni pesa nyingi sana kwenye investments, Kwa nchi zilizoendelea hiyo ni super profit, Kwa faida hiyo ukifanya re investment hiyo billion Moja itakuwa zaidi ya billion mbili (double) in 5 years, sio faida ndogo hiyo Labda kama unataka pesa za kamari
 
Back
Top Bottom