Nchi ya Tanzania inapitia kipindi kigumu sana wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Kelele, vilio, malalamiko na majonzi yametanda kila sehemu na wengi wakiwa na wasiwasi kama watakuwa salama siku zinavyoendelea kusonga.
Tumefikia kipindi ambacho mtu akiondoka nyumbani kwenda kwenye shughuli zake za kila siku, anaweka mambo kwa namna ya kurudi au kutokurudi. Matukio ya kuliabisha taifa yamepangana kila baada ya siku chache na limeanza kuonekana kuwa jambo la kawaida kwenye nchi inayoitwa "Kisiwa cha Amani".
Tangu kupotea kwa Beni Saanane; mbio za mashindano ya watekaji zimekuwa za kasi sana kiasi cha kuwaza kuna tuzo za watekaji kama zilivyolundikana tuzo za muziki, uimbaji, uchekeshaji na mambo mengine kama hayo.
Mtu kushushwa kwenye basi akachinjwa limekuwa jambo la kawaida. Mtu kupotea tu kama kuku na asionekane tena limezoeleka. Mtu kufuatwa nyumbani kwake akapigwa na akatekwa na kupelekwa huku damu zikichuruzika ni kawaida siku hizi. Mpaka tumefikia wakati hata viongozi wa dini wanapigwa kwenye nyumba zao za ibada na kutekwa bila hofu.
Ni kweli wapo watu wengi ambao wanaendelea kupaza sauti zao wakitumia mitandao ya kijamii, wakitumia mikutano ya hadhara na mikusanyiko ya nyumba za ibada. Lakini sauti yao imekuwa haifiki mbali au kudumu muda mrefu. Hii inafanya sasa tuwaze na kujiuliza swali kubwa, JE, WENYE SAUTI INAYOFIKA MBALI NA NZITO WAMEISHA?
Nashawishika kwa uzoefu wa nchi yetu kuna mtu bado hajaongea. Kuna mtu anajua aseme nini tupate ufumbuzi. Kuna mtu neno lake lina nguvu sana hata ya kukomesha ujinga unaoendelea. Kuna mtu haongei na kila anayemjua anamsubiri kwa matumaini kwamba ataongea.
Anayeandika na anayesoma wote tunawaza mtu yuleyule! Sijajua kama kuna namna ya watu kumwambia kwamba nchi inamsubiri, watanzania wanataka aongee hata kidogo. Uhakika ni kwamba akiongea tu sauti yake inafika kila sehemu na mambo ya kijinga na maigizo yanaisha.
Siku akisema tu wote tutajua kuwa kasema kama ambavyo kunyamaza kwake kumegundulika kwa kila mtu kwamba anayetakiwa kuongea yuko KIMYA.