Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ni nani huyu hapo chini?
Ikiwa unamfahamu tafadhali nitajie jina lake.
Hakuna leo anaemjua Iddi Tulio.
Picha ya Mzee Iddi Tulio nimeitafuta kwa miaka mingi na nikakata tamaa ya kuipata.
Msamaria mwema ameniletea leo.
Allah amjaze kheri nyingi.
Hivyo hapo chini ndivyo nilivyomweleza Mzee Iddi Tosili Katika kitabu cha Abdul Sykes:
Mwanzo wa harakati 1954:
''Wazee wengine mashuhuri waliomuunga mkono Nyerere walikuwa Sheikh Suleiman Takadir mwanachuoni wa Kiislamu aliyeelimika sana, akijulikana zaidi kwa jina la utani ‘’Makarios,’’ Jumbe Tambaza, mzee aliyekuwa akihodhi ardhi kubwa pale mjini; Mshume Kiyate, mzee muuza samaki aliyekuwa na kipato kizuri; Mwinyijuma Mwinyikambi, mzee aliyekuwa na viunga vya minazi na miembe; Rajabu Diwani, seremala hohehahe lakini aliyejaaliwa ufasaha mkubwa wa kuzungumza; Makisi Mbwana, kiongozi wa Wazaramo mjini Dar es Salaam; Sheikh Haidari Mwinyimvua, fundi cherehani na mtu mwadilifu; Iddi Faizi Mafongo na Iddi Tosiri ndugu wawili Wamanyema na binamu wa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Khalifa wa tariqa ya Qadiriya.
Iddi Faizi akiwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Iddi Tosiri mwanachama shupavu; Iddi Tulio, mzee mwenye heshima zake, Mashado Ramadhani Plantan, mhariri na mmiliki wa gazeti la Zuhra na kaka yake Schneider Abdillah Plantan, watoto wa Affande Plantan na wazee wengine wengi wa mjini.
Uzinduzi wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo, August 1954:
Mkutano wa uzinduzi wa TANU ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.
Mkutano wa Kura Tatu Tabora 1958:
Ujumbe wa Nyerere mwenyewe kutoka makao makuu ulikuwa na watu wengi ambao wasingeweza hata kidogo kusimama kama wagombea katika uchaguzi chini ya masharti yale.
Makao makuu ya TANU yalikuwa yanawakilishwa kwenye mkutano mkuu na Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, John Rupia, Elias Kissenge, Dossa Aziz, Julius Mwasanyangi, Michael Lugazia, Ramadhani Chaurembo, Hussein Mbaruk, Clement Mtamila, Iddi Tulio, Mzee Salum, Idd Faiz Mafongo, Idd Tosiri, Haidari Mwinyimvua na Rajabu Diwani.
Mara baada ya kurudi kutoka Tanga Nyerere aliondoka kwenda Tabora akiongoza ujumbe mkubwa sana kutoka makao makuu ndani yake wakiwemo: Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, John Rupia, Elias Kissenge, Dossa Aziz, Julius Mwasanyangi, Michael Lugazia, Ramadhani Chaurembo, Hussein Mbaruk, Clement Mtamila, Iddi Tulio, Mzee Salum, Idd Tosiri, Hadari Mwinyimvua, Rajab Diwani na wengine.
Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU iliamua kuunda kamati ya haraka haraka kwenda nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Msimbazi kumuuliza kwa nini alimshutumu Nyerere. Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo walikuwa Idd Faiz, Mwenyekiti wa Halmashauri ya TANU, Iddi Tulio na Jumbe Tambaza. Sheikh Takadir akarudia tena maneno yale yale aliyomwelezea Nyerere, neno kwa neno, akiongeza kwamba hana majuto yoyote kwa msimamo wake huo. Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Iddi Tulio walisimama na kuondoka kimya kimya. Matokeo yake ikawa Sheikh Takadir kufukuzwa kutoka TANU kwa kuanzisha suala la udini, ambalo lilidhaniwa lingewagawa wananchi. Idd Tulio akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kushika nafasi ya Sheikh Takadir.
1963:
Tarehe 11 Machi, 1963, Kamati Kuu ya TANU iliyokutana Dar es Salaam ilipiga kura kuvunja kamati ya wajumbe kumi na moja ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Idd Tulio.
Wazee walikusanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na wakasomewa uamuzi wa Kamati Kuu ya kulivunja Baraza la Wazee.
Taarifa ilisema wazee hao ni kero kwa sababu dini na siasa vilikuwa vitu viwili tofauti na hawa wazee walikuwa wanachanganya dini na siasa. Hiki kilikuwa chombo cha ushauri ambacho wajumbe wake wote walikuwa Waislam; chombo kilichokuwa ndani ya TANU ambacho kilimuunga mkono Nyerere na TANU tangu siku za mwanzo kabisa, kwanza chini ya uongozi wa Sheikh Suleiman Takadir na kisha chini ya Iddi Tulio baada ya kufukuzwa kwa Sheikh Takadir kutoka TANU.''
Huyu ndiye Mzee Iddi Tosiri.
Baada ya Baraza la Wazee wa TANU kuvunjwa wazee hawa wote wakapotea katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mzee Iddi Tosiri alikufa baada ya kugongwa na gari akivuka barabara.
Mzee Tulio alikuwa akielekea Msikiti wa Sheikh Idrissa bin Saad kusali.
Hapo hapakuwa mbali na nyumbani kwake Mtaa wa Kongo na Pemba.
TANU haikuweko katika maziko yake.