Ni nani Mmiliki Wa Blog Hii Millardayo.com?

Ni nani Mmiliki Wa Blog Hii Millardayo.com?

Habari Jf

Nimekua nikifuatilia kwa ukaribu sana habari kutoka blog mbalimbali Tanzania, mwisho wa siku nikalizishwa na kuiamini MILLARDAYO.COM kama blog inayocover habari za aina zote ndani na nje ya nchi.

Kilichonifanya kujiuliza, hii blog pendwa ni nani mmiliki wake?

nimejiuliza sana kutokana na ukimya wa blog hii huru kutokuripoti habari za tunza za EATV zilizofanyika usiku wa tarehe 10.

Vipi wakuu, mwenye uelewa wa hii blog inamilikiwa na nani ajaribu kunielekeza.
Pia inasimamia vitu gani hadi iweze kuripoti habari yako kwani kwa tukio la jana ndio lilikua tukio kubwa katika burudani hapa nchini lakini likasusiwa na millardayo kitu ambacho si kawaida yake!

Mwisho, pongezi nyingi ziwafikie East Africa Tv kwa kufanikisha EATV AWARDS 2016
Alafu wewe.una maswali ya uchochezi.uliona wapi bongo fleva ikapigwa kwenye matangazo ya vifo?
 
Clouds media bwana wanajiturumuaga kushindana na IPP kitu ambacho kiuhalisia hawawezi

Wanasahau baba ni baba tu vyombo vya habari vya IPP vikiamua vifanye utoto wanafanya kina Ruge mwezi mmoja tu tu Ruge ataomba nape awakutanishe na kina sister joy ili wayajenge beef liishe sema kule IPP wapo kiweredi zaidi sio ujanja ujanja tu
 
Kuna watu hujitokeza na kumsifia Millardayo kwamba ni miongoni mwa vijana wenye mafanikio zaidi!

Kumbe nayeye amna kitu anategemea kibarua clouds, Ninavyomuona hatakiwi kuwa muoga kiasi hiki wakati anauwezo wa kujitegemea pasi na Clouds ya Ruge.
Elimu kwa wanahabari wetu inahitajika ili waondokane na utumwa wa namna hii na kujitambua.
 
unauliza mmiliki wa dangote cement ni nani?
 
Inamilikiwa na millard ayo mtangazaji wa clouds fm,ila hii blog sio huru kama alivo mmiliki wake japo naona ni kukosa weledi tu,sawa EATV ni washindani wa clouds lakini sikutegemea kama huyo jamaa angekuwa mnazi kiasi hicho,hata habari za jide huwa haandiki,hizo ndo akili za waandishi wetu wa habari kanjanja.
Degree anayo lakini?
 
Kuna watu hujitokeza na kumsifia Millardayo kwamba ni miongoni mwa vijana wenye mafanikio zaidi!

Kumbe nayeye amna kitu anategemea kibarua clouds, Ninavyomuona hatakiwi kuwa muoga kiasi hiki wakati anauwezo wa kujitegemea pasi na Clouds ya Ruge.
Elimu kwa wanahabari wetu inahitajika ili waondokane na utumwa wa namna hii na kujitambua.
Unajua bongo unaweza ukawa unajua kitu ...lakini ukionyesha ujuaji wako mbele ya watu inakula kwako ni bora kuishi kinafiki kama watakavyo wao ili siku ziendelee.
 
Back
Top Bottom